Jumuia ya wasio na ajira

king11

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
327
79
Wote tunatambua ya kuwa ajira ni muhimu katika maisha ya mwanadamu, pia tunatambua ya kuwa kama kijana kuishi ni muhimu kuwa na ajira hivyo ukosefu wa ajira ni jambo gumu kwa kijana, kuliona hilo kuwa ni tatizo kwa vijana nimeona kuanzisha jukwaa litalokusanyisha wasio na ajira ili kuwa na sauti moja. Lengo si tu kutaka ajira bali kutafuta namna serikali itavyoweka namna ya vijana waweze kupatiwa mitaji au fursa za kujiajiri

Walio tayari kwenye jukwaa la wasio na ajira naomba wajiunge ili sauti ya umoja ni sauti ya Mungu


kuna kitu lazima ukitambue kazi ya taasisi hii ni ya kisera zaidi , kwani kazi yake ni kuweka mazingira mara ya watu kuweza kukabiliana na tatizo la ajira. na kwa mfumo wake itakuwa na bodi ambayo wajumbe wake watatoka sehemu mabali mabali , kwa ufupi mchanganuo wa mfumo wa bodi hii

1. Kutoka katika kundi la wasio na ajira

2. muwakilishi kutoka bungeni

3.muwakilishi kutoka katika wizara ya ajira/utumishi

4.Wawakilishi katika vyama vyote vya siasa

5.muwakilishi kutoka taasisi ya msajili wa kampuni na biashara

6.muwakilishi kutoka makampuni mbali mbali


LENGO LA JUMUIA HII

1. Kusaidia vijana kutuma maombi ya ajira kwenda sehemu mabali mbali

2. kutafuta ajira na fulsa za kibiashara sehemu mbali mbali na kuziweka wazi kwa wasio na ajira

3.Kuwasiliana na serikali hili kutoa usajili na utoaji wa leseni za kibiashara kwa wasio na ajira kwa gharama ndogo au bure kabisa

4.kuwawezesha vijana walio katika biashara ndogo ndogo kutambulika na kuweza kukopesheka

5.Kutafuta mitaji kutoka katika taasisi mbali mbali ikiwemo kujaribu kushauri makampuni makubwa ya madini, mabenki na makampuni ya simu kuchangia angalau 1% ya faida kama ruzuku kwa vijana wasio na ajira

5. kusimamia ajira za umma kutotolewa kwa upendeleo au rushwa


kwa maoni na ushauri pls sms 0752798074
 
Wote tunatambua ya kuwa ajira ni muhimu katika maisha ya mwanadamu, pia tunatambua ya kuwa kama kijana kuishi ni muhimu kuwa na ajira hivyo ukosefu wa ajira ni jambo gumu kwa kijana, kuliona hilo kuwa ni tatizo kwa vijana nimoona kuanzisha jukwaa litalokusanyisha wasio na ajira ili kuwa na sauti moja . lengo si tu kutaka ajira bali kutafuta namna serikali itavyoweka namna ya vijana waweze kupatiwa mitaji au fulsa za kujiajiri


walio tayari kwenye jukwaa la wasio na ajira naomba wajiunge ili sauti ya umoja ni sauti ya mungu

king nimekutumia pm umeipata? Nichek kama vp?
 
lazima tuwe pamoja na kuhakikisha kuna mazingira bora ya kujiajiri na pia kuunda mfumo huru utaohakikisha kuwa ajira si za kibaguzi au za kujuana , lazima tufike wakati ata kama mkate ni mdogo basi ugawanywe kwa haki
 
This is a novel idea... tena isiishie hapa, iende hadi mitaani na nina imani this movement will change our country
 
Kweli ajira ni ishu sana kwa vijana. Tatizo ni kwenda shule kwa malengo ya kuja kuajiriwa badala ya kwenda shule ukitegemea kuja kujiajiri wenyewe!
 
Wakuu nimesoma post moja inayouhusu jumuiya ya wasio na ajira; nimeshawishika kuandaa tamasha la wasio na kazi kujadili mambo mbalimbali yanayotuhusu ikiwemo namna ya kujikwamua na hii hali ngumu ya bongo.

Natamani watu wa kada zote wasio na kazi wasomi na tusio wasomi washiriki.
Naliweka kwenu wakuu mnishauri namna ya kuboresha hili tamasha; Nitashukuru kwa maoni yenu.
Nawasilisha wakuu
 
Wazo linaonekana zuri, lakini yatokananyo na tamasha hilo yanaweza kuwa machungu kwa wenzetu wasio sikia la mkuu nakujifanya huwa hawasikii.
 
ok naunga mkono hoja lazima tufike wakati tuwe pamoja na kuwa na sauti ya pamoja
 
Sawa kabisa vijana.

Tamasha la wasio na kazi litaiamsha serikali usingizini.

Jipangeni sawa sawa ili muwe na matawi mikoani, wilayani na ngazi ya kijiji.

Hii itakuwa jumuiya yenye nguvu sana Tanzania.

Hata wale walio na ajira isiyo rasmi, pia jiungeni.

Now, how to start and connect yourselves?- a challenge.....
 
"I am not kidding" wakati tunapata dinner nilijaribu kuwaambia comrades juu ya kuanzisha same thing, but kupitia facebook..what a coincidence.! Lets put it into life. Watu wana malengo mengi katika maisha, sasa unapoona miaka inakatika halafu uelekeo lazima ushituke, hii ni dalili nzuri na kwamba watu hawafurahii kutokutimiza ndoto. "Not Too Late, Still We Can Live Our Dreams"
 
Wadau tafadhalini sana naomba hii movement iwe ndo turning point kuondoa jinamizi hili la wasomi. Kwani kauli mbiu kuwa vijana ni taifa la kesho imepitwa na wakati muda mrefu uhalisia ni kwamba "VIJANA NI TAIFA LA SASA" vijana tuamke wakati ni huu wa ukombozi.
 
Back
Top Bottom