JWTZ kusherekea miaka 52 kwa kutoa huduma bure kwa wananchi

Ohooooo ile mbinu ya maandano ya UVCCM ya Umoja wa KUmpongeza MAgufuli imeishia wapi?
Sinema linaendelea .
UVCCM wanataka kuandamana tarehe 30/31 hapa tunaongelea tarehe moja ...mbona unajitoa akili?
 
kuna hila ndani yake. tunafahamu walichopanga and they can't fool us. BTW, haki ya wananchi kuandamana na kutumia wajibu wao kikatiba September 01 uko palepale. Tutaona siku hiyo!
 
Acha wafanye ili tuwe wananchi tunaopenda demokrasia+polisi+wanajeshi...ukisikia wimbo wa parapanda italia....ICC na ICJ hawatapata tabu kuwakamata watuhumiwa
 
niliwai kusema nw ni mabaka mabaka sasa jiulize usafi utafanywa wapi kama c mitaani hahahah wanaukuta tukutane site mkiwa na maboss zenu wa ufipa
 
L Unaambiwa wanajeshi wamejifunza kuua

Wanajeshi wamefunzwa kuua sio watu tu lakini pia kuua wadudu wa maradhi ambao hujificha kwenye uchafu mitaani.Ndio maana siku hiyo watafanya usafi wa kuua wadudu wa maradhi mitaani kwa kuondoa kila aina ya uchafu mitaani
 
Acha wafanye ili tuwe wananchi tunaopenda demokrasia+polisi+wanajeshi...ukisikia wimbo wa parapanda italia....ICC na ICJ hawatapata tabu kuwakamata watuhumiwa
Mkuu wao watafanya usafi na nyie mtafanya maandamano na sisi wengine tutafanya shughuli zingine bila kuingilia shughuli ya mwenzie.

Sasa kwa hiyo mnataka nyie mfanye shughuli zenu wengine wasifanye?
 


Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) leo linaanza shamrashamra za maandalizi kuelekea siku ya maadhimisho ya 52 ya majeshi inayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu kwa kufanya usafi na upandaji miti katika kambi za jeshi na baadhi ya taasisi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa JWTZ Kanali Ngemela Lubinga aliwatoa hofu wananchi kuwa wasitishike pindi watakapoona wanajeshi katika maeneo ya karibu na makazi yao.

“Kesho (leo) tuaanza kufanya usafi kuanzia maeneo ya Kawe hadi karibu na kambi ya Lugalo, na kwamba niwatoe hofu wananchi pindi watakapoona wanajeshi wengi mitaani kwa kuwa hatuna nia mbaya hivyo wasitufikilie vibaya,” alisema.

Alisema jeshi hilo litafanya usafi pamoja na upandaji miti katika baadhi ya maeneo nchini hadi siku ya kilele cha maadhimisho hayo. Pia wanajeshi watajitolea damu salama katika hospitali za kambi za jeshi.

“Siku kuu ya majeshi itaadhimishwa pamoja na wanajeshi kujitolea damu kwenye vituo maalumu vya kutolea damu salama mikoani, katika hospitali zetu za kanda,” alisema na kuongeza.

“Sanjari na utoaji damu, madaktari wetu JWTZ watatoa huduma za tiba bure kama upimaji wa virusi vya Ukimwi, kisukari, na upimaji wa shinikizo la damu. “

“Kama ilivyo mila na desturi ya majeshi kufanya usafi na utunzaji wa mazingira, kuelekea siku ya maadhimisho tutafanya usafi na kupanda miti maeneo ya jirani na kambi na kwenye taasisi za kiraia kadri mahusiano yatakavyofanyika na taasisi hizo, ”
alisema.

Pia alisema siku hiyo ya maadhimisho itaadhimishwa kwa kuienzi michezo na kudumisha urafiki baina ya JWTZ, wananchi, na Taasisi na kwamba mashindano mbalimbali yatafanyika.

Tarehe hiyo hiyo ya Septemba 1 , Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetengaza kufanya maandamano na mikutano nchi nzima ili kulaani kile wanachokiita udikteta unaofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Tayari tangazo hilo la Chadema limepingwa vikali na Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Nsato Marijani, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Operesheni na Mafunzo huku chama hicho kikiendelea kusisitiza azma yake.

Chanzo:mpekuzi blog
 

Kwani maandamano ya UKUTA ifikapo tarehe 1 yatashindwa kufanyika kisa wanajeshi wote watakuwa brabarani wakifanya Usafi?
 
Duh hii nchi kiboko....kwahio wakati wengine wanaandamana, wengine wanafanya usafi.
 
Back
Top Bottom