Ufunuo
JF-Expert Member
- Jun 6, 2011
- 563
- 160
Mzee mwanakijiji umenena vyema Seif na Jusa wanatamaa sana wanataka kuvunja Muungano na kutengeneza wa mkata huo mkataba wanautaka na nani? wameshawauliza watanganyika kama wanataka mkataba? hizi ni hadithi za kusadikika naamini watanganyika si wajinga, wao wanataka mkataba ili kulinda rasilimali zao bara wakati watanganyika hawamiliki kitu huko visiwani, Kwa Tanganyika ni marufuku kwa mgeni kumiliki ardhi, na jambo la kwanza wakishavunja muungano katiba itamke kwa herufi kubwa ARDHI NI MALI YA MTANGANYIKA then tuone hawa ndugu zao watabeba haya majumba yao kupeleka znz? si bure wanataka mkataba wameshanusa hili, wanabore sana hawa watu binafsi sioni faida ya huu muungano. mwisho niwapongeze watanganyika wenzangu kwa kukaa kimya katika hili na tusilishabikie ili laana iwatafune wenyewe, wavunje watugawie mbao zetu, kila siku mijadala, ktk redio zao ni kero za muungano, huku wamekaa na kula kwa fedha zinazochumwa tanganyika poor Zanzibarians, niliwahi kuposti hapa ZANZIBAR HAKUNA KIONGOZI MWENYE UTHUBUTU WA KUONGOZA/KUTAWALA VISIWA HIVI BILA TANGANYIKA kwa mawazo na ueledi, wanafitna na chuki sana hawa watu kati yao, tanganyika ni kama inawanutralize siku wakitupa mgongo wanaenda kuuana.Seif Sharrif na Jussa wasikie vizuri sana;tupo ambao hatutaki Muungano "wa mkataba"! Kama wao na wale wanaowashabikia wanaona kweli Tanganyika inawanyonya na wanataka uhuru kamili njia iko rahisi kabisa.
Wawaondoe wabunge wao kwenye Bunge la Muungano; waitishe kampeni ya Wazanzibari wanaotumikia serikali ya Muungano kuachia nafasi zao (akiwemo Ghaib Bilal) na wajitangazie "uhuru wao".
Lakini la kwanza ni kwa yeye (Seif) kuacha ziara za kisiasa Tanzania bara na kuamua kuvunja CUF ili chama cha siasa cha Wazanzibari watupu kizaliwe.
Hapo ndio tutajua kweli wanataka kuwa huru. Watoke kwanza wawe na Zanzibari yao halafu ndio watuulize kama tunataka Muungano wowote na wao! Siyo watoke halafu wakati huo huo waamue aina ya mkataba wanaoutaka wao!
LET ZANZIBAR GO!