Jumamosi kutoka Dodoma!

Mwanakijiji hongera sana kwa juhudi zako. Matangazo kama yatafanikiwa naomba mada itakayofuata iwe kuhusu Kiwira. Inaelekea wanataka kuhalalisha ununuzi wa Kiwira ambao ulikuwa ni wa kifisadi kwa kudai kwamba mgodi ulikuwa katika hali mbaya na hivyo hakuna ubaya wowote Mkapa na Yona kujimilikisha Mgodi huo katika mazingira ya kifisadi.

Tatizi nilionalo mimi ni jinsi walivyojimilikisha mgodi huo? Je, kuuzwa kwa mgodi huo kulitangazwa hadharani? Je, ni nani aliyeamua Mkapa na Yona wauziwe mgodi huo? Mgodi unasemekana una thamani ya shilingi bilioni 4 lakini wameununua kwa shilingi milioni 700 na haijulikani hadi sasa wamelipa kiasi gani. Je, ni nani aliyeamua mgodi huo uuzwe kwa 17.5% ya thamani yake?

Pia mkataba uliosainiwa wa shilingi 326 billioni kati ya kampuni hiyo na TANESCO ni halali? Maana inasemekana waliosani kwa niaba ya TANESCO ni wale wazungu wa Net Group toka South Africa ambao Mkapa aliwaingiza kwa mtutu wa bunduki pale TANESCO.

Kwa mara nyingine tena hongera sana kwa juhudi zako.

Natanguliza shukrani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom