Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kazi imeanza sasa. Mbunge gani huyo aliyetumbua jipu ambalo kwa hakika mimi naona limeiva.

Ila kitu kimoja ambacho amesahau ni kuwa, ikiwa hoja ni wingi wao(SIJUI KWA SENSA GANI?)basi wawatuletee sharia kabisa waanze kutukata mikono.

Huyo mbunge mimi amenifurahisha kuwa walichikuwa wakikitaka si kashi bali ni kuleta utawala wa kidini TANZANIA.

Kwa kuwa hoja kama ni kadhi sijui kama kuna mtu alikuwa analikataa, kilichokuwa kinagomna ni jinsi serikali ianzishe chombo cha waislamu badala ya waislamu wenyewe kuanzisha.

Serikali ni ya wote, Kadhi niwa waislamu, sasa serikali ndio ndio inaanzisha au waislamu wenyewe waanzishe.

Ngoja tusubiri ila naomba jina la mbunge husika.
Haki ya mtu si lazima wawe wengi, kwanini Wazanzibar wanapata mambo mangapi jee kwa idadi ya watu?
Serikali ya UK imeruhusu benki ya Kiislam kuoperate jee wewe na wenzako ikasemwa inaanzishwa benki ya waislam mtasema nini?
Waislam UK hawefiki asilimia tano bado wanafikiriwa na serikali ya Uingereza. wenzetu wanafikiri More positive, more productive.
pitia Islamic Bank of Britain.
http://news.bbc.co.uk/2/hi/uk_news/england/london/4487749.stm
 
Chadema wa UK walipotembelea Islamic Bank of Britain.
http://www.ethnicnow.com/channels/g...servatives-visit-islamic-bank-of-britain.html
Mwanakijiji kukaa kwako nchi kungesaidia kukuondoa chuki za kidini. Wenzetu wanatizama kuwa asilimia tano ya waislamu wa UK wakiwa na maisha mazuri ni faraja kwao.
leo hii ikitokea Benki ya kiislam inaanzishwa Tanzania nadhani hakutakalika.
kulikuwa na Benki ya GreenLand kwa vile owner wake alikuwa muislam ilifanyiwa fitina na kuvunjwa, wengi walikosa ajira lakini kwa vile ni muislam.
 
Mtalii
Morogoro Islamic University na Zanzibar University pia wanatoa degree ya dini hakuna anayewanyima- hata Makumira College-Lutheran pia wanatoa degree ya theology- hakuna mtu anawanyima. Wewe unapendekeza UDSM waintroduce degree za dini? Ila kama ni national priority mimi sidhani- Watz wakutaka kusoma hizo degree wanaweza kwenda Zenj, Morogoro, Arusha n.k
 
Hakuna mtu anayekataa kuwa na mahakama ya kadhi tanzania bara.. waislamu wanaweza kuunda Kadhi huyo kama Wakatoliki walivyo na Kardinali, nk... hakuna atakayewaingilia. Mwaweza kusikiliza hoja za Mhe.Shoka na Majibu ya Bi. Nagu kwenye matangazo ya leo.
 
nnaomba nielimishwe bakwata iliundwaje? maana nna tetesi kuwa serikali ilishiriki kuiunda.

na kama ni kweli kwa nn hili liwe mwiba?(mahakama za kadhi)
 
leo hii ikitokea Benki ya kiislam inaanzishwa Tanzania nadhani hakutakalika.
kulikuwa na Benki ya GreenLand kwa vile owner wake alikuwa muislam ilifanyiwa fitina na kuvunjwa, wengi walikosa ajira lakini kwa vile ni muislam.

..hamna mtu anayekataa benki kama hiyo isianzishwe!

..hivi wajua kwamba benki ya kiislam ina taratibu na masharti tafauti ya kibenki ukilinganisha na hizi za kawaida?

..hiyo greenland ya wale waganda haikuwa ya kiislam bali ilimilikiwa na waislam.halafu tuwe wakweli hapo,hao jamaa walikiuka taratibu nyingi za kibenki,ukiachilia mbali kwamba ilikuwa ikitumika kusafishia fedha chafu!

..mtalii si kila kitu lazima ukihusishe na waislam kuonewa. mtindo huu[wa wewe na wengine]unawashushia hadhi waislam!
 
KWA HILI JF SIO WAJUZI LAKINI MWAWEZA KUENDELEA NA UMASAKU WENU KAMA KAWAIDA KUONGEA HAKUNA KUTOA KODI

ILANI YA CCM YA MWAKA 2005 INASEMA JE?

Duh! kaka, sikujua kama hapa tunafanya 'umasaku' Yaani wana JF wote isipokuwa wewe!
Ukiacha jazba kidogo utagundua kuwa mtoa hoja hakuegemea upande wowote; alitoa taarifa ya kinachoendelea bila kujiweka upande wowote; wengine wakaendelea kuchangia kwa kuuliza maswali ili waeleweshwe; bahati mbaya sana hayo maswali yao yanatafsiriwa kama upinzani, hata wale waliopinga hujawatendea haki kwa kuwaambia waendelee na 'umasaku' pengine hawaelewei, unachotakiwa kufanya ni kuwaelewesha, ndio uzuri wa kubishana kwa nguvu ya hoja, unaweza ukawashawaishi wakaunga mkono hiyo hoja ya mahakama ya kadhi ikiwa utaijenga hoja vizuri; lakini usituweke wana JF wote kwenye kapu moja la "Umasaku" sio fair.

Na mimi nauliza swali;
-ni kitu gani kinakosekana katika mfumo wa mahakama zilizopo ambacho unafikiri ni muhimu kiundiwe mahakama ya peke yake?
-Je; hiyo mahakama ya kadhi itahusisha masuala ya Jinai?
na kama ndio; pale mlalamikaji na mshtakiwa wanapokuwa wa imani tofauti mmoja wao atakuwa na uhuru wa kuchagua kesi yake isikilizwe mahakama gani, au islamic law itakuwa na nguvu zaidi?
Na kama ndivyo, haki ya huyo asiye Muislam itakuwa wapi?
-katika masuala ya mirathi sheria ya Kiislam iko kinyume na sheria nyingi sana za haki za binadamu ambazo mikataba yake ya Kimataifa imesainiwa na nchi yetu; je, kwa kuipitisha hiyo sheria ya mahakama ya kadhi, nchi yetu itakuwa imejiondoa kwenye hiyo mikataba ya haki za binadamu ya Kimataifa?
-pamoja na kwamba imesemwa hapa kuwa wasio waislam hawataathirika na sheria hiyo; wewe binafsi huoni kuwa italeta mgongano katika sheria ya nchi yetu ambayo haifungamani na dini yoyote?
 
Na mimi nauliza swali;
Sawa na Utajibiwa kama ifuatavyo
-ni kitu gani kinakosekana katika mfumo wa mahakama zilizopo ambacho unafikiri ni muhimu kiundiwe mahakama ya peke yake?
Sheria inatambua kwamba kuna ndoa za Kiislamu, lazima pia kuwe na utaratibu wa kisheria wa kuvunja ndoa zilizofungwa Kiislamu, hence mahakama ya kuapili in case divorce zitakuwa zinamatata... in short mahakama za sasa haziwezi kuifanya hiyo kazi,,, iliyokwenye imani za dini ya kiislamu na kitabu chao

-Je; hiyo mahakama ya kadhi itahusisha masuala ya Jinai?
Jibu ni hapana, makosa ya jinai yatakuwa kwenye mahakama ya ki-serikali.

-katika masuala ya mirathi sheria ya Kiislam iko kinyume na sheria nyingi sana za haki za binadamu ambazo mikataba yake ya Kimataifa imesainiwa na nchi yetu; je, kwa kuipitisha hiyo sheria ya mahakama ya kadhi, nchi yetu itakuwa imejiondoa kwenye hiyo mikataba ya haki za binadamu ya Kimataifa?
Hapa ndio umasaku ulipo!, sheria zilizotungwa na kina Bush, na kupewa tafsiri zenu mnazosema ati haki za binadamu, na sheria hizi zimetungwa na walewale waliosema democracy ni vyama vingi na kuacha watu wachague serikali wanayoitaka, watu hao hao, HAMAS ilivyoshinda Palestina, wakasema hapana... so... Tafsiri za binadamu ni dhaifu huwezi kulinganisha na imani za dini ambazo ni kwamba hicho kitu ni cha Mwenyezi Mungu

-pamoja na kwamba imesemwa hapa kuwa wasio waislam hawataathirika na sheria hiyo; wewe binafsi huoni kuwa italeta mgongano katika sheria ya nchi yetu ambayo haifungamani na dini yoyote?
Haiwezi leta mgongano, ndio maana unatakiwa sheria zote zinazogongana ziweke sawa ili mahakama ya kadhi ifanye kazi yake bila kuathiri vifungu vingine vya katiba... mifano, Kenya, Zanzibar, Mozambique no case study ya kusema kulikuwa na mgongano otherwise tunaomba kama una sehemu ili tusome nasi tuelimike
 
Sheria inatambua kwamba kuna ndoa za Kiislamu, lazima pia kuwe na utaratibu wa kisheria wa kuvunja ndoa zilizofungwa Kiislamu, hence mahakama ya kuapili in case divorce zitakuwa zinamatata... in short mahakama za sasa haziwezi kuifanya hiyo kazi,,, iliyokwenye imani za dini ya kiislamu na kitabu chao

-Hata sasa iko sheria na utaratibu wa kuvunja ndoa ya kiislam ndani ya Uislam, na inatumika. Kinachoongezeka hapa ni kwamba waislam wana uwanja pmana zaidi wa kuchagua, ama kutumia sheria ya kiislam au ya kiserikali(sheria ya ndoa)
-Hapo kwenye appeal sijakuelewa. Ninavyoelewa, unisahihishe kama nakosea, katika sheria za kiislam utaratibu wa kuvunja ndoa ni mzuri na una vipengele vingi vinavyojitosheleza, hadi vya mgawanyo wa mali ambapo huko kuna 'kitoka unyumba' nk
-Mahakama zilizopo sio kwamba haziwezi kuifanyahiyo kazi kama ulivyosema; tatizo hapa ni kwamba unapopeleka shauri lako mahakamani mahakama inatumia sheria ya ndoa/mirathi ya kiserikali, lakini kwenye masuala ya ushahidi hizo element za uislam zinategemea ni nani anasikiliza kesi..hakimu/jaji mwingine anaweza kuheshimu hivyo vipengele vya taratibu za kiislam wakati mwingine anasimamia sheria ya ndoa/mitarhi inasema nini bila kujali uislam au ukristo hata kama kufanya hivyo kutaathiri; hapo inaweza kuwa na mgongano wa maamuzi kati ya mahakama moja na nyingine. Suluhisho la tatizo hili sio kuanzisha mahakama ya kadhi; kurekebisha hizo sheria ili zi-accomodate interest za pande zote inaweza kutosha.

Jibu ni hapana, makosa ya jinai yatakuwa kwenye mahakama ya ki-serikali
.

-Kwanini wakati sheria ya Kiislam ina utaratibu wa kushughulikia wakosaji wa kijinai?
-Nina hakika mahakama hii ikianzishwa kama vipengele vya kijinai havitaingizwa basi muda si mrefu kashehse litazuka. Nikiwa muislam nikimfumania mke/mume wangu nitataka sheria ya kiislam ichukue mkondo wake; polisi wakinikamata nitataka kesi yangu isikilizwe mahakama ya kadhi maana huko waislam wenzang watanielewa.

Hapa ndio umasaku ulipo!, sheria zilizotungwa na kina Bush, na kupewa tafsiri zenu mnazosema ati haki za binadamu, na sheria hizi zimetungwa na walewale waliosema democracy ni vyama vingi na kuacha watu wachague serikali wanayoitaka, watu hao hao, HAMAS ilivyoshinda Palestina, wakasema hapana... so... Tafsiri za binadamu ni dhaifu huwezi kulinganisha na imani za dini ambazo ni kwamba hicho kitu ni cha Mwenyezi Mungu

-hapo hujajibu swali langu: je, serikali yetu itajiondoa kwenye hiyo mikataba ambayo tayari imesharidhia?
usilichukulie suala hili kirahisi maana kwa kiasi kikubwa hiki ndicho kinawapa kigugumizi wakubwa, watawaambia nini mabosi wao wa nje? si unajua hatuna uhuru kamili? Imagine Asha-Rose Migiro au Getrude Mongela asimame NY aseme "Tanzania tumeamua kujiondoa kwenye 'Universal declaration of Human Rights'/African Charter On Human and Peoples Rights' etc kwasababu nchi yetu inatambua sheria za Kiislam ambazo zinapingana katika vipengele fulani fulani na vipengele vya hiyo mikataba"
Hizo sheria unazosema zimetungwa na Bush upende usipende ndio zinaongoza kula na kulala kwako hapa Tz na kokote kwingineko ingawa kwa macho yako ya kawaida huoni!

