Jussa na ajenda ya siri dhidi ya muungano

Acha ngonjera zako hizo bana, kama ni ukhabithi wa 1884 kwa nini msijiunge na Kenya au Uganda au Malawi nk nk? Mna mambo yenu myajuayo ndo maana hamtaki kuachia. Kwani kuungana unaona ni bora na Zanzibar tu. Labda Dar es salaam je Kigoma na Burundi, Kyaka na Uganda, Namanga na Kenya nk nk? Waachieni nchi yao bana tumechoshwa na malumbano ya kila mara sisi.


[
QUOTE=umsolopagaz;3679652]kwa uchungu....ningependa ajue kuwa wazawa asilia wa eneo hili la dunia tunatazamana kimahusiano nyuma zaidi kabla ya 'ukhabith" wa 1884 ambao yeye jussa anaonekana kuuona kama ni "wokovu" unaompa haki ktk eneo hili, ya kuendeleza njozi za kihabith za bismark and company...anataka kitu gani kikubwa ambacho hakipati ndani ya muungano, ambao msingi wake ni makubaliano ya viongozi wetu walioongoza harakati za kutukomboa kutoka ktk ukoloni wa kiingereza na kiarabu halikadhalika?...[/QUOTE]
 
ewe tanganyika lini utamuacha zanzibari aende zake? Kijikisiwa chenyewe kina watu 1. 3 tu..... Ya nini kikubane bane????
 
Hata z'bar ikijitenga nini kinachowauma ndugu zetu wa bara kwani kila anaedai z'bar huru nyinyi huwa adui yenu na kumpachika majina ya kiajabu na kuleta propaganda za kinyerere nje ya muungano kuna mpemba na muunguja hivi mbona haiwi nje ya muungano kuna arusha kaskazini na lindi kusini hali hiyo kwanini iwe z'bar tu ama kweli ukitaka kuwa mbaya dai chako, MUNGU IBARIKI Z'BAR.
 
Tatizo letu sisi vijana ni kukubali kutumiwa bila kuona adhari na malengo ya wanaotutumia.jussa nimekuwa nikimfuatilia maneno na vitendo vyake ni dhahiri kuwa yeye ni kati ya wanasiasa uchwara wanaoishi kwa fadhila za wakubwa.

Siamini kuwa jussa ajui adhari ya kitendo chake cha kutaka suala la watanzania wa bara kutoajiriwa katika sekta ya utalii zanzibar kama ingepita na kuwa sheria na wabara nao wakiamua yapo mambo ya ajira,bodi ya mikopo elimu ya juu umili wa ardhi n.k. ila kwa uchwara alionao leo nimejua kwa nini ulipinga bila kujua lengo la tanzania kuomba iongezewe eneo la bahari un bila kuona faida za kiuchumi kwa taifa letu.

Kwa nini alisema kufanya vibaya kwa CUF ktk jimbo la rahaleo kumpata mwakilishi tatizo ni wakristo na watanzania bara.

Nashubiri nisikie kituko kingine kutoka kwake

Mkuu Jussa hana ajenda yoyote ya siri wala hana chochote kinachoitwa ajenda.

Huyo jamaa anatekeleza aliyoagizwa kama rekodi za zamani zikiitwa HMV-His Masters Voice


Jussa ana Master wake anayemtumia.
 
Jussa hatumiwi,ukifatilia asili yake mababu zake wanatoka ukoo wa sultani mfalme...,na ndugu zake Oman wamemuahidi kuwa akifanikisha kuua muungano Zanzibar itakuwa kama Oman na yeye atakuwa ndo Rais.
 
Hawana kitisho chochote!hakuna kuwaachia!
Mkuu nyinyi ndiyo mnaofanya wazanzibar wahisi labda tuna kitu tunafaidika kutoka kwako,sisi huku kuna kila aina ya rasilimali,kikubwa ni kujipanga na kuanza maisha mapya!
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Hawa waZanzibar wakitoka kwenye huu "muungano magumashi" wataendelea kuliko sisi waTanganyika na watatuacha mbali sana.

Hiyo 1964, nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar lakini leo hii hakuna Tanganyika tena ila ni Tanzania bara na Zanzibar, kwanini Tanganyika ilikufa? Mimi naona waZanzibar wameamka sasa. Kuwe na serikali tatu (ya Tanganyika, Zanzibar na ya muungano) au tuwaachie kisiwa chao.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom