JWTZ waigomea SERIKALI...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katika hali isiyotarajiwa,Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limegoma kutoa Madaktari kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Madaktari wanaogoma katika Hospitali mbalimbali za Rufaa, Teule na nyinginezo.

Viongozi waandamizi wa Jeshi hilo Makao Makuu wameitaka Serikali kutafuta haraka suluhu ya mgomo huo badala ya kukimbilia kwa Jeshi kwa msaada huku tatizo likibaki.

'Tumewaambia waende wakatafute suluhisho' alisema mmoja wa Maafisa Waandamizi wa JWTZ mwenye cheo cha Brigedia Jenerali. 'Hii tabia siyo njema. Tatizo halitakwisha kwakuwa Serikali itakuwa na uhakika wa huduma ingawa si rasmi' aliongeza.

Serikali ifanye nini sasa?
 
Ndio, tunataka jeshi lenye misimamo na kujua kazi yao na sio jeshi linalotumiwa kwa maslahi ya viongozi wasiofanya kazi zao. Big up wanajeshi.
 
Si wameamua kufunika funika habari ili watu wasijue impact ya mgomo huu. These people are not serious.
 
Yani naona hawa makamanda wamechelewa tena kama serikali itakaidi naomba huyo BRIGEDIA JEN ajitangaze kuwa rais mara moja ana sapoti yetu wananchi na ya MUNGU.
 
Kumbukeni nyinyi ni Jeshi letu wananchi yaani JWTZ. Katia katiba mpya nataka kupendekeza raisi asiwe amirijeshi mkuu. B unge lishike hatamu.
 
Hakuna kitu kama hicho jeshini.

Hata kama ni kweli bado huko sio kugoma bali ni kushauri na kusaidia namna ya kufikia suluhu ya mvutano wa serikali na madaktari.

Jeshi haligomi kijingajinga namna hiyo,
 
JF ya siku hizi unaweza tu ukaamka usingizini na kutunga taarifa kisha ukasema source ni mimi mwenyewe.......
 
.

huna jipya kulisingizia jeshi kwa maneno ambayo hayana chanzo cha uhakika.
Nyinyi ndio mliozoea kusoma magazetini au kusikiliza redioni.Hamjui kuwa ni sisi ndio tunaoandika na kutangaza huko.Subiri kesho au baadaye uipate kwenye 'source' uitakayo...
 
Ni afadhali nchi iongozwe na hao wanajeshi kwa mda wa 2 years 2015 cdm wachukue utawala kwa njia box.
 
Kama kweli JWTZ wamefikia hapo, saa ya ukombozi i karibu!

HAKIKA MKUU!
Jeshi letu limejishusha kabisa hadhi, vile lilivyokuwa linaburuzwa kulinda maslahi ya wanasiasa! Siwapendi na nawaona kama mavi!
Lakini kama kweli wamefikia hapo...HESHIMA KWAO.
Ila isije ikawa propaganda za siasa, kwani sikuizi zinatumika kila idara, hadi kwa waganga wa kienyeji na muuza mbege kilabuni!
Mungu wetu bado anaita!
 
Back
Top Bottom