Haiwezi leta mgongano, ndio maana unatakiwa sheria zote zinazogongana ziweke sawa ili mahakama ya kadhi ifanye kazi yake bila kuathiri vifungu vingine vya katiba... mifano, Kenya, Zanzibar, Mozambique no case study ya kusema kulikuwa na mgongano otherwise tunaomba kama una sehemu ili tusome nasi tuelimike
- lakini serikali yetu imeshakataa suala zima la marekebisho ya Katiba; unless igeuze huo msimamo kwa makusudi tu ya kuweka suala la Kadhi.
-Sheria za mirathi na ndoa nazo itabidi zbadilike; pengine na nyingine nyingi ambazo sizikumbuki kwa sasa; huoni kama hiyo itakuwa kikwazo? Miaka mingi sasa sheria ya ndoa imepigiwa kelele ibadilishwe ili iende na wakati; bado bunge halijaona umuhimu; unafikiri kweli gurudumu la mabadiliko ya sheria zote hizi litafika panapostahili October mwaka huu?
 
Mimi nijuavyo diplomatically tanzania inaweka position ya waislamu na wakristo equally at 35/% each to make it 70% na dini nyingenezo the last 35% including wapagani.
Kuhusu kadhi we can say ok, lakini anayetaka suala lake liamuliwe kwa kutumia Sheria hizo asaini tu mkataba huo , maana kuna wengine waislamu lakini kutokana na mabadiliko ya Dunia wasinge penda kutumia Sheria Hizo.
Pili naommba jina la Huyo mbunge aliye ulizia hilo Jambo. ili niweze kutafakari vizuri hiyo kauli yake na yeye mwenyewe.
 
Hivi Wakristo wapo wangapi? RC wangapi? Lutheran, Anglikan? Na hao wengine? then tunaweza kuchukua total number ya 38m tokatoa Wakristo itatuta picha fulani!
How is 35% arrived at?
 
-Hata sasa iko sheria na utaratibu wa kuvunja ndoa ya kiislam ndani ya Uislam, na inatumika. Kinachoongezeka hapa ni kwamba waislam wana uwanja pmana zaidi wa kuchagua, ama kutumia sheria ya kiislam au ya kiserikali(sheria ya ndoa)
Katika sheria hiyo ya Kiislamu ndio inatambua kwamba wale watakaokuwa hawajaelewana kuhusu mgawanjo wa mirathi na n.k. watapeleka shauri lao kwenye mahakama ya kadhi.

-Hapo kwenye appeal sijakuelewa. Ninavyoelewa, unisahihishe kama nakosea, katika sheria za kiislam utaratibu wa kuvunja ndoa ni mzuri na una vipengele vingi vinavyojitosheleza, hadi vya mgawanyo wa mali ambapo huko kuna 'kitoka unyumba' nk
Swadakta, kawaida kwenye masuala haya sio kila kitu kinatakiwa kiende mahakamani lakini, pale wanandoa wanandugu wakishindana haya yanatakiwa yapelekwe mahakamani ambapo, mahakama inayotambuliwa na dini/imani hiyo ni mahakama ya kadhi. Kuappeal hapa ni kile kitendo ambacho wanafamia hamjakubaliana kwa hiyo mnapeleka mbele... mnakata rufaa mahakamani... na si kwingine bali mahakama ya kadhi

-Mahakama zilizopo sio kwamba haziwezi kuifanyahiyo kazi kama ulivyosema; tatizo hapa ni kwamba unapopeleka shauri lako mahakamani mahakama inatumia sheria ya ndoa/mirathi ya kiserikali, lakini kwenye masuala ya ushahidi hizo element za uislam zinategemea ni nani anasikiliza kesi..hakimu/jaji mwingine anaweza kuheshimu hivyo vipengele vya taratibu za kiislam wakati mwingine anasimamia sheria ya ndoa/mitarhi inasema nini bila kujali uislam au ukristo hata kama kufanya hivyo kutaathiri; hapo inaweza kuwa na mgongano wa maamuzi kati ya mahakama moja na nyingine. Suluhisho la tatizo hili sio kuanzisha mahakama ya kadhi; kurekebisha hizo sheria ili zi-accomodate interest za pande zote inaweza kutosha.

Hapa ndio watu wengi wanatoka nje ya mstari, ili mahakama ya sasa ikidhi haja ya mahakama ya kadhi, maana yake tusomeshe mahakimu Quran (maana hii ndio katiba yao). na hata hivyo haitakuwa suluhisho! waislamu wana hoja kwamba kama ndoa ilitambuliwa,,, namna ya kuivunja itambuliwe,,, na vyote viwili viko kwenye vitabu vyao... mahakama ya kadhi iko kwenye vitabu vyao.

-Kwanini wakati sheria ya Kiislam ina utaratibu wa kushughulikia wakosaji wa kijinai?
-Nina hakika mahakama hii ikianzishwa kama vipengele vya kijinai havitaingizwa basi muda si mrefu kashehse litazuka. Nikiwa muislam nikimfumania mke/mume wangu nitataka sheria ya kiislam ichukue mkondo wake; polisi wakinikamata nitataka kesi yangu isikilizwe mahakama ya kadhi maana huko waislam wenzang watanielewa.
Makosa mengi ya kijinai (hapa ni mawazo yangu) ni ya kiutendaji/utawala na kwa kuwa Tanzania sio dola ya kiislamu... Mahakama ya Ki-serikali inachukua mkondo.

-hapo hujajibu swali langu: je, serikali yetu itajiondoa kwenye hiyo mikataba ambayo tayari imesharidhia?
Kwanza sheria za dini ya kiislamu kwenye mambo ya ndoa/nirathi haziendi tofauti na hizo zinazoitwa haki za binadamu, hence hakuna haja ya kujitoka kwenye kuridhia mikataba. Only tunekuwa kwenye jinai pia huko ndio kungekuwa na tatizo ya mitazamo

Hizo sheria unazosema zimetungwa na Bush upende usipende ndio zinaongoza kula na kulala kwako hapa Tz na kokote kwingineko ingawa kwa macho yako ya kawaida huoni!

Sasa huwezi lazimisha wenye imani zao wamwamini mdhaifu George Bush.

- lakini serikali yetu imeshakataa suala zima la marekebisho ya Katiba; unless igeuze huo msimamo kwa makusudi tu ya kuweka suala la Kadhi.
Ume-missquote; wamekataa kuleta katiba mpya, marekebisho wanafanya kwa sasa yalishafikia 11
 
Na kwanini sheria za Jinai zisitumike hizo hizo za kiislamu kwa muislamu anayetaka kutumika sheria za kadhi? au ndio kuchagua iliyo bora kwako na kuacha unayo ona itakuumiza?
 
Hivi Wakristo wapo wangapi? RC wangapi? Lutheran, Anglikan? Na hao wengine? then tunaweza kuchukua total number ya 38m tokatoa Wakristo itatuta picha fulani!
How is 35% arrived at?

Ukisoma vizuri nimesema DIPLOMATICALLY inawekwa namna hiyo, ili kuondoa dhana ya Dini moja kuwa above the other.
So ukichukulia hiyo 35% ya 38 Millioni , itakuwa 13.3 millioni kwa kila kundi, lakini ikiwa wewe una data tofauti unakaribishwa, maana hapa tunajaribu kuelimishana na kufahamishana
 
Hivi Wakristo wapo wangapi? RC wangapi? Lutheran, Anglikan? Na hao wengine? then tunaweza kuchukua total number ya 38m tokatoa Wakristo itatuta picha fulani!
How is 35% arrived at?

Mzalendohalisi,

Nilimsikiliza huyu mbunge alichosema ni Zanzibar kuna waislamu wengi (>90%), na sheria hiyo inatumika, na Jaji kiongozi alikuwa mkristo na mwanasheria mkuu alikuwa mkristo na kila kitu kimeenda vizuri,,, anauliza ni tatizo gani ambalo serikali ya jamhuri ya muungano inalitia shaka kwa tanzania bara?

Kuhusu statistics,,, hakuna chombo chochote ambazo kinaweza kutupatia kwa kuwa hakuna hata siku moja sensa iliwahi ku-include mambo ya dini.
 
Full name: United Republic of Tanzania
Population: 38.4 million (UN, 2005)
Capital: Dodoma (official), Dar es Salaam (commercial)
Largest city: Dar es Salaam
Area: 945,087 sq km (364,900 sq miles)
Major languages: English, Swahili
Major religions: Christianity, Islam
Life expectancy: 46 years (men), 46 years (women) (UN)
Monetary unit: 1 Tanzanian shilling = 100 cents
Main exports: Sisal, cloves, coffee, cotton, cashew nuts, minerals, tobacco
GNI per capita: US $340 (World Bank, 2006)
Internet domain: .tz
International dialling code: +255

Hizi Data zilikuwa hapa lakini naona sasa hivi zimebadilishwa kwenye hicho kipengela cha DINI, lakini ukiwaa unaweza kupata data za miaka mingi in the summary section unaweza kupata hizo data. Eg CIA web unaweza kupata au UN
 
Back
Top Bottom