Jumuiya ya Kikristo yamtaka Kikwete ataje viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya

huyu ndo rais tuliyenaye!huwa namshangaa sana vitu anavyoongea!UDINI aliuasisi yeye.ameona wananchi wamemdharau hasa christians leo anataka kuwafanya viongozi wa kikristu kunyoosheana vidole!ana hila ya kuwagawa.ana tabia za ajabu ajabu.ni mfitini sana.Akiwa kama rais wa nchi anatakiwa aongee mambo kwa uhakika na afanyie kazi anachokisema sio upupu anaoutoa!SHAME ON HIM
 
Duh mimi ni silent observer. Wote hapo juu mmeongea vitu vizito (kasoro FF) na nakubaliana na hoja zenu wakuu

Mimi sikuongea, nimeweka hiyo habari inayoongewa. Usitie maneno ya mwingine kinywani mwangu, na source nimeiweka, heee babuwee unanini?
 
Haya ndio aliyoyaeleza, kipi kibaya hapa?:

Tuesday, May 31, 2011

VIONGOZI WA DINI NA TAASISI SAIDIENI SERIKALI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA - JAKAYA KIKWETE


Rais Jakaya Kikwete, ametangaza kuwa ataunda chombo maalum cha kupambana na ongezeko kubwa la tatizo kubwa la biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Aidha, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini na taasisi za dini nchini kusaidiana na Serikali katika kupambana na tatizo hilo lenye madhara makubwa kwa jamii, na hasa miongoni mwa vijana ambao wanaunda asilimia 60 hadi 80 ya Watanzania wanaotumia dawa za kulevya ambazo zinaharibu mwili na akili ya mtumiaji.


Vile vile, Rais amesema kuwa wakati ni kweli kuwa mikoa yote ya Tanzania inakabiliwa na tatizo hilo, lakini ni mikoa saba inayoongoza kwa kuwa na tatizo kubwa zaidi ikiwa ni Dar es Salaam, Mwanza, Mjini Magharibi – Zanzibar, Arusha, Tanga, Mbeya na Dodoma.

Rais Kikwete alitangaza kusudio lake la kuunda chombo maalum cha kupambana na dawa za kulevya jana wakati wa sherehe za kusimikwa kwa Askofu Mteule Albert Jella Randa wa Kanisa la Mennonite, Tanzania, kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mwanza ambako alikuwa mgeni.


Sherehe hizo zilifanyika kwenye makao ya Dayosisi hiyo Nyakato, mjini Mwanza.


Akihutubia mamia ya waumini wa Kanisa hilo pamoja na wananchi wengine waliohudhuria sherehe hizo, Rais Kikwete amewaomba viongozi wa dini, madhehebu ya dini mbali mbali nchini kuongeza juhudi za kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.


Akisema kuwa pamoja na kwamba matunda ya juhudi za Serikali katika kupambana na tatizo hilo yameanza kuonekana bado kazi iliyoko mbele ya jamii ya Tanzania ni "kubwa sana".


"Mwaka jana, 2010, watu 12,119 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Katika kipindi hicho, dawa za kulevya zilizokamatwa ni heroine kilo 190 na gramu 780, cocaine kilo 65, morphine kilo 11, bangi kilo 279,520 na mirungi kilo 10,317. Takwimu zinaonyesha kuwa mkoani Mwanza tatizo linakua kwa kasi sana," amesema Rais Kikwete na kuongeza:


"Dawa za kulevya zina madhara makubwa kwa watumiaji na kwa jamii. Kwa watumiaji hatima yake ni mtu kuharibikiwa kimwili na kiakili. Watu huwa mazezeta na hivyo kushindwa kutokuwa na manufaa kwa jamii. Hii ni hasara kwa familia, jamii na taifa. Bahati mbaya sana waathirika wengi ni vijana. Tafiti zilizopo zinaonyesha kwamba asilimia 60-80 ya watu wanaotumia dawa hizo ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 30, alisema."


Aliongeza: "Hii ni hasara kubwa kwani vijana ndio nguvukazi ya leo na kesho. Ndiyo roho ya taifa na warithi wa familia, jamii na taifa. Wakiharibikiwa taifa letu litaangamia. Tusikubali. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kulichukia tatizo hili na kulikemea kwa nguvu zake zote ili kuokoa taifa letu. Nawaomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali na watu wote wenye mapenzi wa nchi yetu kupambana mpaka tufanikiwe kudhibiti na hatimaye kulitokomeza tatizo hili."


Sherehe za leo za kusimikwa Askofu Randa (50) kuwa Askofu wa Kanisa Mennonite, Jimbo la Mwanza, pia zilihudhuriwa na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa hilo na wananchi wengine.


Kwenye sherehe hizo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), Mhashamu Severin Watson Mang'ana amemkabidhi askofu huyo mpya nguvu kuu ishara za mamlaka na madaraka ya uaskofu ikiwamo Biblia, Katiba ya KMT, Cheti cha Uaskofu na vitabu vya taratibu ya kuendesha ibada za Kanisa hilo na nyimbo.

Kanisa la Mennonite lililoanzishwa duniani mwaka 525 na Mchungaji Menno Simon mjini Zurich, Uswisi, liliingia nchini miaka 77 iliyopita mwaka 1934 na liko katika maeneo yote ya Tanzania isipokuwa Zanzibar, Ruvuma na Pwani. Kanisa hilo lina makao yake mkoani Mara.

Source: Maganga One.: VIONGOZI WA DINI NA TAASISI SAIDIENI SERIKALI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA - JAKAYA KIKWETE

http://magangaone.blogspot.com/2011/05/viongozi-wa-dini-na-taasisi-saidieni.html
Kuna mengine aliyosema zaidi ya haya, nimepita mstari kwa mstari sioni mokiwa anataka nini hasa
 
Tukiwaambieni Jakaya Mrisho Kikwete Mdini watu humu jamvini mnaona kama tunamwonea,this fool has ****ed this country and now is looking for a scapegoat na kwa akili yake ndogo anafikiri atawasaidi au kuwavutia Waislam kwa kuwabagua Wakristo anajilisha upepo sababu Waislam na Wakristo wa leo hawawezi pumbazwa na siasa muflisi za kiongozi aliyechoka kiafya na kiakili kama yeye ambaye hata hajui kwanini aliutaka urais wala hajui kwanini nchi na wananchi wake ni maskini.

Habari za Kikwete kuhusu madawa ya kulevya, tumebandika hapo juu, sasa tuoneshe udini uko wapi humo? na ukishindwa basi wewe na wenzako mnaoshabikia uongo ndio wadini. Na kama hizo hazitoshi tuletee souce yako utuambie wapi alipoongea hayo mnayozuwa. Wacheni hizo siasa za chai maharage.
 
Si ya leo haya, ndio uongozi wake kumtishia mtu mzima nyau. Si alipelekewa majina ya wauuza unga, mafisadi bandarini, bali majizi ya EPA nini alichofanya? kiduuuuchu kijiko cha sukari ndani ya bahari.
Am challenging him kama atawataja within 6 months not 6 days mimi najitoa humu JF.
 
Sasa kama aliropoka analo, alifikiria kila sehemu unaweka usanii tu ili aonekane anafanya kazi!!:confused2:
 
Nami nawaunga mkono. Rais wa nchi lazima azungumzie jambo kwa ufasaha na siyo kutoa kauli kama za taarabu.
 
Wallah hana ubavu wa kuwataja. Ni propaganda tupu za kujaribu kuset another agenda ili kuwachanganya mawazo WaTZ ili waache kujadili mambo ya muhimu ya kitaifa. Tuliambiwa kuwa kuna viongozi wa dini ambao walikuwa wanaingiza mashangingi kinyume cha sheria... mbona hakuwataja? He is just wasting our time......
 
hizi kikwete ni balozi wa nyumba kumi au Raisi wa nchi.
kauri zake ni kama kiranja wa shule ya msingi hana kauli za kiongozi
nadhani huyo aende kwa mandela akapate semina elekevu
baada ya hapo kwa mzee CASTO
kiongozi uwezi kuongea kwa design ya kushuku watu wa vitu, ukiongea unakuja na shuruhisho na utatuzi wa mambo.
ndio maana yeye tunamlipa hela nyingi na tumempa uwezo wakuchagua wasaidizi wa kutosha kumshauri kwa ajiri yetu,
sasa hawataje na kuchukua hatua.
ngonjera tu, harafu akitoka hapo anasema CHADEMA wanataka kumpindua.
uzee wa kichwa ni mbaya sana.
 
Yan huyu mbaba kwa kuropoka ropoka amezidi kweli, sasa karopoka hilo sijui atasema nini sasa, then nao kwa nin wanamwalika huyu, hawajifunzi tokana na madudu anayongea?
 
Kikwete supposedly ni rais wa nchi. Anayo mamlaka kwa mujibu wa katiba kuwadhibiti wahalifu wote ikiwa pamoja na wale wanaojishughulisha mna biashara haramu. Tangu enzi za marehemu Amina Chifupa amejisifia kuwa na orodha ya watu wanaojishughulisha na madawa ya kulevya. Lakini action taken: nduhu! Either anyamaze au awapishe wale walio na uwezo wa kuchukua hatua kwa sababu nchi inazidi kudidimia.
 
huyu jamaa mdini live,
wenzake jana walitoa tamko kuhusu kukamatwa kwa mbowe mpaka huruma sijui wanalipwa kiasi gani kujimahimbo
 
Askofu Mokiwa amesema wanamuheshimu sana kama Rais na wataendelea kumheshimu kama atawataja viongozi wa dini wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya vinginevyo hawatakuwa na njia nyingine zaidi ya kuamini kasema uongo.

Wanasema wanahisi kwa ujumla wao wamedhalilishwa hivyo awataje.
 
At last one money is talking some sense here!

Kikwete we taja tu, katika hili umeingia pabaya sana
 
Lakini yamempataje kuwachokoza Maaskofu? anadhani sanaa zake watazivumilia? ni watu hatari sana hwa na wanaheshima kubwa kwenye jamii hawa. watamharia asipo waheshimu. Kikwete take care















la
 
Nimeisoma habari yenyewe kuhusu JK kusema viongozi wa demi na madawa ya kulevya.

Inavyoonekana ni kama mtu asiye na uhakika na anachokisema kwa sababu kwenye maelezo yake anawaomba tena viongozi wa demi wawataje wanaohusika na madawa ya kulevya ili hatua zichukuliwe!

Kwa kweli kunakazi sana. Inabidi ifike sehemu asiruhusiwe kuongea mpaka apate ruhusa kutoka kwa mkapa angalau itasaidia.

Kweli ni afadhali mtu unyamaze kimya watu wafikirie wewe ni mjinga; kuliko uongee watu wa-prove kwamba kweli wewe ni mjinga. Huyu alitakiwa awe na cheo cha Nape asiende zaidi ya hapo; ndani au nje ya chama.
 
mjinga tu huyu!!!!!!!!!!!
anaendelea kudhirirsha alivyo mpuuz wa hali ya juu!!!!!
list ya wauza madawa si alisema anayo
si tunakumbuka kilichomuua amina chifupa jamani
 
Hii issue aliongea jana tarehehe 5/6 mbinga na sio hii uloweka hapa ya tarehe 31/5... kama kitu hujui uliza kwanza sio kukurupuka we Faiza vipi... soma hiyo hapo chini!!
Mkuu, watu kama hawa huwa sijibishani nao. Kama wana-act hawajui huwa nawaachaga huko huko. Ukishaona hamna substance- silence is a good answer.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom