Jumamosi Iwe Siku ya Usafi Nchi Nzima

Amanikwenu

Senior Member
Dec 1, 2009
187
0
Kutokana na hali ya uchafu uliokithiri nchini hasa Mkoani Dar es Salaam, napendeza Serikali iiteue siku ya Jumamosi kuwa siku Maalum ya kufanya usafi nchi nzima kwa kuwahusisha na kuwashirikisha wananchi wote. Ikibidi BUNGE lipitishe Sheria Maalum kuhusu suala hili.
 
Wananchi washiriki vipi? Kwa kutoa pesa au kushika fagio na koleo? Na kodi tunayolipa inafanya kazi gani? Kwanza majumbani kwenu ni pasafi? Kabla ya kwenda nje ya nyumba zetu, tuanzie majumbani mwetu. Kagua leo nyumba yako kama hautakuta tandabui, majani mengi nje ya nyumba, rangi ya choo si ile wakati choo kipya!! Halafu wewe mwenyewe mfano umekata kucha zako au kucha zako ni fupi, unapiga mswaki mara ngapi kwa siku?
 
Dar Es Salaam watu walivyo wavivu unadhani wanaweza kubali wazo kama hili?. Kila mtu atakuja na kisingizio chake ili tu wasifanye usafi.
 
Hili ni la muhimu, lakini kwa watu walivyo wabishi sijui kama linawezekana.
 
Ikijengwa kama sheria/taratibu kwa kusaidiwa na mkazo wa adhabu, tunaweza.
 
Jumamosi iwe siku ya usafi !!!! SIYO SAWA.

Usafi gani wa siku nzima, uzalishaji usimame kwa ajili ya kufagia?, kumbuka usafi ni hulka ya mtu, mbona mji wa Moshi wameweza kuweka mji wao safi hadi miaka miwili mfululizo wamepata taji za usafi za kimataifa. Madiwani wa Dar waende Moshi wakapate darasa la usafi.
 
Naona kama wazo limeanza kutekeleza japo si kwa kila Jumamosi na pia naona bado umakini unakosekana katika kutekeleza wazo hili.
 
dar es salaam watu walivyo wavivu unadhani wanaweza kubali wazo kama hili?. Kila mtu atakuja na kisingizio chake ili tu wasifanye usafi.

ni wavivu kusafisha tuu ila kuchafua!!!!??
Mtu mzima na akili zake kavaa suti ya maana gari zuri anatuoa takataka hovyo,eti kwake anaziona nux anakuja kutuchafulia mazingira uswazia! Tugeuke tarimee nini!tuwapopoe mawe washike adabu shenzi sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom