Julius Mtatiro apandisha jazba kuhusu Tamko la Chadema kutoungana na CUF Bungeni

Toa na wewe background yako tuijue, mbona unaongea undercover? mmbea wa kiume lol. Siku hizi wanaume ni wambea kuliko wanawake, tutakupa tuzo kwa umbea dada/kaka na tutakuvisha kanga.

Na shanga za kiunoni hehehehehe

Hao wanaotaka background za wenzao zijadiliwe hapa JF hao hao ukiwapa background za mathalan Dr W. P Slaa watakutolea mimacho hao mpaka thread utaiona chungu hawataki kusikia eti Mhe aliwahi kuwa CCM, na mengineo mengi hawajui mtu akiingia kwenye siasa anakuwa kama coin anatizamwa pande zote mbili tail and head. Ngoja niishie hapa nisije nikakimbia bure
 
Nafurahi kuwa unaheshimu mapenzi yangu ila nadhani hutanitendea haki kusema mie chama changu ni chama fulani as mie ni muumini wa ile sheria ya "mgombea binafsi".

Siasa za afrika ni kama sarakasi
Wakubwa nacheka na kugonga glass
Wanyonge wanaumia na kula nyasi
Wanatuhadaa tunawapa uongozi kwa makaratasi
Uchaguzi ukimalizika wanatuasi
Kwa ari wanatuibia kwa kasi
Lini mtakaa mkaona huu uasi?

Kwenye picha wancheka kwa bashasha
Kwenye mikutano wansema mapanga shaaaa
Sisi mahajawani tunaendelea namaisha

Damu imekuwa yao dua
Ya zanzibar si mnajua?
Hivi nani wa kuwazindua
Inafaa tujitambue na janja kuzigundua

Sitapenda kuona watu wanakufa eti kwa ajili ya watu fulani, familia zao zikateseka wachache wakanufaika. Hivi hamjua mfano kule Zanzibar watu walipoteza maisha yao 2001 wanafamilia wanaumia kupeteza wapendwa wao leo wale waliochochea mukari watu wakauwawa wapo kwenye ulwa. Hivi hamjaiona picha ya Rais na Mhe sana Mbowe na tabasamu la bashasha? mnataka niamini kuwa familia za wahanga wa Arusha wameshasahau na hawana majonzi? hapana mie siamini hata kidogo! Labda mie nina matatizo ya akili sijijui au I am in a wrong planet.

Utakuwa umenitendea haki kuniambia chama changu. Thanks and good day mkuu.

Picha hizi hapa chini zinatufunza mengi ambayo zanaweza kuja pages! lakini kikubwa ni siasa sio uadui wapo kwa ajili yetu sisi na nchi yetu basi maslahi ya taifa yawekwe mbele.

Picha Ya JK Na Freeman Mbowe: Kwa niaba ya mjengwa

moz-screenshot-3.png

DR W P SLAA AKISALIMIANA NA MIZENGO PINDA

abmizingoslaa.jpg

Mkuu kwani nani alikwambia siasa ni ugomvi na uhasama??? TUnapingana kwa hoja na si ngumi. Kuwa mpinzani haimaanishi kuchukia watu wa upande mwingine. Tunachukia sera zao lakini wao kama binadamu bado tunawapenda. We ulitaka viongozi wa upinzani wasicheke na viongozi wa chama kinachoelekea kufa cha CCM
 
Na kwa hali hii, na unafiki huu wa watu wa jf ccm itatawala daima. Hata Kenya waliitoa KANU kwa kuungana, lakini nyie chadema mnaojidai you can do it alone, wait for a suprise, maana hata presidential material hakuna huko. CCM itaendelea kutawala saana nawambia, mark my words.

I agree with you 110% katika kila neno ulilosema, mie mtizamo wangu pale CDM kumejaa wanaharakati wengi kuliko wanadiplomasia siasa ina mbinu zake wanaharakati wao wakitaka mvua inyeshe basi ni lazima inyeshe hata kama hakuna mawingu wanahitaji watu wenye kuijua siasa na mbinu zake waweke strategies ili waweze ku move forward wameridhika na viti vya ubunge kwa mwendo huu tungojee tuone hiyo 2015 itakuwaje nachelea kutabiri maana si kazi yangu kutabiri ila dalili ya mvua ni mawingu na madhali radi nazisikia {as wanataka kumwajibisha Zitto} basi mvua inakaribia kunyesha tuanze kusafisha mashamba tayari kupanda na kungojea kuvuna tulicho otesha hiyo siku ya mavuno 2015.
 
poleni wote mnaonyimwa usingizi na mtatiro. ila kilicho wazi watu wa humu wote mmelewa chadema kiasi hamuwezi kuona logic (hata kama ipo) Na ukweli unabaki kwamba, Mtatiro is much, much better than a million of you in here..as Mugabe once said..go hang.

Habarrri yako bana musubati,

Kama wote tumelewa hiyo pombe aina ya chadema ni vizuri kwa kuwa na wewe ni mmoja wao, na kwa maneno mengine hata wewe umeshindwa kuona logic ya cuf kutostahili kushirikishwa kwenye kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa tayari wameshiriki kuunda serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar.
Homeboy Mtatiro ni kiongozi wa chama kama walivyo wengine, lakini sijui ni jambo gani la kisiasa ambalo tunaweza kulisimamisha kama mafaniko yake binafsi ambalo halijapata kufanywa na vijana wengine wa nchi hii.
Kama si kwamba umeongezea ulevi wa pombe ya cuf basi usingekuwa mkali kiasi cha kuwashambulia wenzako kiasi hicho.

I love you my great sister carmel, tuko pamoja.
 
Mkuu kwani nani alikwambia siasa ni ugomvi na uhasama??? TUnapingana kwa hoja na si ngumi. Kuwa mpinzani haimaanishi kuchukia watu wa upande mwingine. Tunachukia sera zao lakini wao kama binadamu bado tunawapenda. We ulitaka viongozi wa upinzani wasicheke na viongozi wa chama kinachoelekea kufa cha CCM

Vizuri sana kwa kulijua hilo na shukrani kwa kuingia kwenye kumi na nane ngoja nifunge goli sasa, ikiwa maneno yako ni ya kweli na si kinafiki kwasababu ya picha ya Jakaya na Mbowe kwanini humu ndani jamvini Jakaya amekuwa akikejeliwa kwa kila aina ya kejeli? mpaka kufikia kutengeneza picha ya mwanamke na kuweka kichwa cha Jakaya hii ndio siasa?

Uliona maneno yaliyotolewa pale mkutanoni Arusha? ile ndio siasa? naamini siasa inahitaji diplomacy ya hali ya juu na si maguvu hili jamaa wa CUF walilitambua na sasa wanawatumikia raia wa zanzibar kwa msemo likifana letu sote likizama lawama yetu sote. Nyie mmebakia na madua mabaya na kuombea matatizo ilhali sie sote tumo kwenye hiyo safina na wengi hatujui kuogelea sasa ikizama kwa dua zenu hatapiga ngabu?

Bado naamini na nitaendelea kuamini siasa si ugomvi na nitaendelea kulaani wale wote wanaoshabikia na kuhubiri fujo na kudharauliana. Mungu atawaangaza wale wote wanaotumia uhai wa wenzao kujinufaisha kwa hali yoyote.
 
I agree with you 110% katika kila neno ulilosema, mie mtizamo wangu pale CDM kumejaa wanaharakati wengi kuliko wanadiplomasia siasa ina mbinu zake wanaharakati wao wakitaka mvua inyeshe basi ni lazima inyeshe hata kama hakuna mawingu wanahitaji watu wenye kuijua siasa na mbinu zake waweke strategies ili waweze ku move forward wameridhika na viti vya ubunge kwa mwendo huu tungojee tuone hiyo 2015 itakuwaje nachelea kutabiri maana si kazi yangu kutabiri ila dalili ya mvua ni mawingu na madhali radi nazisikia {as wanataka kumwajibisha Zitto} basi mvua inakaribia kunyesha tuanze kusafisha mashamba tayari kupanda na kungojea kuvuna tulicho otesha hiyo siku ya mavuno 2015.
Kwa watakaoudhika smahani kama nimewakwaza, lakini kwa mtaji huu naomba ccm iendelee kutawala, wapinzani wote hawako tayari, they act like teenagers. Wao wenyewe hawajui nafasi yao kama wapinzani, hawana msimamo wala umoja, ni manyang'au tu pengine kushinda hata ccm ila tu ishu ni kwamba hawana nafasi ya kuonyesha makucha.
 
Mohamed Shossi udini tu unakusumbua huna lolote, huna haja ya kuficha u-CCM/CUF wako. Utaumia sana!
 
Vizuri sana kwa kulijua hilo na shukrani kwa kuingia kwenye kumi na nane ngoja nifunge goli sasa, ikiwa maneno yako ni ya kweli na si kinafiki kwasababu ya picha ya Jakaya na Mbowe kwanini humu ndani jamvini Jakaya amekuwa akikejeliwa kwa kila aina ya kejeli? mpaka kufikia kutengeneza picha ya mwanamke na kuweka kichwa cha Jakaya hii ndio siasa?

Uliona maneno yaliyotolewa pale mkutanoni Arusha? ile ndio siasa? naamini siasa inahitaji diplomacy ya hali ya juu na si maguvu hili jamaa wa CUF walilitambua na sasa wanawatumikia raia wa zanzibar kwa msemo likifana letu sote likizama lawama yetu sote. Nyie mmebakia na madua mabaya na kuombea matatizo ilhali sie sote tumo kwenye hiyo safina na wengi hatujui kuogelea sasa ikizama kwa dua zenu hatapiga ngabu?

Bado naamini na nitaendelea kuamini siasa si ugomvi na nitaendelea kulaani wale wote wanaoshabikia na kuhubiri fujo na kudharauliana. Mungu atawaangaza wale wote wanaotumia uhai wa wenzao kujinufaisha kwa hali yoyote.

Wakimaliza wanasema Mtatiro ana ongea bila kufikiri je yale yalifanyika pale arusha ndo kufikiri kote kwa viongozi wa chadema? they all the same, i dont trust them. na ukitaka kupima hayo yote angalia yasemwayo humu, watu hawana hekima, wala hawana muda wa kutafakari, na wanajiita wasomi, full kufata upepo, bora chadema imesema hivi, woote wanaunga mkono, kama mazezeta. namna hii taifa hili halina mkombozi, hadi tuweze kutofautisha ushabiki na reality.
 
Kwa watakaoudhika smahani kama nimewakwaza, lakini kwa mtaji huu naomba ccm iendelee kutawala, wapinzani wote hawako tayari, they act like teenagers. Wao wenyewe hawajui nafasi yao kama wapinzani, hawana msimamo wala umoja, ni manyang'au tu pengine kushinda hata ccm ila tu ishu ni kwamba hawana nafasi ya kuonyesha makucha.

acha ujinga wewe na u-CCM wako, inshu ni cuf kuungana na cdm. Kwani hawawezi kuleta upinzani mpaka waungane na cdm? Mbona wao walipoiwekea mtimanyongo cdm kwenye mambo kadhaa cdm ilinyamaza? Wake up!
 
Habarrri yako bana musubati,

Kama wote tumelewa hiyo pombe aina ya chadema ni vizuri kwa kuwa na wewe ni mmoja wao, na kwa maneno mengine hata wewe umeshindwa kuona logic ya cuf kutostahili kushirikishwa kwenye kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa tayari wameshiriki kuunda serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar.
Homeboy Mtatiro ni kiongozi wa chama kama walivyo wengine, lakini sijui ni jambo gani la kisiasa ambalo tunaweza kulisimamisha kama mafaniko yake binafsi ambalo halijapata kufanywa na vijana wengine wa nchi hii.
Kama si kwamba umeongezea ulevi wa pombe ya cuf basi usingekuwa mkali kiasi cha kuwashambulia wenzako kiasi hicho.

I love you my great sister carmel, tuko pamoja.

nitajie hao vijana kwanza kaka. mimi si mkali bali sioni logic ya watu kumshambulia mtatiro kisa ka oppose chadema, why, he has that right ya kuwa chama anachokipenda kama nyie mlivyo chadema, msilazimishe akubali reasoning yenu, muache areason anavyotaka yeye. na hata weqwe unajua kwa umri wake na uchanga wake katika siasa yuko mbali kushinda wote mnaopiga kelele kwenye keyboard hapa, na wakati hata maandamano ya kupinga dowans yakiitishwa hamtokei.
 
Haha haa shossi, karibu Tanga yahkee, hapo kwenye bold hapo ndo ukweli upo. Mtatiro chadema wamtaka usiku na mchana ati kwa vile kaweka ngumu ndo wanaishia kutaka kumtoa roho kisa kawambia ukweli.
Hebu twende zetu kwenye jukwaa la mapenzi sie lol.

Nipo Ngamiani dada yangu nimekuja kushughulikia matatizo ya kifamilia dua zako mpendwa ili niweze kufanikisha. Naona mate yamekutoka nilipokutajia hombo na dona.

Husifia dona na hombo na kuiponda nyama
Kumbe wanaitamani ila uwezo hawana

Hawa bandugu wanataka Sitta, Mwakyembe, prof safari waingie CDM na pengine hata Rostam wanamtamani ila kimoyomoyo maana wanajua kuwa ni mtu mjanja na anaweza kufanikisha malengo yao akiwa upande wao. Rostam ni genius na jasiri mambo anayoyafanya mtu yeyote lazima amfeel na kushangaa anawezaje? hicho ni kipaji wengi wanavitafuta kama hivyo.
 
Mkuu kwani nani alikwambia siasa ni ugomvi na uhasama??? TUnapingana kwa hoja na si ngumi. Kuwa mpinzani haimaanishi kuchukia watu wa upande mwingine. Tunachukia sera zao lakini wao kama binadamu bado tunawapenda. We ulitaka viongozi wa upinzani wasicheke na viongozi wa chama kinachoelekea kufa cha CCM
Kuna wengine upinzani kwao ni NGUMI, MATUSI, etc..etc. na si hoja.
 
Uliona maneno yaliyotolewa pale mkutanoni Arusha? ile ndio siasa? naamini siasa inahitaji diplomacy ya hali ya juu na si maguvu hili jamaa wa CUF walilitambua na sasa wanawatumikia raia wa zanzibar kwa msemo likifana letu sote likizama lawama yetu sote. Nyie mmebakia na madua mabaya na kuombea matatizo ilhali sie sote tumo kwenye hiyo safina na wengi hatujui kuogelea sasa ikizama kwa dua zenu hatapiga ngabu?.
Nani alitumia nguvu Arusha, Uliona maneno tu hukuona risasi na mabomu?
 
nitajie hao vijana kwanza kaka. mimi si mkali bali sioni logic ya watu kumshambulia mtatiro kisa ka oppose chadema, why, he has that right ya kuwa chama anachokipenda kama nyie mlivyo chadema, msilazimishe akubali reasoning yenu, muache areason anavyotaka yeye. na hata weqwe unajua kwa umri wake na uchanga wake katika siasa yuko mbali kushinda wote mnaopiga kelele kwenye keyboard hapa, na wakati hata maandamano ya kupinga dowans yakiitishwa hamtokei.

Mwita Maranya,

Anataka kutuambia CDM wakishinda wataongoza Serikali peke yao vyama vinavyofuatia vitabaki kuwa vya upinzani. Wao wana sera zao "ubinafsi" na hawakubaliani na sera za kijinga "sharing of power" pengine mimi ninavyoona wananjaa sana na mwenye njaa akimkaribisha mtu anaona hata shiba!
 
nitajie hao vijana kwanza kaka. mimi si mkali bali sioni logic ya watu kumshambulia mtatiro kisa ka oppose chadema, why, he has that right ya kuwa chama anachokipenda kama nyie mlivyo chadema, msilazimishe akubali reasoning yenu, muache areason anavyotaka yeye. na hata weqwe unajua kwa umri wake na uchanga wake katika siasa yuko mbali kushinda wote mnaopiga kelele kwenye keyboard hapa, na wakati hata maandamano ya kupinga dowans yakiitishwa hamtokei.
unauhakiaka kwenye nyekundu?
 
Yaani Tangia Jana watu wanabishana hapa hata kuweka Tamko la Mtatiro hawajaweka. Kilichpo hapa watu wanazungumza Hisia ni vyema kilichozungumzwa na Mtatiro kikawekwa hapa tuone kama kina Substance
 
Nani alitumia nguvu Arusha, Uliona maneno tu hukuona risasi na mabomu?

Moto haujiwashi wenyewe cheche inaweza kuteketeza msitu mnene, mtoto hazaliwi bila kutungwa mimba. Huwezi kumeza bila kutafina labda kama unakula dona na bamia/hombo.

Kila kitu kina chanzo na huwezi kutibu ugonjwa bila kuzuia chanzo chake. Naamini kabisa huwezi kuzuia malaria kwa vyandarua na vivyovivyo huwezi kutengeneza jambo la kiasasa kwa kubomoa ujenzi wa nyumba peke yake ndio unaweza ukaboamoa na kujenga!
 
I agree with you 110% katika kila neno ulilosema, mie mtizamo wangu pale CDM kumejaa wanaharakati wengi kuliko wanadiplomasia siasa ina mbinu zake wanaharakati wao wakitaka mvua inyeshe basi ni lazima inyeshe hata kama hakuna mawingu wanahitaji watu wenye kuijua siasa na mbinu zake waweke strategies ili waweze ku move forward wameridhika na viti vya ubunge kwa mwendo huu tungojee tuone hiyo 2015 itakuwaje nachelea kutabiri maana si kazi yangu kutabiri ila dalili ya mvua ni mawingu na madhali radi nazisikia {as wanataka kumwajibisha Zitto} basi mvua inakaribia kunyesha tuanze kusafisha mashamba tayari kupanda na kungojea kuvuna tulicho otesha hiyo siku ya mavuno 2015.

Hizi ndo dua zenu watu wa cuf, dua la kuku halimpati mwewe,
cdm ilianza kufanya siasa tangu kupata usajili kama vyama vingine,
cdm imekuwepo bungeni tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995,
cdm imewaunga mkono nccr mageuzi 1995 nafasi ya urais,
cdm imewaunga mkono cuf 2000 nafasi ya urais,
cdm imekuwa ikiongeza idadi ya wabunge kidogo kidogo 1995, 2000, 2005 na 2010,
cdm imeonyesha kwamba ina viongozi makini hadi kukiwezesha kukubalika na watanzania wengi
cdm imekuwa na ustawi kutoka kuwa chama kidogo nyuma ya cuf, nccr na udp mwaka 1995 hadi kuwa chama kikuu cha upinzani mwaka 2010, wakati udp iko icu, nccr ndo imezinduka usingizini baada ya kuwa icu muda mrefu na cuf imesimama pale pale hadi kupigwa overtake na cdm. Kwahiyo yeyote anayetabiri kifo cha cdm anaota ndoto za mchana.
cuf imesaini maridhiano zenji bila kushirikisha vyama vingine na hilo kwenu mnaona sawa,
cuf imeshirikiana na ccm kuunda serikali zanzibar kufuatia maridhiano ya kibinafsi kati ya cuf na ccm,
cuf hao hao wanaounda serikali ya zanzibar wanataka kujumuishwa kambi ya upinzani bunge la jamhuri ya muungano,
cdm kukataa kuwashirikisha cuf kuunda kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa tayari wao wanaunda serikali wanaanza kupiga mayowe.
Hebu wapambe wa cuf kubalini ukweli, nyie mnaunda serikali mtakuwaje tena upande wa upinzani???
 
Gazeti La majira

CUF yalia na CHADEMA

*Yashutumu kuwatenga katika Kambi Rasmi Bungeni
*Yadai CHADEMA na wabaya wao watakufa na kuiacha

Na Rabia Bakari

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimedai kuhujumiwa na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana 'kauli za kichochezi' zinazotolewa dhidi yake kuhusu sababu za kukataa kushirikiana nao bungeni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema kuwa licha ya kuhujumiwa na CHADEMA lakini pia wanasikitishwa na kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa kwa kudai kuwa CUF sio chama cha upinzani nchini.

"Tunasikitishwa na kauli hiyo ya Dkt. Slaa na nikimnukuu anasema kuwa 'CUF siyo chama cha upinzani Tanzania tena, eti kwa sababu kiko serikalini Zanzibar' na kwa hiyo CHADEMA hawawezi kushirikiana na CUF katika kuunda kambi ya pamoja bungeni.

"CHADEMA wanaishambulia sana CUF hivi sasa, wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa kitendo cha CUF kuwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni dhambi kubwa mno na kuwa Watanzania wasiiunge mkono CUF Tanzania bara, jambo ambalo ni ndoto za alinacha na kamwe halitatokea kwani Watanzania wa sasa hawadanganywi kwa propaganda zisizo na maana,"aliongeza.

Kauli ya Bw. Mtatiro inatokana na Tamko la Kamati kuu ya CHADEMA lililotolewa na Dkt. Slaa, kuwa CC ya chama hicho imemuagiza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, kuunda baraza kivuli kwa kuhusisha wabunge wa CHADEMA pekee.

Akitoa tamko hilo, Dkt. Slaa alisema: "Kamati Kuu imeendelea kuzingatia umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana katika kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini. Hata hivyo, kamati kuu imezingatia kuwa Chama cha Wananchi (CUF) wamejiunga na CCM kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

"Na kwa kuwa sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za muungano na kwa kuwa vyama vingine vya upinzani vyenye wabunge vimo katika ushirikiano na CUF, Kamati Kuu imeona kuwa CHADEMA haiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo.

"Sasa kwa mfano tukiazimia kitu kinachopingana na serikali, Katibu Mkuu wa CUF ambaye ndiye Makamu wa kwanza wa Rais huko Zanzibar unategemea atakubaliana nacho ili apingane na serikali, hivi vyama vingine navyo tayari vimeshakuwa sehemu ya watawala maana wameamua kushirikiana na CUF katika kamati yao," alisema Dkt. Slaa.

Akizungumzia maazimio hayo, Bw. Mtatiro alisema kuwa CUF haiwezi kuwalamba miguu viongozi wa CHADEMA kwani hakuna faida yoyote wala umuhimu ambao wao wameonesha tangu walipojaribu kila namna kuwafanya wafanye kazi kwa umoja na vyama vingine na kugonga ukuta.

"Mara zote CHADEMA wamekuwa na historia ya kuvisaliti vyama vingine vya upinzani huku wakikimbilia kwa umma kuomba waungwe mkono wao peke yao," alidai.

Aliongeza kuwa CHADEMA kina matatizo mengi sana tangu mwaka 2007, na waliwavumilia kwa kiasi kikubwa na hata baada ya uchaguzi mkuu kuisha mwaka jana, CUF iliiomba CHADEMA iweze kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuwa na kambi ya upinzani imara zaidi na yenye nguvu.

"CHADEMA walikataa kabisa suala hili kwa maelezo kuwa “wao wako tayari kuungana na CUF tu katika kambi ya upinzani na kuwa hawaviamini vyama vya NCCR, TLP na UDP, na tulijaribu kuwasihi lakini hawakutaka kubadili msimamo huo.

"Lakini baada ya yote hayo, jana (juzi) CHADEMA wametoa kauli ya kinafiki, eti wao hawawezi kushirikiana na chama kinachoongoza dola, yaani CUF na kuwa wao CHADEMA wako tayari kushirikiana na NCCR-Mageuzi," aliongeza.

Bw. Mtatiro alisema kuwa hivi karibuni NCCR ndio walikuwa kikwazo kwa CHADEMA kushirikiana na vyama vingine, hata mwezi haujapita wamegeuka na kudai CUF ndiyo adui.

"CHADEMA ni chama popo sana, hawajui wanachofanya, wamelewa madaraka na kuchanganyikiwa vibaya baada ya kupata majimbo 20 Tanganyika, sasa hawana haja na CUF na vyama vingine, wanadhani majimbo 20 ndio Ukombozi wa Tanzania umemalizika.

“Ni sawasawa na maskini sana anayeamka ghafla anajikuta tajiri, hajui namna gani atatumia utajiri wake, anaanza kuwatukana majirani zake alioishi nao kwa shida na raha katika umaskini wao, anawatukana majirani huku anaendelea kuponda mali na wasichana warembo katika kijiji hichohicho, siku moja mali zinaisha……hadithi ya tajiri mjinga inaishia hapo," aliongeza Bw. Mtatiro kwa jazba.

Aliendelea kukishutumu chama hicho kuwa kinafanya kusudi kutoa kauli za kichochezi, wakiamini kuwa CUF ikifa bara wao watapumua mno.

Alisema ni wazi CHADEMA wanaiogopa CUF, huku wakifahamu fika kuwa chama hicho kina mtandao mkubwa na kina mbinu ya kujiimarisha bara na hatimaye kuongoza nchi.

Bw. Mtatiro alidai kuwa kitendo cha CHADEMA kuwadharau Wazanzibari, kudharau maamuzi ya wananchi wa Zanzibar katika nchi yao, kudharau katiba ya Zanzibar ni kitendo cha kijinga mno.

"Wazanzibar ndio walioamua kwa kupiga kura kuwa wanahitaji serikali yao, ya umoja wa kitaifa kwa maslahi ya nchi yao ya Zanzibar kwa kujali amani maendeleo na ustawi wa taifa lao.

"Wazanzibari ndio walioamua kuwa chama kitakachoongoza katika uchaguzi kitatoa rais na mawaziri na cha pili kitatoa pia makamu wa kwanza wa rais na mawaziri. Wakapiga kura, wakatoa maamuzi haya, wakayaingiza katika katiba yao ya Zanzibar katika mabadiliko ya 10 ya katiba," aliongeza.

Alisema ni ujinga kudai CUF kuwa katika mfumo wa serikali iliyoamuliwa na wananchi katika upande mmoja wa nchi ni dhambi.

Alihoji kuwa, CUF ilipopata nafasi ya pili Zanzibar CHADEMA walitaka ikiuke matakwa ya wananchi na kukataa kuingia serikalini ili iwafurahishe CHADEMA ambao Zanzibar hawana hata mjumbe wa mtaa wala tawi?

"Nani asiyejua kuwa CUF ni chama chenye nguvu na mtandao Zanzibar na Tanganyika na ni chama cha pekee cha upinzani chenye wabunge kutoka pande zote za muungano? Nani asiyejua kuwa CHADEMA ni chama kilichoko Tanganyika peke yake?

"Nani asiyejua kuwa CHADEMA kinaumizwa sana na mafanikio na utulivu wa kisiasa Zanzibar yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na busara na viongozi wa CUF ambao hawakuweka maslahi ya chama mbele katika kulinda uhai na maisha ya Wazanzibar?" alihoji.

Bw. Mtatiro aliyewania ubunge katika Jimbo la Ubungo na kushindwa na Bw. John Mnyika wa CHADEMA, alidai kuwa CUF kama chama chenye nguvu kubwa Zanzibar watazidi kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi kila mara bila kujali kama CHADEMA watakasirika au la.

Aliongeza kuwa chama kipi ili kuwatumikia Watanzania, kuwatetea katika madhila yote na manyanyaso wanayofanyiwa.

"Tutaendelea kuwa katika SUK na kulinda maamuzi na matakwa ya wananchi wa Zanzibar lakini kwa upande wa Tanzania bara ambako katiba iko wazi, kuna chama kimoja kinachoongoza dola na vingine vyote vikiwa vyama vya upinzani, tutaendelea kuheshimu matakwa ya kikatiba yaliyopo Tanzania bara," alisema.

Aliwataka CHADEMA wafahamu kuwa CUF kitazidi kuwa chama cha kitaifa kwa kuzidi kupata wabunge wengi kutoka Bara na Zanzibar, kujiimarisha pande zote za nchi hadi waione njema inayosubiriwa na Watanzania wote.

Bw. Mtatiro aliongeza: "CHADEMA na watu wote wanaoitakia mabaya CUF watakufa na kukiacha chama hiki kikishamiri kama tegemeo la pekee la Watanzania," alisema.
 
Mkuu hilo haliwezekani hapa, ni lazima watu wawe na mapenzi na watetea upande wao. Bora tu wewe ungetoa mawazo yako kama unadhani kwamba CUF inaweza kuwa chama tawala Zanzibar na wakati huo huo kikawa chama cha Upinzani Bara. Ukizingatia chama kinachotawala Zanzibar ndicho kinachotawa bara.[/QUOTE
Nakubaliana sn na ww na endapo CHADEMA watafanya hivyo watavurugwa ss hivi ktk misimamo na mipango yao.
 
Back
Top Bottom