Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mzee Mwanakijiji,

Nafikiri msimamo wa JK ni mzuri. Binafsi nakubaliana na alichosema.

Mapambano ya USA na Iran ni ya kwao na afadhali sisi tukae katikati
na kufuata mikataba ya dunia. Hakuna haja ya kuingia kwenye ugomvi wa watu wengine.

Iran na Israel hawana tofauti yoyote. Mmoja ametamka dhamira yake kwa maneno na mwingine anafanya kwa vitendo kule Palestina.

Wacha sisi tukae pembeni maana hatuna nguvu ya kuamulia huo ugomvi.
 
Swala la Nyukilia ya Iran JK anajiengua na ukaribu wa west . Sina hakika kama kweli Iran imesha changia kusukuma bajeti ya Tanzania tangia JK awe Rais ila wa west they have done much already . JK anataka kutuweka hatarini . Kwani JK akikaa kimya ha hili swala hata kama alipata pesa za Kampeni huko itakuwaje ?Ndiyo maana Mogiro atapata hard time na hii issue UN . Sioni sababu ya JK kudhani kwamba ana ubavu hadi kusema haya hadharani. Nadhani hata huko Vatican hawataki kuona Iran anakuwa na Nyuklia.


JK karibu vatican lakini ujuen la kusema kule mahapa pazito pamoja na madhambi yao . Lakini pale mahala ukiitwa pale utie akili maana pale watu wamekula shule na wanakujua kiundani .

Ujumbe wa ushenzi wa kanisa langu well useme ukiweza. Ila ninawashauri wakristo wa Tanzania na hasa wakatoliki kuwapa adhabu hawa akina Pengo na Kilaini ni kuacha kutoa sadaka na michango ya ajabu .

Kanisa Katoliki ni Serikali ambayo inaenda pia kwa faida ya watu na si mpango wa kidini. Napingana na Papa wa sasa na John Paul (RIP) kwa issue ya ukimwi na condom. Najiuliza kwa nini awe naulinzi alale majimba ya dhahabu wakatoliki kibao tunakufa kwa kukosa aspirini kisa sadaka na michango ya kanisa ambayo haishi .

Amwambie Papa tunataka kujua kwa nini sisi watu wa Dar tulichanga pesa yetu kumpa Pengo zawadi kwa mategemeo kwamba atanunua pickup kwamba akionamtu kaanguka na anahitaji msaada atambeba na kumpeleka Hospitali lakini yeye akanunua RAVAL 4 short chasis na anaendeshwa na sista .

Amuulize kwa Fr.Michael ambaye sasa ni mkuu wa Mapadre wa Merryknoll Africa alifanya ushenzi pale Seminary ya Makoko na bado akapewa nafasi kubwa kama hii wakati alikuwa padre wa kawaida wa Parokia fulani na Mkurugenzi wa miito wa Jimbo la Musoma.

Amuulize kwa nini Maaskofu wanakuwa miungu watu , hadi kufikia Askofu Sanmba(RIP) kufa na maiti kusindwa kupelekwa Musoma on time kwa kuwa alikufa na sahihi akiwa signatory pekee na hivyo pesa hakuna maiti ikakaa sana Dar kabla ya mazishi.

Kuna mengi nitaishia hapa kuna ufedhuli kibao .

Juu ya safari nadhani JK anapenda kukwea mapima sasa hata akiitwa kila kona mwezi mzika yuko tayari kwenda .

JK unaenda Roma ukirudi hutaongelea Mahakama ya kadhi mimi nakueleza mapema maana unaenda kupikwa na kupewa maonyo kwa kuwa nadhani wamesha kuona kwamba unapotoka na unaendesha serikali iliyo jaa ufisadi .
 
Mwanakijiji

Je unajua jinsi gani serikali ya Iran invyoongozwa? kwa sababu maneno hayo hayakuwa official standing ya serikali ya Iran vile vile usisahau kuwa Iran kama Pakistan na Israel wote wana haki ya kuwa na Nuclear kama ambavyo Saudi Arabia,Egypt na Jordan wanavyotaka kuwa na nguvu hizo
 
DA yaani maneno ya Rais siyo Official? Je yangesemwa na na Rais wa Israel kuwa anatarajiwa kuilipua Syria na kuifuta kwenye ramani ya dunia yasingesababisha maandamano?
 
JK aende kisha awaeleze idadi ya WATANZANIA WAKATOLIKI ambao wamekufa kwa sababu ya msimamo wa VATICAN kuwaambia wafuasi wao wasitumie CONDOM hilo la MAPADRE WALAWITI awaahie hao waamerika watadela na vatican

Assumption ni kwamba wakatoliki wameambiwa wasitumie condom na wao wakakubali matokeo yake wakafa kwa ukimwi. Well and good mbona hatuambiwa kwamba wakatoliki hawa hawa waliambiwa waachane na uasherati hawakusikia? Nina tatizo na hizi reasoning. Sasa kanisa au madhehebu nyinginezo zikiruhusu matumizi ya condom nani atahakikisha kweli wanatumia?

Kama ambavyo watu wanaambiwa wasifanye zinaa wanafanya, vivyo hivyo wanaofanya wakiamua kutumia condom ni juu yao. Huwezi kusema nakatazwa zinaa sikubaliani na hilo ila nikiambiwa nisitumie condom nafuata. Naunga mkono madhehebu zinazo kataza matumizi ya condom kwani aliyeamuua kufanya zinaa anatakiwa aendelee kuwa mkaidi nakutumia condom vilevile. Do these at your peril.
 
zaidi ya yote, hivi watu wale wote wanaotumia condomu hawafi kwa Ukimwi? Je kuna walutheri, wasabato, waislamu na watu wengine ambao nao wanakufa kwa Ukimwi licha ya kuwa wao siyo wakatoliki? Je Kanisa Katoliki likiruhusu watu kutumia kondomu tatizo la maambukizi ya Ukimwi litakoma? Hivi mashoga wapo miongoni mwa viongozi wa dini Katoliki peke yake? Je kuna Walutheri mashoga? Je yule mchungaji wa Anglican ambaye alikuwa ameoa na watoto na akaamua kujitangaza kuwa ni shoga mbona watu hawakulaumu kanisa katoliki? Je kuna viongozi wa kiislamu ambao miongoni mwao wamo mashoga (kesi ya yule Shehe na mwalimu wa Madrasa walivyomfanyizia mtoto mdogo mwaka jana bila ya shaka mmeisikia!).

Je, hakuna walimu wanaoharibu watoto wetu kila siku, na viongozi wakubwa ambao wanakula vikondoo vya bwana vilivyokonda!? Je Kanisa Katoliki likitoa amri kuwa Wakatoliki wote waanze kutumia Kondomu je wakatoliki wote watakubali? wakati mwingine tufikiri kidogo kabla hatujatoa majibu ya maswali magumu ya kimaadili.
 
Mtanzania, kwa jinsi tunavyokwenda inaonekana sisi tunataka kupokea kutoka huku na kule! Ila siku moja itabidi tuchague pande!! Siku Marekani itakapoishambulia Iran, baada ya Iran kuishambulia Israel!
 
Mwanakijiji,

Binafsi sioni sababu ya kuchagua upande. Uhuru ni bora kuliko mkate wa siku moja. Kwa hili nakubaliana moja kwa moja na JK. Hatuwezi kuchaguliwa marafiki. Ugomvi wa USA na Iran sisi hautuhusu. Tuna uhuru wa kuamua nani atakuwa rafiki.

Mbona TZ hatukuunga ujinga wa Iraq je tumekosa nini?
 
naelewa kwa sababu nyerere alitumia kanuni hiyo hiyo ya kukataa rafiki zetu watuchagulie adui zetu.
 
Maswali yote hayo Asha atapambana nayo kule UN kwenye press conference yake ya kwanza (sijui lini)
 
What is the issue here? Suppose we say, he shouldn't, won't he go? Kwa nini leo tunauliza hili swali, mbona kafanya safari kibao hatukuuliza? Au upeo wangu mdogo kuna kitu kinafichwa katika hili swali?
 
mwanasiasa... we are trying to make a point..kwamba serikali yetu iko huru kufanya kazi na Vatican kama nchi nyingine. Na pointi nyingine ni kujaribu kuwadodosa wale ambao huhoji kila siku kuhusu Vatican kuwa na ubalozi wao Tanzania! (kina Mswahili wa kizazi hiki).
 
iran haina mabomu ya nuklia,haijapigana na nchi yeyotelakini jirani zake India,Pakistan yrusi na israel zaiamabomu na zote zimeshapigana na zingine zinapigana vita sasa chuki dhiidi ya irani imetika wapi mawanakiji unaelewa uyasemayo au kwa sababu marekani amesema. unaelewa kwanini marekani anapiga kelele dhiidi ya irani siyo israel pekee wako wengine soma habari kwa makini utawajua
 
Issue ya Iran ifunguliwe page . Mimi naungana na Mzee MKJJ kuipinha Iran kuwa na Nuclear .
 
Mantiki ya Kanisa Katoliki kukataa matumizi ya condom inaeleweka:inapingana na mafundisho ya kanisa hilo.Hapo hakuna mjadala.Kutumia condom inatafsiriwa na Kanisa hilo kuwa ni sawa na kuingilia process ya uumbaji ambayo ,kwa imani ya Kanisa hilo,ni strictly kazi ya Mungu pekee.Kuhusu msimamo huo wa Kanisa na kuenea kwa ukimwi,nadhani hiyo ni excuse tu ambayo watu wanataka kuitumia kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.Kanisa katoliki linakataza uzinzi kwa vile Amri ya Sita inasema "usizini".Anyway,kwa kifupi msimamo wa kanisa unatokana na imani yake.

However,kanisa hili hivi sasa limetawaliwa na unafiki uliokithiri.Nadhani watu hawapingi kanisa kukataa condom bali wanapingana na hao viongozi wa kanisa wanaokataa condom ie tatizo sio hoja inayotolewa bali watu wanaotoa hoja.Maaskofu na mapadre wetu wamebobea kwenye uzinzi,na kibaya zaidi wanatumia sadaka (wanayotuhimiza kwa nguvu kutoa kila jumapili) kuendeleza zinaa zao.Pia kanisa halijaweza kujitakasa kutoka kwenye kashfa za ulawiti.Na pindi skandali za kanisa hilo zitakapoanza kumwagwa hadharani huko nyumbani basi si ajabu likajikuta linapoteza waumini wengi zaidi.Wachambuzi wa mambo ya dini wanasema kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa makanisa ya kipentekoste ni matokeo ya disaffection ya waumini wa kanisa katoliki.
 
Back
Top Bottom