Jumbe ndiyo lilikuwa Chaguo la Nyerere kurithi urais wa Tanzania

Tunaambiwa mwalimu alikuwa hatembea na fedha mfukoni hata siku moja, Butiku ndiye alikuwa anashika fedha za Nyerere na kuzitumia kwa maelekezo ya mwalimu katika mizunguko yote ya mwalimu. Fursa hii ya kutumia fedha kwa maelekezo ya mdomo ilimpatia butiku nafasi ya kuwajeruhi madada zetu hata ndoa yake ikamshinda ndipo mkewe akakimbilia nje ya nchi kukimbia aibu
Hapa pia umekosea. Aliyekuwa anashika fedha za Mwalimu ni Mkanzabi.
 
Tunaambiwa mwalimu alikuwa hatembea na fedha mfukoni hata siku moja, Butiku ndiye alikuwa anashika fedha za Nyerere na kuzitumia kwa maelekezo ya mwalimu katika mizunguko yote ya mwalimu. Fursa hii ya kutumia fedha kwa maelekezo ya mdomo ilimpatia butiku nafasi ya kuwajeruhi madada zetu hata ndoa yake ikamshinda ndipo mkewe akakimbilia nje ya nchi kukimbia aibu

Mzee naona umempania kweli jamaa....!
 
Hivi Seif Bakari yuko wapi?

Kanali Seif Bakari alifariki kipindi komandoo Salmin Amour akiwa rais wa Zanzibar,na ni miongoni mwa waliokua wanamtia kiburi Salmin aache kumtetemekea na kumsikiliza mwalimu Nyerere katika kila jambo,mpaka kifo kinamkuta alikua ni mshauri wa Salmin katika mambo ya ulinzi na usalama wa taifa!Jinsi Salminn alivyokuwa anaitawala zanzibar ndio karume mzee alivyokuwa akiitawala,ndio wahafidhina wa mapinduzi walikua wanampenda salmin wakimuona kama ni kijana wao anaeyaenzi na kuyadumisha mapinduzi "matukufu" kwa vitendo!!!!!

Ikumbukwe kwamba nyerere na seif bakari walianza kutofautiana toka baada ya kifo cha karume;baada ya mauaji ya kutatanisha ya mzee karume,Katika kumtafuta mrithi wa Karume, Wazanzibari wengi walitaka Kanali Seif Bakari achukue nafasi ya Karume, lakini Mwalimu, kwa kuelewa pia uhusiano wa Seif na Karume, alikataa eti kwa madai kwamba kwa kuwa Karume aliuawa na Mwanajeshi, kumteua Bakari ambaye ni mwanajeshi kuchukua nafasi ya Karume, kungehalalisha dhana kwamba yaliyotokea yalikuwa mapinduzi ya kijeshi. Ni kwa sababu hii (ya uongo) Jumbe aliteuliwa kumrithi Karume badala ya kanali Bakari ambae Nyerere alimuona kama karume mpya

Nimesoma kitabu cha Masimulizi ya Thabit Kombo Jecha. Yeye ndiye aliyempa idea Mwalimu kuwa Mwinyi achukue Zanzibar baada ya kuondolewa kwa Jumbe mwaka 1984. Mwalimu alipokuwa anang'atuka 1985 alipenda Salim awe rais. Salim alipoleta pozi, ni Thabit Kombo tena akampendekeza Mwinyi na mwalimu akamkubali. Sasa sijui kati ya Kombo na ninyi mnaosema haya kuwa wajumbe walimkataa Salim, nani ni mkweli.
 
Mwalimu mwenyewe alitoa indication. Baada ya kuteuliwa Mwinyi alitembelea Zanzibar na akalalamika sana kwa kauli za Uhizbu.
Wakati huo sikuelewa Mwalimu anasema nini. Rafiki yangu Mzanzibari ndiye akanitaarifu juu ya Wazanzibari kumkataa Salim kwa sababu ha historia ya kuwa Hizbu. Ukisilikiza hotuba zake Zanzibar wakati anastaafu utagundua hilo. Thabit Kombo anaweza kuwa anajipigia chapuo tu kujiongezea umaarufu kihistoria.
 
Nimesoma kitabu cha Masimulizi ya Thabit Kombo Jecha. Yeye ndiye aliyempa idea Mwalimu kuwa Mwinyi achukue Zanzibar baada ya kuondolewa kwa Jumbe mwaka 1984. Mwalimu alipokuwa anang'atuka 1985 alipenda Salim awe rais. Salim alipoleta pozi, ni Thabit Kombo tena akampendekeza Mwinyi na mwalimu akamkubali. Sasa sijui kati ya Kombo na ninyi mnaosema haya kuwa wajumbe walimkataa Salim, nani ni mkweli.
Katika siasa za uzanzibar na upemba usije ukafanya kosa hata siku moja la kusikiliza wanachosema wanaoitwa "wahafidhina wa mapinduzi" ya unguja,watakupoteza mbaya,watazungumza hili lakini wanamaanisha lilee,Thabit kombo ni mmoja wa hao wahafidhina ama kwa jna lingine waasisi wa mapinduzi wanayoyaita "matakatifu".

Tatizo historia ya zanzibar imechezewa sana kwa makusudi tu ili kuvuruga ukweli,kwani wewe unajua kwamba hata huu muungano yalikua ni matakwa ya marekani ili kuhofia zanzibar isiwe new cuba kwa kumezwa na wakomunisti ambao walikua karibu mno naABDULRHMAN BABU ambae alikua muumini wa ukomunisti na ambae wamarekani walimuhofia sana kutumiwa na wacomunist wenzake kumshawishi karume kwa kutumia usomi wake (Karume hakuwa msomi alikua baharia tu mjanja mjanja kutokana na kusafiri duniani mapema na meli).

Thabit kombo hata nyerere hawawezi kulisema hili japo walilijua!historia ya zanzibar kuijua yataka ukae kitako hasa na uwe mdadisi wa style ya ushushushu hivi,maana mengi wakubwa wanayaficha sana!ni "siri" eti!,wamaerekani walifikia mpaka kumhonga karume helikopta na schoolarship kwa ajili ya AMANI au ALLY KARUME mmojawapo kwenda kusoma marekani ili alainike na kuukubali muungano, Nyerere na kambona walitumika na CIA Kulazimisha muungano na zanzibar!
 
Hizi allegation kwa maalim seif nazisikia sana kuna namna yeyote ya ku-prove hii kitu..kuna document yeyote au ilikuwa hearsay? tu naomba nisaidie mkuu nataka nifahamu hii story kwakuwa si mara ya kwanza kusikia kuna wazanzibar kama wawili wameshaniambia hii kitu...

Bado siwaamini kwakuwa wote ni wana ccm na ni waunguja inawezekana wanacheza kadi ya personality attack..naombi nisaidie kama kuna mahali naweza kupata siri hii ..

Kilichotokea ni kwamba Maalim Seif alikuwa waziri wa elimu wakakorofishana na Jumbe, jumbe akampiga chini. baada ya kupigwa chini Nyerere akamchukua Seif na kumpa kitengo pale makao makuu Dodoma. jumbe ikamuuma kwamba haiwezekani yeye ampige chini halafu Nyerere ampe cheo kingine tena kikubwa wakati huo si unajua chama ndicho kilichoshika hatamu. Vile vile tukumbuke kwamba Nyerere tayari alikuwa ameshawachukua vijana wengine ambao walikuwa kama wahasi kule Zanzibar, Kina Ahmad rashidi na wengineo.

Sasa wale wazee wanaojiita wa mapinduzi wakaandaa mipango hili kumkomoa Seif. mipango hiyo ni kupeleka hoja ya serikali tatu hili Seif na wenzake warudishwe Zanzibar wakumbane na kilichomtoa kanga manyoya. Jumbe akampa secretary achape barua na wakati huo tukumbuke Zanzibar walikuwa na usalama wao wa taifa na pia kulikuwa hakuna Computer. basi ile barua maalim Seif kainasa akampelekea Nyerere maana kaona asipoangalia itakula kwake. Basi kwenye kikao cha NEC Nyerere akamuuliza Jumbe huu muandiko wa nani Jumbe hana la kusema. Basi Nyumba ilikuwa imeshaandaliwa mjimwema ilikuwa hakuna kurudi Zanzibar tena kama alivyo akalazimishwa ajiuzuru na kuwekwa kizuizini kimtindo pale mji mwema. Hapo ndipo Seif akarudi kwenye serikali ya mapinduzi kama waziri kiongozi chini ya Mzee Ruksa. Nawasilisha
 
Interesting story..

Hayo ndio matatizo ya rais kuwekwa na mtu badala ya wananchi??
For your information, hakuna Rais kwenye hizi nchi zetu zenye njaa atakayewekwa na majority. Ni wajanja wachache wenye agenda zao ndio watakaosimika watu.

Tukirudi kwenye mada, kuanguka kwa Jumbe halikuwa tatizo la Nyerere. Ni unafiki na fitna ambayo watu waliotaka madaraka waliitumia kuona hamrithi Nyerere. Akafanya kosa ambalo kwa wakati ule ilikuwa ngumu kusameheka.

Napenda kuujua ukweli wote jinsi ulivyo na kila tunavyokwenda mbele, hata yale tunayodhani ni siri, yataanikwa hadharani. Tutayapima kila mtu kwa nafasi yake na kuamua nini cha kukiamini na nini hakiko sawa.
 
Hizi allegation kwa maalim seif nazisikia sana kuna namna yeyote ya ku-prove hii kitu..kuna document yeyote au ilikuwa hearsay? tu naomba nisaidie mkuu nataka nifahamu hii story kwakuwa si mara ya kwanza kusikia kuna wazanzibar kama wawili wameshaniambia hii kitu...

Bado siwaamini kwakuwa wote ni wana ccm na ni waunguja inawezekana wanacheza kadi ya personality attack..naombi nisaidie kama kuna mahali naweza kupata siri hii ..

hiyo ya kuhusu Maalim kuwasaliti wazenj ni ki2 ambacho hata cuf wenyewe wanakisema waziwazi. Naskia kuna muda mpaka maalim seif mwenyewe huwa anajuta kwa huo unafiki na usaliti aliowafanyia wazenj wenzake.
 
Mkuu The ROmantic,

Kuna madai ya muda mrefu kwamba Mwl Nyerere alitengeneza mfumo kristo sasa kinachonishangaza na kunistajabisha sioni Mwl akimwandaa mgalatia [Mkatoliki] mwenzake wa kuendeleza mfumo kristo au ndiyo tuseme Mzee Mwinyi,Salimu A Salimu,Rashid Kawawa walibatizwa kabla ya kupigiwa chepuo la kuachiwa kigoda cha Magogoni ?.

Ni swali la kizushi kwa Dada FF & Co.

Walikua mwinyi,salim na mzee kawawa;hawa wawili mwinyi na kawawa walikua wamewekwa kwa ajili ya bosheni tu,lakini mgombea aliekuwa anatakiwa na mwalimu offcourse alikua ni Salim,mwinyi na kawawa ilikuwa wajitoa na kumuachia salim,kawawa kwa utiifu wake kwa mwalimu kweli akatatekeleza "makubaliano" hayo ya kijinga,lakini hali haikua hivyo kwa mzee Mwinyi,wahafidhina wa mapinduzi ya zanzibar ambao waliapizana toka siku ya mapinduzi ya zanzibar kwamba mpemba hatakuja kuwa rais na kuwatawala kutokana na ushiriki mdogo na wa mashaka wa wapemba kwenye mapinduzi wakamshika masikio kijana wao mwinyi na kumuambia yule mzee wa butiana anatka kutuwekea rais mpemba....usijitoe komaa mpaka mwisho na kura zote za wajumbe wa nec toka zanzibar tutazipiga kwenye sanduku moja (la mwinyi)halafu tuone hawa wabara wakitaka kutulazimisha tunavunja muungano!kweli mwinyi akadinda nyerere akawa haaamini macho yake kimachotokea ukumbini,ndio ikabidi Salim ashauriwe kujitoa ili hali ya hewa isichafuke,na baadae nyerere akampigia pande la O.A.U SALIM Kama kumpoza!
 
Mkuu The ROmantic,

Kuna madai ya muda mrefu kwamba Mwl Nyerere alitengeneza mfumo kristo sasa kinachonishangaza na kunistajabisha sioni Mwl akimwandaa mgalatia [Mkatoliki] mwenzake wa kuendeleza mfumo kristo au ndiyo tuseme Mzee Mwinyi,Salimu A Salimu,Rashid Kawawa walibatizwa kabla ya kupigiwa chepuo la kuachiwa kigoda cha Magogoni ?.

Ni swali la kizushi kwa Dada FF & Co.

Asiyejua maana hawezi kuambiwa maana. Kuna watu washapotea kwenye ulimwengu wa fikra huru. Wanafikiria kama wako kwenye mahandaki ya zama za mawe
 
Nahisi kama hapa kuna gundu baada ya Mwalimu kumkataa Dingi wako! ...... ingawa kuna ukweli!
Mzee Malecela ndio Waziri mkuu pekee aliyesimamia na kupitisha hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, huyu mzee is my hero kwa ujasiri huu, nadhani chuki za Nyerere kwa Malecela zinatokana na jambo hili. zingine ni porojo tu za kisiasa.
 
Hivi mwalimu alijua hatokufa? kwa nini alituacha na matatizo haya ya makundi ndani ya hii CCM yake...kama kweli ni baba wa taifa angeivunja ccm ziwe mbili, angeshinikiza katiba mpya isiyowapa nguvu hawa mafisadi...tanzania ingekua ya neema...
 
Mkuu The ROmantic,

Kuna madai ya muda mrefu kwamba Mwl Nyerere alitengeneza mfumo kristo sasa kinachonishangaza na kunistajabisha sioni Mwl akimwandaa mgalatia [Mkatoliki] mwenzake wa kuendeleza mfumo kristo au ndiyo tuseme Mzee Mwinyi,Salimu A Salimu,Rashid Kawawa walibatizwa kabla ya kupigiwa chepuo la kuachiwa kigoda cha Magogoni ?.

Ni swali la kizushi kwa Dada FF & Co.

Kumbe sometimes huwa mnatofautiana!!!
 
Hivi mwalimu alijua hatokufa? kwa nini alituacha na matatizo haya ya makundi ndani ya hii CCM yake...kama kweli ni baba wa taifa angeivunja ccm ziwe mbili, angeshinikiza katiba mpya isiyowapa nguvu hawa mafisadi...tanzania ingekua ya neema...
Aliwasaidieni kwa kuhimiza kuwepo multiparty. CCM walikuwa wamelikataa hilo. Shida yetu Watanzania ni kwamba tulitegemea Nyerere atufanyie kila kitu. Na yeye alikuwa binadamu kama wewe na mimi.
 
Kweli dunia hii usimuamini mtu,hata mama yako aliyekuzaa!Kumbe Seif kawa groomed na Jumbe,halafu akaja kutosa?
 
Lakini kuna wachunguzi wa mambo wanadai kuwa Mwl Ndiye aliye tuletea Mr Clean, kumbe hata kipindi cha Mzee Ruksa Mwl alikuwa bado anaushawishi mkubwa sana ndani ya chama chake kwa bara na visiwani, tukumbuke haikuwa rahisi kumpenyeza mr Clean.
 
Bado Mwalimu was the smartest Politician our land ever produced, he had a record ya Uongozi ambayo Mwinyi hakuwanayo after his 10 years. Na at the same token Mwalimu created Mrema as his threat political tool ya kumpitishia Mkapa, na Mwalimu never let Mwinyi to touch vyombo vya Dola ambavyo viliendelea kuongozwa na Mwalimus people na who were 100% loyal to him, Mwalimu also knew kwamba Salimin kwamba anataka sana Urais wa Muungano ndio maana it was very easy kumtumia kumpitisha Mkapa under One understanding ya kuachiwa after Mkapa.

But later Salimin came to realize kwamba alidanganywa So akaanza kudai term ya Tatu Visiwani believing Mkapa would pay him back the 1995 favor, ha! Ha! It was CC Dodoma that not only stopped him but even his Man Bilali ambaye alimshinda Karume lakini akapewa Karume ushindi na CC but Salimin never went away recently ameweza kumrudisha tena Bilali. Mwalimu was a smartest politician than all.

- Le Baharia
 
mkuu the romantic,

kuna madai ya muda mrefu kwamba mwl nyerere alitengeneza mfumo kristo sasa kinachonishangaza na kunistajabisha sioni mwl akimwandaa mgalatia [mkatoliki] mwenzake wa kuendeleza mfumo kristo au ndiyo tuseme mzee mwinyi,salimu a salimu,rashid kawawa walibatizwa kabla ya kupigiwa chepuo la kuachiwa kigoda cha magogoni ?.

Ni swali la kizushi kwa dada ff & co.

alitaka kuwatoa mkosi waislam na kupunguza manung'uniko ya wapigania uhuru hao ambao walimpokea mjini akitokea kwao musoma na kaptura yake,wale wazee pale stanley street wakamshonea suruali yake ya kwanza na kumwambia hapa mjini hatukai uchi(kutembea na kaptura)!na ndio kuanzia hapo akaijua suruali mzanaki yule!pia alitaka kuulinda muungano "wake" kwa kuwachia mzenji,kumbuka alimtaka mkatoliki mwenzake mzalendo sokoine,lakini wakati huo alikua hayupo!

Back
Top Bottom