Jussa aongoza Mawaziri na wabunge Igunga

janja pwani

Senior Member
Jul 27, 2011
104
9
Naibu katibu mkuu CUF Zanzibar Ismail jussa Ladhu ameongeza msafara wa mawaziri wa CUF na wabunge wa chama hicho kuelekea igunga. Akiongea na waandishi wa habari mjini Igunga Naibu katibu mkuu Julius Mtatiro amesema kuwa tokea tuanze kampeni 13.09.2011 zilizofunguliwa na Mwenyekiti Prof Ibrahim Lipumba tumekuwa tukifanya mikutano 36 kwa siku, kutokana na timu 6 tulizokuwa nazo.

Kuanzia leo tutakuwa tukifanya mikutano 45 kwa siku, mpaka sasa tumeisha shinda tunasubiri kulinda kura kwa mgombea wetu anakubalika tofauti na wagombea wengine, amezaliwa hapa, amesoma hapa, amefanya kazi hapa, alisema kaimu katibu mkuu Julius Mtatiro.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom