Jussa na Seif mnawachelewesha Wazanzibari kuwa "huru kamili"!

Umaarufu hauji bure jussa anatafuta umaarufu kwani hoja ya muungano tulianza kuisikia long time lakini hatuoni lolote wanalofanya bali ni kuwalisha maneno ya ujinga Wazanzibari.Mimi nafikiri Maalim na Jussa watangaze kuwa hakuna muungano kwa sasa na kuwataka waznz wote wanao kaa Tanganyika warudi kwao then wajipange upya.
 
Maalim Seif na JUssa wake ni wahuni tu wa KISIASA:
-CUF sio chama cha KIMKATABA kati yao na LIPUMBA na akina Mtatiro;
-Maalim Seif ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar. Hana MKATABA na Dr Shein;
-Jussa aliteuliwa na Kikwete kuingia Bunge la JMT. Hakuyasema haya anayoyaimba sasa hadi anamaliza muda wake;
-Baraza la Wawakilishi halina muwakilishi yeyote toka Bunge la Muungano ingawa Baraza lenyewe linao Wawakilishi watano ndani ya Bunge la JMT;
-Hotuba za Maalim Seif anapokuwa kwenye mikutano ya CUF huku bara hazisemi lolote kuhusu Muungano wa mkataba.
Kuna wabunge wengi tu wa CUF kutoka Zanzibar. Waje na hoja hii ya Muungano wa Mkataba haraka. Hili sio suala la majukwaani. Chombo pekee cha kulishughulikia hili ni BUNGE la JMT lenye wabunge wa pande zote. Wabunge ambao wana haki sawa kwa suala lolote la Muungano.
 
MM, nadhani umesahau kwamba huu ni Muungano uliopo kjwa hivyo kila mmoja ana fursa ya kutumia rasilami zizizopo. Wanachokizungumza Maalim Seif na Jussa ni wanachokitaka for the future of their country..

Kwa taarifa tu Jussa si mbunge katika bunge la Jamhuri ya Muungano , aliteuliwa na Rais kikwete Bunge lililopita.
 
Week iliyopita Maalif Seif alikuja Arusha kwa ndege/gharama za Tanganyika na kuwaambia vijana wanalewa viroba. Jana alikuwa Pemba (ulinzi kwa gharama ya Tanganyika) kuhutubia ni jinsi gani anataka Zanzibar huru na kuachana na koloni Tanganyika. Kesho Jumanne tunaambiwa atakuwa Bukoba (Tanganyika).

Hivi Maalim Seif anaamini anachosema? Afuatafuata nini Tanganyika? Kwanini asikae chini na kuandaa muswada wa kuachana na koloni? Chama chake (CUF) kina wabunge wengi toka toka Zanzibar kwenye bunge la Muungano, asiwapoge marufuku kuja Dodoma?

Hii inanikumbusha issue ya Issa Ponda Isaa, kuzuia watu wasihesabiwe while yeye mwenyewe anaacha details zake zote home, hi nayo inafanana na huyu mwishiwa!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
MM, wanataka ZNZ huru wakiwa na 'strings attached' yaani muungano wa mkataba.
Hapo ndipo ninaposema Maalim na Jusa wanauma maneno na sijui kama Wazanzibar wanjaua nini wanataka.

Jusa ni mbunge, kwa vile amejiuzulu uongozi wa CUF ili kuimarisha juhudi za ZNZ huru anapaswa pia ajiuzulu ubunge katika bunge la JMT. Akiendelea kuwa mbunge atakuwa anatafuna si maneno bali matapishi.

Maalim Seif hatakiwi kuja Tanganyika katika mikutano ya kisiasa. Kwa kauli ya ujirani mwema kama Kenya, nasi tunataka ujirani mwema hivyo siasa za CUF mwisho Chumbe. Kama ataendelea kuja katika mikutano, kwanza apuuzwe kwasababu anaongea sichokiamini na watu wasiomhusu. Pili atakuwa amekula matapishi achilia mbali kujiuma uma.

Maalimu Seif na Jusa wavunje kwanza CUF ili wawe na vyama huru vya kizanzibar halafu wavunje muungano. Kama hawawezi kuvunja CUF, wafunge midomo na kukaa kimya kwasababu wanakula matapishi yao na si kujiuma uma.

Wamwite Gharibu na wafanyakazi wote wa muungano kutoka ZNZ, watengeneze Passport za ZNZ haraka haraka na watumie Rupee au dollar kama hatua za kuvunja muungano. Wasipofanya hivyo basi wakipanda katika majukwa waiteni manafiki, vizabi zabina, warongo na wahuni.
Nguruvi3,
Jussa sio MBUNGE ni MUWAKILISHI. Aliteuliwa Ubunge na KIkwete. Muda Bunge lililopita ulipoisha akaenda kwao kugombea Uwakilishi. Alipokuwa kwenye Bunge la JMT hakuwa akiyasema haya kama ambavyo bosi wake Maalim Seif asivyosema kitu anapokuwa huku bara. Makengeza yanamdhuru JUssa kidogo. Yanampunguzia uwezo wa kufikiri vizuri.
 
Seif Sharrif na Jussa wasikie vizuri sana;tupo ambao hatutaki Muungano "wa mkataba"! Kama wao na wale wanaowashabikia wanaona kweli Tanganyika inawanyonya na wanataka uhuru kamili njia iko rahisi kabisa.

Wawaondoe wabunge wao kwenye Bunge la Muungano; waitishe kampeni ya Wazanzibari wanaotumikia serikali ya Muungano kuachia nafasi zao (akiwemo Ghaib Bilal) na wajitangazie "uhuru wao".

Lakini la kwanza ni kwa yeye (Seif) kuacha ziara za kisiasa Tanzania bara na kuamua kuvunja CUF ili chama cha siasa cha Wazanzibari watupu kizaliwe.

Hapo ndio tutajua kweli wanataka kuwa huru. Watoke kwanza wawe na Zanzibari yao halafu ndio watuulize kama tunataka Muungano wowote na wao! Siyo watoke halafu wakati huo huo waamue aina ya mkataba wanaoutaka wao!

LET ZANZIBAR GO!

Mkuu mwanakijiji hawa watu wanadhani eti sisi tunaupenda na kuung'ang'nia muungano. Pamoja na kwamba utengano ni udhaifu muungano tulionao ni udhaifu zaidi. Iwapo kutakuwa kura ya maoni ya kuwepo ama kutokuwepo kwa muungano mimi nitakuwa wa kwanza kupiga kampeni ya kutengana na watu wa visiwani kutokana ubinafsi wao uliokubuhu.
 
Seif na jussa hawajitambui hawa jamaa,wanataka kutufanya mazezeta let them go the time is now!!!!!!!!!
 
Maalim Seif na JUssa wake ni wahuni tu wa KISIASA:
-CUF sio chama cha KIMKATABA kati yao na LIPUMBA na akina Mtatiro;
-Maalim Seif ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar. Hana MKATABA na Dr Shein;
-Jussa aliteuliwa na Kikwete kuingia Bunge la JMT. Hakuyasema haya anayoyaimba sasa hadi anamaliza muda wake;
-Baraza la Wawakilishi halina muwakilishi yeyote toka Bunge la Muungano ingawa Baraza lenyewe linao Wawakilishi watano ndani ya Bunge la JMT;
-Hotuba za Maalim Seif anapokuwa kwenye mikutano ya CUF huku bara hazisemi lolote kuhusu Muungano wa mkataba.
Kuna wabunge wengi tu wa CUF kutoka Zanzibar. Waje na hoja hii ya Muungano wa Mkataba haraka. Hili sio suala la majukwaani. Chombo pekee cha kulishughulikia hili ni BUNGE la JMT lenye wabunge wa pande zote. Wabunge ambao wana haki sawa kwa suala lolote la Muungano.

Nimefikiri nakuona njia ya muongo kama si mnafiki ni fupi, mbali ya kuwa na nafasi nyingi tu za kuwasilisha hoja zao zikawa na uzito stahili tofauti zitolewapo majukwaani lakini hasirani hutoona wakichukua hatua stahiki, wao ni kusema tu huku wakijua wazi hayo ni matamko tu holela na ya kihuni kihuni. Hatujaona nia ya dhati na dhabiti ya kutaka kujitenga iwe kimkataba au vyovyote.
Japo sisi Tanganyika tumetulia tu na hizi chokochoko kwa kuwapa fursa za kujitua mzigo kwakuwa nafasi wanazo za kufanya hivyo, eti itakuwaje tukiwasaidia waondoke kabisa for good
 
Maskini Julius Mtatiro,sijui anatakuwa wapi?au ndo ukipenda unaona ......................................!
 
Utashangaa Mtikila wanamfungulia kesi za uchochezi, gazeti la Mwanahalisi likafungiwa kwa uchochezi, wananchi wengi tu wanazo kesi eti ni uchochezi lakini hawa akina Jussa, Seif na wengineo haya wayafanyayo sio uchochezi.

Labda tuseme tafsiri ya sheria zetu ina rangi na dini, lakini kama haina basi hawa jamaa wana kesi zaidi ya moja ya kujibu.

Binafsi nimefika mahali sipendi aina yoyote ya muungano kati ya Tanganyika na hawa wazenj, labda ushirikiano kama tulivyo nao na Kenya, Uganda na Rwanda ila sio zaidi ya hapo.

" mkuu ndio huo muungano wa mkataba tunaoizungumzia ati, kama wa Kenya, Uganda n.k. si tumeambiwa katika tume ya mabadiliko ya katiba tusizungumze kuuvunja muungano? ndio tumo tunatoa mawazo yetu ya "muungano wa mkataba" ili kuuboresha zaidi kwa pande zote, tanganyika na zanzibar"
 
Thank you MWanakijiji... Nafananisha Jussa na mwenzake Sefu kama wanawake wanaohangaika kuvuta sharubu za mzee waone zitakatikia wapi, dawa ni talaka tu

wangeanza kukataa marupurupu ya serikalini, wafute kabisa chochote kitokacho bara tena kwa vitendo, halafu waanze, wafanyayo sasa ni sawa na kukata tawi walilokalia, huku wakipiga ukunga kwamba wanakufaaaaaa

SIUPENDI MUUNGANO
 
Zanzibar kuondoka kwenye muungano si kitu rahisi kama kina Jussa wanavyoaaminisha wenzao. Ila katika hili mitaa ya Kariakoo kuna hoja inajengwa na wangazija pamoja na ndugu zao wa Unguja na Pemba na hoja hiyo inajengwa kwenye Historia Upogo na uzushi wa kishirikina.

Wao wanadai Zanzibar ikijitenga itakuwa na haki ya kudai miliki yake kuanzia Fukwe za Unguja, Pemba, Mombaza, Pangani, Bagamoyo, Dar es salaam na kote kule kulikokuwa kunamilikiwa na Sultani. La pili wanapandikiza chuki za kidini kwa watanganyika kwamba Muungano ni wale wanaotetea mipango ya Kanisa iliyoasisiwa na Nyerere kwa usimamizi wa Vatican. Lengo lao ni kuwaaminisha watu wa pwani kwamba wao ni sehemu ya Zanzibar ya waislamu "wenzao" na wala si sehemu ya Tanganyika ya wapagani na wakristu!!
 
Seif Sharrif na Jussa wasikie vizuri sana;tupo ambao hatutaki Muungano "wa mkataba"! Kama wao na wale wanaowashabikia wanaona kweli Tanganyika inawanyonya na wanataka uhuru kamili njia iko rahisi kabisa.

Wawaondoe wabunge wao kwenye Bunge la Muungano; waitishe kampeni ya Wazanzibari wanaotumikia serikali ya Muungano kuachia nafasi zao (akiwemo Ghaib Bilal) na wajitangazie "uhuru wao".

Lakini la kwanza ni kwa yeye (Seif) kuacha ziara za kisiasa Tanzania bara na kuamua kuvunja CUF ili chama cha siasa cha Wazanzibari watupu kizaliwe.

Hapo ndio tutajua kweli wanataka kuwa huru. Watoke kwanza wawe na Zanzibari yao halafu ndio watuulize kama tunataka Muungano wowote na wao! Siyo watoke halafu wakati huo huo waamue aina ya mkataba wanaoutaka wao!

LET ZANZIBAR GO!

MMK umeona ambako siamini kama Seif na Jusa walipaona kabla ya kuanza kampeni zao. Swali la kujiuliza: Je wako pekee yao CUF tu? Intelejensia ifanye kazi sasa ili kujua zaidi ya hapo.
 
aah nyie, wabembelezeni wenzenu angalao kidogo, kila siku wanawaambieni hawawataki na nyie mnataka kuwaachia? vibaya hivyo, wabembelezeni japo kidogo wasituache bwana, si bado tunawapendapenda eti? waambieni tutawaongezea matunzo wasituache jamani
 
Back
Top Bottom