Jussa Ismail na Doyo Hassan Doyo LIVE On Star TV

Kuna thread ingine Yahya M kaanzisha..next time pitia thread zote kabla hujapost yako ku avoid kurudia post
 
Hivi ukitaka kuchangia huu mjadala unafanyaje wadau nisaidieni.
Nahitaji kuchangia sasa hivi pamoja na kumumliza jusa.
Mkuu soma thread ya Live on star tv juu ya huo mjadala uandike ujumbe wako utasomwa live!
 
Yahya muulize swali jussa. Kwa maalimu kuwa katibu mkuu wa cuf kwa miaka mingi sasa, je suala hilo halithibitishi kauli kuwa Cuf ni maalim seif na maalim seif ni cuf? Pia anaongeleaje cuf kupoteza mvuto ktk ngome zake kama ilivyo wilayan kondoa?
 
Hii tabia ya kufukuza viongozi wanaohoji mambo ya msingi ndani ya vyama inaelekea kuwa sugu ndani ya vyama. 1.Mh.Jusa na Moses Machali wanadhani kufukuzana huko kutamaliza migogoro ndani ya vyama?, 2. Utaratibu unaozungumzwa na viongozi wetu kina Machali na Jusa unawahusu tu wale wasiofungamana na viongozi wakuu? 3. Nini mstakabali wa vyama vyetu vya upinzani kwa mtindo huu wa kupunguza wabunge wetu wachache?
 
Muksini muulize huyo machali.mim ni mpiga kura wake jimbo la kasulu mjin.bunge halipo kwa sasa. Mbona hayuko jimboni?
 
Swali kwa Doyo na Jussa. Je, wanasoma maoni ya wananchi katika mitandao mbalimbali ikiwemo huu wa JF?
 
Yahya, niulizie swali kwa Jussa, nasikia Wawi, wananchi wamempelekea Ahmad Rashid, trekta lake ni kweli?
 
Yahya huyo Mmbunge wa NCCR anateka mjadala wa CUF inatosha! Apewe siku yake!
 
maalim seif na mkubali hamad rashidi ni mtu wa tama hafai kabisa good kwa kumpiga chini asiletee matatizo ktk chama
 
Yahya mada ya leo ni Mgogoro wa CUF, mbona unampa nafasi kubwa huyo Machali kumzungumzia Kafulila? Kuna hoja za msingi kuhusu CUF zinahitaji ufafanuzi.
 
1.ni kipi kinachomfanya jusa ajihisi anamamlaka sana na cuf?na nguvu hiyo anaitoa kwa wanakafu au kwa nani?mana haeleweki anaendeshwa kwa nguvu ipi?
 
Hi yahya naomba doyo atufahamishe wadau, bado anafikiri cuf inamfaa kuendelea kuwa mwanachama ikiwa akisamehewa? Au kwa sasa anafikiria nini katika mstakabari wa siasa za tanzania,
 
Jussa kumuacha maalim seif na hata lipumba kuendelea kuwa katika nafasi hizo bila kuwa na tija hamuoni kwamba ni kama mnafuata nyayo za udikteta wa muasisi wa mapinduzi yanayoitwa matukufu ya zanzibar mzee Abeid Aman Karume ambae baada ya kupata madaraka alitangaza zanzibar hakutakuwa an uchaguzi na yeye atakuwa rais wa kudumu mpaka baada ya miaka 50?
 
katika star tv,tuongee asubuhi,hoja ni mgogoro ndani ya cuf lakini yeye kapiga cm na kugeuza mjadala na kuanza kumshambulia kafulila akimuita hambiliki na pia akitumia neno'aliyekuwa mbunge wa kigoma kusini'
Imemlazimu muendesha kipindi kuikata cm yake na kuwaachia nafasi waalikwa.
 
Nimeipenda NUKUU YA WIKI inayosema "Uhuru ni Uhuru, na Mipaka ni Mipaka"...

Mpaka sasa inaonekana Viongozi wakuu wa CUF wameonesha nia ya kuwatisha kina Hamad Rashid na Doyo kwamba WANYAMAZE (wasiongelee hili kwny vyombo vya habari) kisa eti "Uhuru una Mipaka"...
Swali langu kwa Dusa ni kwamba, Ni kwanini wanatumia hoja ya "kina Hamad&Doyo kuzungumzia mambo haya kwny vyombo vya habari" kama njia ya kuwaziba midomo??..kwani si vikao vilishafanywa na sasa kila mmoja "ana Uhuru" wa kusema Anaonewa??...hawaoni wanataka kuingilia uhuru wao kikatiba.??
 
Je na kama mwanachama hasikilizwi au hoja zake hazifanyiwi kazi ndani wa vikao vya Chama nini kinatakiwa kufuata kana siyo kuongea na wanachama wenzako kupitia media ili mawazo yako yasikike?..
 
Doyo Hassani, CUF waishakufukuza sasa unaangaika kwenye Media nini unataka kusamehewa?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom