Justin Nyari ameanza mbio za kumrithi Lema Arusha

Huyu si ndio yule aliyefungwa kwa ujambazi?kweli MAGAMBA yameishiwa yani yanataka kusimamisha JAMBAZI lakini sina hofu na machalii.

Ndio huyu huyu!
Unashangaa nini? Yeye na wenzake hawana tofauti, wote majambazi, ila wanatofautiana mbinu tu za ujambazi huo. Kama wamempa udiwani watashindwaje kumteua kugombea ubunge hao magamba?

Kumbe jamaa ni jambazi la dhahabu!!!!!!!
Magamba jipangeni upya

Pia ni Mh. Jambazi, ooh sorry, ni Mh. Diwani kwa tiketi ya Magamba. Inamaana waliomchagua wanamwamini kuwa yeye ndiye Jambazi, aaah!, diwani bora!
 
Justin Nyari alishafungwa kwa kosa la jinai. Haruhusiwi kugombea.

Alishinda rufaa na akachiwa kama alivyoachiwa Aden Rage, kwa hiyo hana hatia!
Habari ni kuwa Nyari hana uwezo wa kushinda hata ndani ya CCM yenyewe.
 
Mkuu si alitakaswa na mahakama ya rufaa kama alivyotakaswa Rage.

Kumbukumbu yangu inaniambia siku Rage alipoachiwa kwa msamaha wa rais Alitimua mbio kuogopa kukamatwa tena! Nlikifurahia sana hicho kipande cha movie
 
Mahakama yamwokoa kifungo miaka 30 mfanyabiashara maarufu Arusha
Na Mussa Juma, Arusha

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Arusha, Justine Nyari, ambaye alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha na Makama ya Hakimu Mkazi Arusha, ameachiwa huru na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.

Mamia ya wakazi wa jijini Arusha, wakiwamo maafisa wa Usalama wa Taifa, polisi kawaida na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliokuwa katika magari mawili, jana walifurika katika viwanja vya Mahakama Kuu kusikiliza hukumu ya rufani hiyo.

Nyari kabla ya kutia hatiani, alikuwa ni mmoja wa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamanda wa Vijana na wa CCM Wilaya ya Simanjiro, ilikuwa nadra kwa viongozi wa kitaifa kufika Arusha bila kuonana na Nyari.

Akisoma maamuzi ya rufani hiyo yaliyochukuwa saa matatu na nusu, kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:35, Jaji Othaman Chande wa mahakama hiyo, alisema amekubaliana na hoja za mawakili wa Nyari, Loom Ojare na Medium Mwale kuwa Nyari alikuwa hana hatia.

Kazi kwako.

Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/5362-nyari-aachiwa-2.html
Kimbunga,
Ubarikiwe. Na jaji huyo akatunukiwa na magamba nafasi ya Chief Justice. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo, Mawakili wa Nyari, Mwale na Oljare walipongeza uamuzi wa Jaji Chande kuwa wa haki, lakini wakadai watakata tena rufaa dhidi ya Banjoo.

Baadhi ya viongozi wa CCM
waliokuwapo mahakamani hapo walishangilia kuachiwa huru Nyari.

Hata hivyo, Wakati hukumu hiyo ikitolewa, Nyari na Banjoo hawakuwepo mahakamani kwani Nyari bado yupo Gereza la Isanga Dodoma na Banjoo yupo gereza la Arusha.

Mawakili wa Nyari walisema kuwa Jumatatu wanatarajia kuanza utaratibu wa kumrejesha Arusha Nyari mara baada ya kupata barua ya mahakama.
 
Pia ni Mh. Jambazi, ooh sorry, ni Mh. Diwani kwa tiketi ya Magamba. Inamaana waliomchagua wanamwamini kuwa yeye ndiye Jambazi, aaah!, diwani bora!

Huyu Nyari alitolewa gerezani baada ya kutetewa kwa udi na uvumba na wakili mmoja maarufu wa Arusha, ambaye kesi zake anazotetea aghalabu ni za ujambazi wa kutumia silaha. Wakili huyo naye kwa sasa amefunguliwa kesi ya "Money Laundering" (alikutwa na pesa haramu zisizo na maelezo ya namna alivyozipata). Thread yake ipo hapa JF, itafute.
 
Na Janeth Mushi, Arusha
HATIMAYE wakili maarufu mkoani hapa, Medium Mwale anayeshtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi wa zaidi ya sh. bilioni 18 na kughushi nyaraka aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Mkoa ya Mt. Meru kwa matibabu amepelekwa mahabusu katika Gereza Kuu la Mkoa la Kisongo.
Taarifa ambazo mtandao huu umezipata zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi limefikia hatua hiyo baada ya kukamilisha taratibu za kisheria na kumkabidhi mshtakiwa huyo Magereza juzi majira ya saa 11 jioni, huku akiwa chini ya ulinzi mkali.

Taarifa zaidi zinadai baada ya taratibu hizo kukamilika Mwale alichukuliwa na kupelekwa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha lililopo eneo la Kisongo hadi hapo kesi yake itakapotajwa tena Agosti 31 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha. Juzi Wakili Mwale alisomewa mashtaka 13 akiwa wodini katika Hospitali ya Mount Meru, yakiwemo ya uhujumu uchumi, kughushi nyaraka kwaajili ya kujipatia fedha kinyume cha sheria zaidi ya Sh bilioni 18 kkwakutumia kampuni sita tofauti.

Shtaka la kwanza hadi la tatu anadaiwa kughushi Januari 6 hadi Januari 13, 2010 na kuhamisha fedha kutoka kampuni za Olive Green, Nyamao Mbeche Hollo, Gregg Motachwa, Ogembo Meetchel, John H. Adam na Mosoto O. Hoye. Shtaka la tatu hadi 13 ni la uhujumu uchumi Februari 16, 2010 kwa kuhamisha zaidi ya Sh. bilioni 1.9 kutoka kampuni ya Ogambo Chacha na Gregg Motachwa Mwita. Aidha hati hiyo ya mashtaka imedai shtaka la nne Machi 5, 2010 ni kuhamisha Dola 200,000 za Kimarekani, shtaka la tano Machi 30,2010 kuhamisha dola 159,500 za Kimarekani wakati shtaka la sita anadaiwa kulitenda Septemba 27, 2010 kwakuhamisha dola 5,500 za Kimarekani.

Inadaiwa kuwa shtaka la saba ni Novemba 2,2010 kuhamisha dola 1,246,624.84 za Kimarekani, shtala la nane Desemba 21, 2010 kuhamisha dola 416,000.02 wakati shtaka la tisa alilifanya Desemba 24, 2010 kuhamisha dola 521,000 za Kimarekani.
Shtala la kumi alilifanya Januari 17, 2011 alihamisha dola 808,000.02 za Kimarekani, shtaka la 11 Februari 9 mwaka huu alihamisha dola 527,000.02 za Kimarekani na shtaka la kumi na mbili, Julai 13, 2011 alihamisha sh. 330,000,000.

Baada ya Mwale kusomewa mashtaka hayo ambayo aliyakana yote huku wakili anayemtetea, Loom Ojare akiiomba mahakama imrudishie baadhi ya mali zake Mwale alizokuwa akizitumia ambazo zilikuwa zinashikiliwa na polisi. Baada ya maombi hayo Hakimu, Charles Magesa alitoa amri kuwa baadhi ya mali hizo ambazo hazikuorodheshwa kwenye hati ya mashtaka zirudishwe kwa Mwale ambazo ni simu na gari la kifahari la mtuhumiwa aina ya BMW lenye namba za usajili T907 BTS.
 
Medium Mwalle ndio yule wakili maarufu wa Arusha aliyekutwa na bilioni 20 yuko ndani hadi sasa kesi yake inaendelea ahaaaaa kumbe ndiye alimtoa Justin Nyari na sasa nyari atamtoa yeye.

Wahalifu wanajuana
 
Loom Ojare na Mwalle ndiyo walimtetea nyari na kumtoa gerezani lakini hivi sasa Mwalle anatetewa na Loom Ojare mmmmmhh
 
...gari hiyo ya Bwana Nyari ilikutwa na matone ya damu ya binadamu, baada ya watu hao kuuawa, na mtu anayedaiwa kufanya tendo hilo anadaiwa kuwa ni Justin Nyari!(Ni maneno yaliyotawala Arusha mwaka 2006/2007) ambapo anadaiwa kuwaua watu waliomuuzia dhahabu, ili kurudisha hela aliyotoka kuwapa!..huh!

Mbona ccm mnataka kututia majaribuni wanaArusha, tumewakosea nini?
Mnajaribu kumleta Nyari?...hakuna watu wa Intelijensia kwenye chama chenu wawacheze na kuwakataza?
Acheni hizo ccm bana, mtatulaumu wapinzani bure!

Hivi huyu Nyari si ni Diwani kwenyemoja ya Halmashauri za huko mkoani Arusha? Alipigiwa kura na nani? Au ni Diwani wa kuteuliwa?
 
Huyu Nyari alitolewa gerezani baada ya kutetewa kwa udi na uvumba na wakili mmoja maarufu wa Arusha, ambaye kesi zake anazotetea aghalabu ni za ujambazi wa kutumia silaha. Wakili huyo naye kwa sasa amefunguliwa kesi ya "Money Laundering" (alikutwa na pesa haramu zisizo na maelezo ya namna alivyozipata). Thread yake ipo hapa JF, itafute.

Mkuu Nyari alitolewa jela na Jaji Othman Chande ambaye ni Miongoni mwa Majaji Bora hapa Tanzania. Upande wa mashtaka ulikosa ushahidi usio na shaka mbele ya jaji.
 
Wanabodi.

Habari kutoka Arusha zimemtaja mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, Justin Nyari ambaye ni Diwani wa Kata ya Marerani ametajwa kuanza mikakati kuwania jimbo hilo.

Kwa sasa anasubiri rufaa ya Lema...ameona ni bora kuanza sasa kuonesha nia ya kugombea ili mchakato ukifika iwe rahisi kupiga kampeni.

CCM Arusha wanasema safari hii lazima waweke mtu makini mwenye ushawishi.

Huyu si alifungwa miaka 30 kwa ujambazi wa kutumia silaha akatoka kwa msamaha wa rais?
Nitafurahi sana akisimamishwa na ccm
 
Back
Top Bottom