Jussa ajiuzulu Unaibu Katibu Mkuu (ZNZ) ili 'kusaidia Zanzibar kupata Uhuru Wake'

Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa, muda mchache uliopita, ikielezea azma yake ya kujiuzulu nafasi hiyo. Hata hivyo, Jussa anabakia na nafasi zake nyengine kwenye Chama, ikiwemo ya ujumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, na pia nafasi yake ya kuchaguliwa na wananchi ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jimbo la Mji Mkongwe.

“Leo asubuhi nimewasilisha kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba barua ya kuomba kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar , uamuzi ambao nimeomba uanze kutekelezwa rasmi tarehe 10 Oktoba, 2012.

“Nimechukua uamuzi huu baada ya kuzungumza na kushauriana na viongozi wangu wa juu wa Chama ambao ni Mwenyekiti, Profesa Lipumba, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Machano Khamis Ali na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad takriban miezi miwili iliyopita. Nawashukuru baada ya kunitaka niwape muda wa kulitafakari walinikubalia lakini wakaniomba nibakie hadi tutakapokamilisha baadhi ya shughuli muhimu za Chama katika kipindi hichi.

“Sababu kubwa zilizonisukuma kukiomba Chama kiniruhusu niachie nafasi hii ni kutokana na muda mrefu sasa kuhisi kwamba majukumu niliyo nayo ya kuwa msimamizi mkuu wa utendaji wa Chama kwa upande wa Zanzibar na wakati huo huo kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe hakunipi fursa ya kujifaragua na kutumikia nafasi zote mbili kwa ufanisi unaotakiwa. Nataka kuona kazi ya kuibana Serikali ndani na nje ya Baraza ili iwajibike zaidi kwa wananchi inaimarika zaidi.

“Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.

“Harakati zinazoendelea Zanzibar kwa njia za amani na za kidemokrasia kwa kutumia mchakato wa Katiba Mpya zinahitaji kuungwa mkono na kupewa msukumo wa dhati na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar kwenda kusimamia maslahi yao na ya nchi yao. Nimetafakari na kuona kwamba nikiwa sina majukumu mengine ya kiutendaji nitakuwa na muda kutosha wa kulifanya hili mimi na Wawakilishi wenzangu tunaotoka CUF na CCM, vyama viwili vya siasa vilivyomo Barazani.

“Nafurahi kwamba leo nimetimiza azma yangu hiyo. Pamoja na uamuzi huu, naendelea kubaki kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

“Nawahakikishia viongozi na wanachama wenzangu wa CUF kwamba tutaendelea kushirikiana pamoja katika shughuli nyengine zote za kisiasa za Chama na kwa pamoja tutafanya kazi kuyatimiza malengo tuliyojiwekea. Naahidi kumpa ushirikiano kikamilifu mwanachama yeyote atakayeteuliwa kujaza nafasi ninayoiwacha.”

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
Zanzibar
05 Oktoba, 2012
KAFUKUZWA nafasi hiyo asitake kuzingua watu hapa..Jussa alitaka kukiharibu chama na katika hatua ambazo chama imekuwa ikizijadili kw amuda mrefu ni jinsi Jussa alivyokisambaratisha chama hasa na kuwa sababu ya lawama na mizozo mikubwa inayokikabiri chama.

Unapotaka kujiuzuru wadhifa hakuna sababu ya kufanya mazungumzo na viongozi wa chama kwa muda wa miezi miwili isipokuwa wanabadilisha tu uongozi na kumweka mtu mwingine. Unapoandika barua ya kujiuzuru unashinikiza chama kutoendelea na kazi kinyume cha mategemeo yao, hivyo kama kulitangulia mazungumzo na makubaliano basi tayari chama kimeshamwengua..
 
Kwa mbaaaaaaaaaaaali,naiona Tanganyika Yetu,isiyokuwa na Matatizo ya Uamsho nk,Hongera nenda kadai pemba yenu wawape hao wazanzibara!

hakika tanganyika nasi tunaitaka sana...hawa jamaa tumewavumilia sana.lkn ustaarabu wetu ndio ujinga wetu...watanganyika nasi tuamke tupambane kudai haki yetu ambayo viongozi wa CCM walitunyima kwa muda mrefu..jamaa tumewapa ajira kila wizara ya muungano hata kama hawana sifa...sisi tunasota barabaran...wafunguke wakabanane huko kisiwani
 
Yetu macho na masikio, baada ya miaka mitatu ya kupata katiba mpya na aje atuambie Zanzibar mpya ni ipi! Mungu atupe uzima!
 
umeshafuzu mafunzo ya bokoharamu? kama ndivyo basi mtakutana mwambani!

Habari nzuri kuliko zote kwangu ni hii ya kuvunjika kwa muungano. Haiwezekani Mkoa (Zanzibar) au mikoa (Unguja na Pemba) ukawa na hadhi ya kuungana na nchi (Tanganyika). Si waungane kwa mkataba na Mafia, Comoro, Shelisheli au Somalia? Kwanza wanatubana kwenye ajira na elimu, wakitoka hawa vijana wetu watapata fursa. Wasije wakajilaumu baadae!
 
Tungekuwa na viongozi wenye kufikiri sawa sawa huyu juha angefunguliwa kesi ya uhaini kabla ya kurejeshwa kwao Pakistani akajiunge na Talebani wenzake. Jamaa kwa kutumia masaburi kufikiri hakuna mfano. Hebu juha fikiri.Ingekuwa kwenye Pakistani mswahili angesema unayosema? Think twice.
 
Mkimaliza kutengana na Tanganyika, mtaanza kuulizana hivi wewe Jusa ni wa wapi? Mtagundua ni Mhindi flani then mtamtimua kama mbwa. Halafu mtamuuliza nawe Karume ni wa wapi? Mtagundua ana asili ya Kigoma Ujiji, mtataka naye akupisheni. Mwisho wa yote mtajikuta wote hamna asili ya Unguja wala Pemba, kumbe wengine asili yao ni Komoro, Tumbatu, Ngazija, Moroni, Mayote, Mafia, na Tanga (Tanganyika). Fanyeni fasta mtupishe, nasi Watanganyika tutawataka wanaojiita wazenji walioko huku wachague moja kati ya kurudi Zenji au kuchukua uraia wa huku.

Yaani mnarudiarudia hayo hayo utafikiri santuri mbovu iliyokwama!
 
CUF ni chama dhaifu sana chama makini na imara uongozi wa Jusa asingedumu zaidi ya masaa 24.Tangu mfumo wa siasa za vyama vingi uanzishwe sijawahi kumwona mwanasiasa mpumbavu na mshenzi kumzidi Jussa ni bahati mbaya viongozi wetu wana uwezo wa kuvumilia na kuunyamazia uhaini.
 
Huyu mbona angejiuzulu vyeo vyote? Huyu labda kuwa mchonganishi na mbaguzi tu hana jipya! Aende salama na chama chake cha UAMSHO!
 
hivi anacheo gani kwenye kile kikundi cha kigaidi kinachochoma makanisa na bar za wabara..

mkuu unamaanisha uhamsho???


jihad.jpg
 
Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa, muda mchache uliopita, ikielezea azma yake ya kujiuzulu nafasi hiyo. Hata hivyo, Jussa anabakia na nafasi zake nyengine kwenye Chama, ikiwemo ya ujumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, na pia nafasi yake ya kuchaguliwa na wananchi ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jimbo la Mji Mkongwe.

"Leo asubuhi nimewasilisha kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba barua ya kuomba kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar , uamuzi ambao nimeomba uanze kutekelezwa rasmi tarehe 10 Oktoba, 2012.

"Nimechukua uamuzi huu baada ya kuzungumza na kushauriana na viongozi wangu wa juu wa Chama ambao ni Mwenyekiti, Profesa Lipumba, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Machano Khamis Ali na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad takriban miezi miwili iliyopita. Nawashukuru baada ya kunitaka niwape muda wa kulitafakari walinikubalia lakini wakaniomba nibakie hadi tutakapokamilisha baadhi ya shughuli muhimu za Chama katika kipindi hichi.

"Sababu kubwa zilizonisukuma kukiomba Chama kiniruhusu niachie nafasi hii ni kutokana na muda mrefu sasa kuhisi kwamba majukumu niliyo nayo ya kuwa msimamizi mkuu wa utendaji wa Chama kwa upande wa Zanzibar na wakati huo huo kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe hakunipi fursa ya kujifaragua na kutumikia nafasi zote mbili kwa ufanisi unaotakiwa. Nataka kuona kazi ya kuibana Serikali ndani na nje ya Baraza ili iwajibike zaidi kwa wananchi inaimarika zaidi.

"Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.

"Harakati zinazoendelea Zanzibar kwa njia za amani na za kidemokrasia kwa kutumia mchakato wa Katiba Mpya zinahitaji kuungwa mkono na kupewa msukumo wa dhati na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar kwenda kusimamia maslahi yao na ya nchi yao. Nimetafakari na kuona kwamba nikiwa sina majukumu mengine ya kiutendaji nitakuwa na muda kutosha wa kulifanya hili mimi na Wawakilishi wenzangu tunaotoka CUF na CCM, vyama viwili vya siasa vilivyomo Barazani.

"Nafurahi kwamba leo nimetimiza azma yangu hiyo. Pamoja na uamuzi huu, naendelea kubaki kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

"Nawahakikishia viongozi na wanachama wenzangu wa CUF kwamba tutaendelea kushirikiana pamoja katika shughuli nyengine zote za kisiasa za Chama na kwa pamoja tutafanya kazi kuyatimiza malengo tuliyojiwekea. Naahidi kumpa ushirikiano kikamilifu mwanachama yeyote atakayeteuliwa kujaza nafasi ninayoiwacha."

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
Zanzibar
05 Oktoba, 2012

KWA NINI OCTOBER 10 Sio IMMEDIATELY ???? MBAGUZI HUYOO...
 
Back
Top Bottom