Jumba la kifahari laungua na kuteketea paa-Mbezi Beach.

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
View attachment 66499
Ni tukio la kusikitisha, jumba hili nadhifu lilojengwa na mwenyewe limeungua paa kabisa mnamo saa 11.30 hadi 12 jioni bila msaada wowote.
kwa vile jengo nil la ghorofa wapita njia walisikika wakisikitika tu wasijue la kufanya.
Hata "Fire" walipofika hapo mida ya saa 12.30 paa lote lilisha ungua.

Jumba hilo lipo barabara ya Kawe-Africana, sehemu maarufu kama "kwa Abson".
Nampa pole mwenye nyumba maana kama ndio anakaribia kustaafu,huo ni msiba mkubwa.
 
Pole sana waathirika wa ajali hii. Hali hii inasikitisha sana, na ikumbukwe kuwa huo muda wa saa 11.30 hadi 12 jioni barabara za kutoka mjini kwenda huko Kawe-Africana zinakuwa zimeshiba foleni na hivyo msaada wa magari ya zimamoto kuwahi inakuwa ni tabu tupi!! Kusipokuwa na mikakati ya kusambaza huduma za zima moto kwenda ngazi ya Tarafa au Kata tutaendelea kushuhudia majanga kama hili.
 
Nimepita hapo tena, aina ya vigae vinavyo itwa zinc alume si vizuri maana vilikuwa vinaungua bila idhibati.
 
Poor Design, Yale matank ya maji angeyaweka darini yangesaidia sana kupunguza kasi ya moto. (just an Idea)
 
Mwenye nyumba alifariki kwa ajali ya gari mwaka jana mwezi wanane moshi alipo kwenda kumzika mama yake mzazi.
 
Mwenye nyumba alifariki kwa ajali ya gari mwaka jana mwezi wanane moshi alipo kwenda kumzika mama yake mzazi.

wanasemaga mali zinaondokaga na mwenyewe.....inasikitisha sana....
 
Dah, mkuu huyo jamaa ni ndugu yangu, tulimzika mwaka jana alifariki kwa ajali!
 
Dah, mkuu huyo jamaa ni ndugu yangu, tulimzika mwaka jana alifariki kwa ajali!

Kuna kitu hapo!! Mwenye Nyumba ajali(kategeshewa),kutakua kuna mgogoro wa nyumba(wameunguza tukose wote),Ebu tupe intro kunaendeleaje hapo?
 
Back
Top Bottom