Jumuiya ya Kikristo yamtaka Kikwete ataje viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya

Kuna mchungaji mmoja aliwahi niambia kuwa, 'pale magogoni kwa sasa, pana koti lililowekwa kwenye kiti cha urais mpaka hapo taifa hili litapopata rais'. Hii ilikuwa ni baada ya jk kaulikwa na kuongea kwenye mkutano wa wachungaji wa kilutheri, kama miaka mitatu hivi iliyopita.
Sikua nimeipata kwa kina maana halisi ya maneno ya mchungaji yule, ila kwa sasa ndio nimeyatambua.

Unataka kusema nini hapa wakati taarifa ni za huko majuu. Hivi tukianza kuleta taarifa za masheikh wa Afghanistan na biashara ya madawa ya kulevya, na Morroco kuongoza kwa uzalishaji wa mirungi; Habari za silaha kufichwa msikitini huko Iraq na masheikh huko Pakistan kuandamana kulaani kifo cha gaidi namba moja duniani Osama bin laden tutafika kweli. Waalimu wa madrassa kulawiti nk.
Hivi tukianza hivyo badala ya kuongelea tatizo alilosababisha rais kuwasema vibaya wakatoliki tutafika wewe Faiza Foxy?.

Mkuu achana na hizo habari Wakatoliki wana mengi sana

Tukiwaambieni Jakaya Mrisho Kikwete Mdini watu humu jamvini mnaona kama tunamwonea,this fool has ****ed this country and now is looking for a scapegoat na kwa akili yake ndogo anafikiri atawasaidi au kuwavutia Waislam kwa kuwabagua Wakristo anajilisha upepo sababu Waislam na Wakristo wa leo hawawezi pumbazwa na siasa muflisi za kiongozi aliyechoka kiafya na kiakili kama yeye ambaye hata hajui kwanini aliutaka urais wala hajui kwanini nchi na wananchi wake ni maskini.

May you please try to tone down your rhetoric else it gonna cost you an arm and leg. Gentleman you can drive point home without name calling, Jakaya is but a human being afterall not some Angel Gabriel.

kwa kweli hizi habari ni udhalilishaji mkubwa sna kwa wakristu wote,naungana na wanajamvi kwamba tatizo ni washauri wake,then anatakiwa awapatie Maaskofu wote hio list yake ili nao wajue ukweli wa kauli yake vinginevyo ni jambo la fedheha kubwa sna !!!

Kujisaidia ajisaidie kuku akijisaidia bata ameharisha haya Bwana Raisi we2 mwehu.ila kumbuka haya ni Mawazo tu ila kuomba msada kwa viongoz wa dini ni dharau,kazi zao ni nini hawa viongoz wa dini acheni ubata ninyi! Kama hafai msiwage mnamualika kny Kusimika Maaskofu kwani aliomba huo mualiko Mbona Waislam Hawamwaliki.?kwani raisi ni Nabii bwana! Mnaumiza vichwa bure.kama mnaweza mwambieni Kamanda wa Jesh afanye mapinduz Unadhani hapa ni Baa na hayo mawazo yenu ya Kipopompo.KWANI HAMJUI MADAWA YAKULEVYA YAPO MIJINI NA MITAANI HUMU?!

Viongozi wa dini wamekuwa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya siku hizi?! na polisi wana kazi gani?

Naona kibaraka FF kakimbia, na wenzake wakina Mjepu siwaoni.
wapuuzi sana hawa, wanataka kutuona sisi mafala.
huyu FF ninae tu! hadi tukaangane maini siku moja.

Mkuu achana na hizo habari Wakatoliki wana mengi sana
mengi manini?
kulia lia tu ndo anaweza. we need some action bana! anakuwa kama anakwenda hii makitu!:majani7: anaropoka tu, hata unashindwa kujua aliyeongea ni nani, rais au msela wa mwembe yanga

Duuh!! Sasa hawa wana uhusiano gani na Tanzania?!!
You should try harder next time!

Naona kibaraka FF kakimbia, na wenzake wakina Mjepu siwaoni.
wapuuzi sana hawa, wanataka kutuona sisi mafala.
huyu FF ninae tu! hadi tukaangane maini siku moja.

mkuu hebu jiulize tafsiri ya foxy katika lugha ya kawaida

Na kama hiyo haitoshi na tuchukulie kama mnavyosema nyinyi, basi labda Kikwete alisoma habari hizi:

http://www.ivanfoster.net/pdf/Dec9909.pdf

http://www.bluelight.ru/vb/showthread.php?t=489038

Police find that 'holy sand' was drugs - CNN

Priest Charged With Dealing Drugs out of U. of Illinois Student Center - Graduate Students - The Chronicle of Higher Education

Priest Charged With Dealing Drugs out of U. of Illinois Student Center - Graduate Students - The Chronicle of Higher Education

Jisomee mwenyewe uone wachungaji wakifanya nini. Cha kushangaza ni nini? kwani hao wachungaji si binaadam?

***** akilin weye,hadithi za ndoto za giza na uhuni wa hawala yako jk.kamataa mharifu funga,msilete mambo ya kishoga shoga ktk jamii.wehu nyie.

Tukiwaambieni Jakaya Mrisho Kikwete Mdini watu humu jamvini mnaona kama tunamwonea,this fool has ****ed this country and now is looking for a scapegoat na kwa akili yake ndogo anafikiri atawasaidi au kuwavutia Waislam kwa kuwabagua Wakristo anajilisha upepo sababu Waislam na Wakristo wa leo hawawezi pumbazwa na siasa muflisi za kiongozi aliyechoka kiafya na kiakili kama yeye ambaye hata hajui kwanini aliutaka urais wala hajui kwanini nchi na wananchi wake ni maskini.

May you please try to tone down your rhetoric else it gonna cost you an arm and leg. Gentleman you can drive point home without name calling, Jakaya is but a human being afterall not some Angel Gabriel.

wachungaji wenyewe mnaowatetea si ndiyo hawa? hebu oneni huyu hapa chini, watashindwa kuuza madawa kweli?

BREAKINGNEWZzzzzzzzzzzz NI SIKU ZA MWISHO!!?? MCHUNGAJI KKKT AFUNGWA JELA MVUA SITA KWA RUSHWA YA NGONO...

MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa leo imemhukumu kwenda jela miaka sita jela mwalimu wa shule ya sekondari ya Pomerini wilaya ya Kilolo mkoani hapa Michael Ngilangwa mchungaji wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Njombe kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake.

hii ni kwa mujibu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima tarehe 6/6/2011

Haya ndio aliyoyaeleza, kipi kibaya hapa?:

Tuesday, May 31, 2011

VIONGOZI WA DINI NA TAASISI SAIDIENI SERIKALI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA - JAKAYA KIKWETE

1863000103.jpg
Rais Jakaya Kikwete, ametangaza kuwa ataunda chombo maalum cha kupambana na ongezeko kubwa la tatizo kubwa la biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Aidha, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini na taasisi za dini nchini kusaidiana na Serikali katika kupambana na tatizo hilo lenye madhara makubwa kwa jamii, na hasa miongoni mwa vijana ambao wanaunda asilimia 60 hadi 80 ya Watanzania wanaotumia dawa za kulevya ambazo zinaharibu mwili na akili ya mtumiaji.

Vile vile, Rais amesema kuwa wakati ni kweli kuwa mikoa yote ya Tanzania inakabiliwa na tatizo hilo, lakini ni mikoa saba inayoongoza kwa kuwa na tatizo kubwa zaidi ikiwa ni Dar es Salaam, Mwanza, Mjini Magharibi – Zanzibar, Arusha, Tanga, Mbeya na Dodoma.

Rais Kikwete alitangaza kusudio lake la kuunda chombo maalum cha kupambana na dawa za kulevya jana wakati wa sherehe za kusimikwa kwa Askofu Mteule Albert Jella Randa wa Kanisa la Mennonite, Tanzania, kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mwanza ambako alikuwa mgeni.

Sherehe hizo zilifanyika kwenye makao ya Dayosisi hiyo Nyakato, mjini Mwanza.

Akihutubia mamia ya waumini wa Kanisa hilo pamoja na wananchi wengine waliohudhuria sherehe hizo, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini, madhehebu ya dini mbali mbali nchini kuongeza juhudi za kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Akisema kuwa pamoja na kwamba matunda ya juhudi za Serikali katika kupambana na tatizo hilo yameanza kuonekana bado kazi iliyoko mbele ya jamii ya Tanzania ni “kubwa sana”.

“Mwaka jana, 2010, watu 12,119 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Katika kipindi hicho, dawa za kulevya zilizokamatwa ni heroine kilo 190 na gramu 780, cocaine kilo 65, morphine kilo 11, bangi kilo 279,520 na mirungi kilo 10,317. Takwimu zinaonyesha kuwa mkoani Mwanza tatizo linakua kwa kasi sana,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Dawa za kulevya zina madhara makubwa kwa watumiaji na kwa jamii. Kwa watumiaji hatima yake ni mtu kuharibikiwa kimwili na kiakili. Watu huwa mazezeta na hivyo kushindwa kutokuwa na manufaa kwa jamii. Hii ni hasara kwa familia, jamii na taifa. Bahati mbaya sana waathirika wengi ni vijana. Tafiti zilizopo zinaonyesha kwamba asilimia 60-80 ya watu wanaotumia dawa hizo ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 30, alisema.”

Aliongeza: “Hii ni hasara kubwa kwani vijana ndio nguvukazi ya leo na kesho. Ndiyo roho ya taifa na warithi wa familia, jamii na taifa. Wakiharibikiwa taifa letu litaangamia. Tusikubali. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kulichukia tatizo hili na kulikemea kwa nguvu zake zote ili kuokoa taifa letu. Nawaomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali na watu wote wenye mapenzi wa nchi yetu kupambana mpaka tufanikiwe kudhibiti na hatimaye kulitokomeza tatizo hili.”

Sherehe za leo za kusimikwa Askofu Randa (50) kuwa Askofu wa Kanisa Mennonite, Jimbo la Mwanza, pia zilihudhuriwa na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa hilo na wananchi wengine.

Kwenye sherehe hizo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), Mhashamu Severin Watson Mang’ana amemkabidhi askofu huyo mpya nguvu kuu ishara za mamlaka na madaraka ya uaskofu ikiwamo Biblia, Katiba ya KMT, Cheti cha Uaskofu na vitabu vya taratibu ya kuendesha ibada za Kanisa hilo na nyimbo.

Kanisa la Mennonite lililoanzishwa duniani mwaka 525 na Mchungaji Menno Simon mjini Zurich, Uswisi, liliingia nchini miaka 77 iliyopita mwaka 1934 na liko katika maeneo yote ya Tanzania isipokuwa Zanzibar, Ruvuma na Pwani. Kanisa hilo lina makao yake mkoani Mara.

Source: Maganga One.: VIONGOZI WA DINI NA TAASISI SAIDIENI SERIKALI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA - JAKAYA KIKWETE
Last edited by FaizaFoxy; Today at 06:13 PM.

Source ni Tanzania Daima, msemaji Kikwete? halafu hata hiyo link uliyoweka haifunguki. Iweke sawa tuipitie.

Haya soma hapa chini....

JK awapasha viongozi wa dini
• Asema wapo wanaouza dawa za kulevya

na Stephano Mango, Songea

RAIS Jakaya Kikwete, amewaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini kuacha tabia ya kushiriki biashara ya kuuza dawa za kulevya na badala yake washirikiane na viongozi wa serikali kuidhibiti biashara hiyo haramu.

Alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga wakati wa ibada maalumu ya kupewa daraja la uaskofu na kusimikwa kwa askofu wa jimbo hilo, Mhashamu John Ndimbo, katika kanisa la kiaskofu la Mtakatifu Killian iliyohudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa.

Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakishiriki kufanya biashara hiyo ya dawa za kulevya kwa kuwatumia vijana ambao huwafanyia mipango ya kuwatafutia hati za kusafiria (Passport) kwenda nchi za nje.

Badala yake Rais Kikwete amewataka viongozi hao nchini kuikemea biashara hiyo na kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola katika kuhakikisha biashara hiyo inakomeshwa kwa kuwafichua wahusika wanaoifanya ili wachukuliwe hatua za kisheria.

"Inasikitisha sana na kutisha, biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili kwani baadhi yenu tumewakamata.

"Kwa kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususan vijana waweze kuepuka na matumizi ya dawa hizi," alisema Rais Kikwete.

Ameyaomba pia madhehebu ya dini nchini kuweka mipango endelevu ya maendeleo ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika mipango yao ya kimaendeleo ili kuisaidia jamii katika ushindani wa soko la ajira. Alieleza kuwa kutokana na wananchi wengi kukabiliwa na tatizo kubwa la ajira ni vyema sasa serikali kwa kushirikiana na madhehebu ya dini kujikita zaidi katika kujenga vyuo vya ufundi ambavyo vitasaidia kupunguza kero iliyopo ya ukosefu wa ajira hususan vijana wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari.

"Kufanikiwa kwa viongozi wa dini katika shughuli za kimaendeleo ni faraja kwa serikali iliyo madarakani na Watanzania wote kwa ujumla," alisema Rais Kikwete.

Awali Rais wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki, Tanzania, Askofu Yuda Thadei Ruwa'ichi, aliiomba serikali kuwa makini wakati wa kuandaa bajeti ya nchi ambayo inatarajiwa kupitishwa bungeni hivi karibuni.

Alisema bajeti hiyo ni vyema izingatie maendeleo ya Watanzania ambao wengi wao ni maskini. Aliishauri pia serikali kudumisha amani na utulivu nchini kwa kuhakikisha wakati wote vitendo vya vurugu havipewi nafasi kamwe na kwamba kanisa Katoliki litaendelea kushirikiana na serikali na Watanzania wote bila ubaguzi wa rangi, dini au ukabila.

Naye Askofu Ndimbo baada ya kusimikwa alitoa shukurani zake kwa Rais Kikwete na waumini wa jimbo hilo na kuahidi kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Askofu huyo alisema kuwa kazi yake kubwa ni ya kuwachunga kondoo wa Mungu (waumini) pamoja na kuwahamasisha kujikita katika kilimo cha kisasa ambacho kitawasaidia kupunguza ukali wa maisha.

source: Tanzania Daima 6th June 2011

''Ni keherehere chao, sikuwatuma kunialika. Mi na familia yangu twaropoka tu hatuogopi''

Rais wetu anapenda sana kuangalia movie za kibongo...hapa alikua anakumbushia ile movie ya FAKE PASTERS...

we fox sijajua hasa kwa nini unatetea upuuzi but sikulaumu sana ndo kawaida yenu.

Rais Kikwete: Viongozi wa dini acheni biashara dawa za kulevya

Na Gideon Mwakanosya
6th June 2011

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mhashamu John Ndimbo, askofu mpya wa Jimbo katoliki Mbinga wakati wa ibada ya kumsimika askofu huyo iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Kilian mjini Mbinga leo.

Rais Jakaya Kikwete amepasua jipu mbele ya viongozi wa dini kwamba kuna baadhi yao wanashiriki biashara haramu ya dawa za kulevya.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga jana katika ibada maalum ya kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo wa jimbo hilo, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Killian, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao kuacha biashara hiyo na badala yake washirikiane na viongozi wa serikali katika kuidhibiti.

Katika ibada hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Kikwete, alisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara hiyo kwa kuwafanyia mipango vijana ya kuwatafutia hati za kusafiria kwenda nchi za nje kwa shughuli hiyo.

Rais Kikwete aliwataka viongozi hao kukemea biashara hiyo na kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola ili kuikomesha kwa kuwafichua wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.

" Inasikitisha sana na kutisha; biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, Taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili, baadhi yenu tumewakamata," alisema Kikwete na kuongeza kuwa:

" Kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususani vijana waweze kuepukana na matumizi ya dawa za kulevya."
Aliyaomba madhehebu ya dini katika mipango yao ya maendeleo yaweke kipaumbele kujenga vyuo vya ufundi stadi ili kuisaidia jamii katika ushindani wa soko la ajira.

Alifafanua kuwa kutokana na wananchi wengi kukabiliwa na tatizo la ajira, ni vyema sasa serikali kwa kushirikiana na madhehebu ya dini kujikita zaidi katika kujenga vyuo hivyo ambavyo vitasaidia kupunguza kero hiyo.

" Kufanikiwa kwa viongozi wa dini katika shughuli za kimaendeleo ni faraja kwa serikali iliyopo madarakani na Watanzania wote kwa ujumla, " alisema.

Kwa upande wake, Rais wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki Tanzania, Askofu Yuda Thadei Rwaichi, aliiomba serikali kuwa makini wakati wa kuandaa bajeti ya nchi.

Askofu Rwaichi, alisema bajeti hiyo ni vyema izingatie maendeleo ya Watanzania ambao wengi ni maskini.

Pia aliitaka serikali kudumisha amani na utulivu, kwa kuhakikisha vitendo vya vurugu havipewi nafasi na kwamba kanisa Katoliki litaendelea kushirikiana na serikali na Watanzania wote bila ubaguzi wa rangi, dini au kabila.

Pamoja na mambo mengine, Askofu mpya wa Jimbo la Mbinga, Ndimbo, baada ya kusimikwa alitoa shukurani zake kwa Rais Kikwete na waumini wa jimbo hilo kuwa katika uongozi wake atakuwa bega kwa bega kuhakikisha anashirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hata hivyo, Askofu Ndimbo, alisema kazi yake kubwa ni ya kuwachunga kondoo wa Mungu (Waumini) na kuwahamasisha waumini wa jimbo hilo kujikita katika kilimo cha kisasa ambacho kitawasaidia kupunguza ukali wa maisha.

CHANZO: NIPASHE

Sasa hapo kuna udini upi? kaweka wazi kinaga ubaga kuwa baadhi yao "tumewakamata", hasira yenu mpaka mjuwe ni nani sio?

Sasa, naomba mgoogle kidoogo, muone "watumishi wa mungu" wanavyofanya madudu duniani si haya ya madawa ya kulevya ambayo nimewabndikia sources huko juu, tafuteni mtakuta wanaooana jinsia moja, wanaoharibu watoto wadogo, wanaoolewa, wanaoowa na tunae mpaka hapa Tanzania aliyekuwa padri tena msomi wa kanoni (sina haja ya kumtaja jina) ambae kaowa! sasa kanisa linamruhusu padri aowe? halafu kabla hajaacha anakaa na mke wa mtu, sasa kanoni ndio ilimruhusu hayo mambo machafu?

Mnataka kusema nini nyinyi?

kwa kweli hizi habari ni udhalilishaji mkubwa sna kwa wakristu wote,naungana na wanajamvi kwamba tatizo ni washauri wake,then anatakiwa awapatie Maaskofu wote hio list yake ili nao wajue ukweli wa kauli yake vinginevyo ni jambo la fedheha kubwa sna !!!

Hivi yeye yuko Ikulu kushauriwa tu, hana brain yakuchambua mwenyewe mpaka sasa? In other words ina maana kila anachoambiwa anakichukua hivyo hivyo bila kufikiri??? I do not believe in a second. What about a different theory " ana-washauri wazuri lakini si msikivu".

Back
Top Bottom