Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Vyanzo vyangu ndani ya jeshi la Polisi vinaninong'oneza kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa TAHLISO Bw. Julius Mtatiro anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuhusika na mgomo wa wanafunzi wa elimu ya juu. Bw. Mtatiro (kwa mujibu wa vyanzo hivyo) amekuwa akihojiwa bila ya kuruhusiwa mwanasheria wake kuwepo na kwa muda wa zaidi ya masaa 24. Tangu jana ambako ka nzi kamekuwa kakifuatilia Bw. Mtatiro amekuwa akihamishwa kutoka kituo kimoja cha POlisi na hatimaye kurundikwa pale Msimbazi ambako Polisi wamekataa mtu yeyote kumuona..
Licha ya kumhoji inadaiwa mbinu za "kulazimisha" zimekuwa zikitumika dhidi yake..
Kama kuna Mwanasheria yeyote natoa wito ajaribu kufika Mzimbazi ili kumwakilisha kwani inaonekana kwa mara nyingine tena kijana huyo anajikuta yuko matatani hasa baada ya serikali pia kumnyima nafasi ya kuwa Mwalimu baada ya kukataa kumpatia kazi licha ya qualifications zote alizonazo na baada ya kuambiwa kuwa hatopatiwa kazi mahali popote Tanzania...
Free Julius Mtatiro NOW!! and Stop the Harrassment!

Last edited by a moderator: