Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia Julius Mtatiro na habari za ndani zinadokeza kuwa baada ya habari ya kukamatwa kwake kuwekwa hadharani na wenu mtiifu Jeshi la POlisi limepania kutoa funzo. Baada ya kutoa siri kuwa Mtatiro anashikiliiwa kituo cha POlisi Msimbazi, habari za uhakika zinasema kuwa Jeshi hilo linaloongozwa na Said Mwema, na Kanda ya Dar na Suleiman Kova limeanza mtindo wa kumhamisha hamisha ili hatimaye wamfikishe mahakamani.
Vyanzo hivyo vimeithibitishia KLHN kuwa Bw. Mtatiro amekuwa subjected to mental torture ili aweze kukubali kuwa yeye ndiye kinara wa mgomo wa wanafunzi.
"ndiyo, hajalala kwa siku tatu, chakula kimekuwa cha shida, na hata sasa jeshi halitaki kusema wazi kuwa linamshikilia na linamshikilia kwa misingi gani" kilisema chanzo chetu ambacho kiko karibu kabisa na suala hili.
Mipango ya kumfikisha mahakamani imeandaliwa licha ya ukweli kuwa hadi sasa imekuwa ni zaidi ya masaa 48 tangu akamatwe kininja siku ya Jumapili. Habari hizo zinasema kuwa Bw. Mtatiro anashikiliwa kwenye kituo cha Salenda ambapo Mkuu wa Upelelezi wa Kanda ya Dar Bw. Mkumbo akidai kuwa "watatoa funzo" kwa wale wote wanaoeneza migomo.
Juhudi za kumpata msemaji wa Polisi zimeshindikana baada ya simu yake kuita bila kujibiwa.
Mwanakijiji, hatuwezi kuvumilia ujinga huu katika zama hizi, hizo zilikuwa zama za Mfumo wa Chama Kimoja.
Kwa kuwa uko Majuu jitahidi kuwasiliana na Amnest International, haiwezekani mtu ashilikiliwe siku 3 bila kufikishwa mahakamani na bila kupewa haki ya kumwona Wakili wake. Ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya Mwanadamu, we need to shout. Badala ya watawala wetu kupambana kwa hoja sasa wanaanza kuweka watu vizuizini, very unfair.
Mbona Mafisadi wa EPA waliosababisha vifo vya Watoto, Wamama Wajawazito kwa kukosa dawa walifikishwa Mahakamani na hawakuzuiliwa? Shame!