zubedayo_mchuzi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2011
- 4,873
- 1,216
HAKUNA tatizo kwa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (TPDF) kuingia mitaani na kusaidia kusimamia sheria na kulinda amani.
Tatizo lililopo ni kuwa
hawajatuambia kama Jeshi
letu la Polisi ambalo ndilo
lenye wajibu wa kulinda
amani na utulivu na
kuhakikisha usalama wa raia limeshindwa kazi yake. Kuna sababu moja tu ya Jeshi (army) kuruhusiwa kuingia mitaani kushughulikia matatizo ya kiraia;
wakati Jeshi la Polisi limezidiwa au limeshindwa.
Hili ni muhimu kulielewa. Jeshi la Polisi ndicho chombo ambacho kimeundwa kisheria kushughulikia usalama wa raia na utulivu nchini.
Ndicho chombo chenye jukumu la kuzuia uhalifu, kusaka wahalifu na kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali. Ndicho chombo basi ambacho wananchi wanatakiwa kukizoea katika maisha yao linapokuja suala la usalama wa maisha, mahali, na mali
zao.
Upande mwingine Jeshi lina jukumu la tofauti sana na Polisi. Kwa vile wote wanavaa sare na wanapigiana saluti
kuna watu wanaweza
kufikiria majeshi haya mawili yanaweza kubadilishana;
Polisi wakawa Wanajeshi na Wanajeshi wakawa Polisi.
Jeshi wana jukumu kubwa la kwanza kabisa ambalo ni kulinda mipaka yetu. Mara nyingi watu wanaposikia kulinda mipaka wanachukulia kuwa ni kulinda tu mipaka pembezoni mwa nchi.
Kimsingi kulinda mipaka
maana yake ni kuhakikisha
kuwa nchi yetu inakuwapo na eneo lake linaheshimika
(territorial integrity). Katika hili ni jukumu la Jeshi kuhakikisha kuwa nchi jirani hazitishii eneo letu na hivyo
haziwezi kuchukua hata nchi moja ya eneo leo. Ndiyo maana wakati wote Idi Amin analeta chokochoko tulijaribu kwa njia nyingi za
kidiplomasia kushughulika
naye lakini alipovuka mstari kwa kuingia katika ardhi yetu ana kuidai ni yake hatukuwa na
uchaguzi mwingine zaidi ya kuhamasisha Jeshi kuingia vitani. Hii ni ile sehemu inasema kulinda nchi kutoka kwa maadui wa nje.
Lakini kuna kazi nyingine ya tofauti ya Jeshi ambayo
inahusiana na hiyo ya kwanza; kulinda nchi kutoka kwa
maadui wa ndani. Kiapo hiki cha kulinda nchi kutoka kwa maadui wa ndani hakina
maana wahalifu, vibaka au
wezi. Hii ni kazi ya Polisi.
Tunapozungumzia maadui wa ndani tuna maana wale watu ambao nao kama maadui wa nje wanatishia uhai wa Taifa letu.
Maadui wa ndani wenye
kutishia Taifa wanaweza
kuwa ni wanasiasa au
viongozi walioko madarakani.
Hii ndiyo sababu kwenye
baadhi ya nchi ambapo taasisi za kisiasa zinapokuwa zimeshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi Jeshi
linashika madaraka (kwa
mapinduzi).
Hili lilitokea Misri baada ya
kuanguka kwa serikali ya
Hosni Mubarak. Hata hivyo,
pamoja na vurugu zote
zilizokuwa zinatokea, Jeshi la Misri halikuingia mitaani kuanza kusimamia kazi za Polisi mpaka pale mchakato wa kisiasa na kimapinduzi ulipokamilika.
Jeshi la Polisi limeshindwa?
Ili tuweze kuhalalisha au labda niseme waweze kuhalalisha JWTZ kuingia mitaani na kuzunguka katika makarandinga yao ni lazima kwanza wakubali kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa.
Ikumbukwe tayari wengine
tulishajenga hoja kuwa Jeshi la Polisi ni bovu, viongozi wake wazembe, na maono yake ni ya ki CCM.
Limeshindwa kujipanga na kuwa la kisasa na limeendelea
kuwa lenye mtazamo wa
kisiasa.
Tumeshuhudia jeshi hili
lilivyogeuka kuwa adui wa
demokrasia na kuwa
kandamizi dhidi ya upinzani wa kisiasa. Matokeo yake
limekuwa na haraka kukandamiza upinzani wa
kisiasa na kuminya haki za
raia kusimama dhidi ya
serikali yao. Matokeo yake
limejiaminisha kuwa
linajukumu la kulinda watawala na si kulinda
wananchi wakitumia haki zao za kisiasa.
Hoja ya Lula wa Ndali Mwananzela,Raia mwema 24 oct 2012