Julius Mtatiro amefanya mahojiano na gazeti la Mwanahalisi na kusema kinachomkera na kumuumiza roho ni dhana iliyojengeka kwamba CUF ni chama cha Kiislamu.Amepinga vikali dhana hiyo na kusema hakuna upendeleo wowote wa kidini ndani ya CUF na ndio maana yeye Mkristo akapewa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.Amesema ataanzisha moto nchi nzima kudai katiba mpya na kufuta hiyo dhana ya udini dhidi ya chama chake.Amesema atahakikisha ule umaarufu wa kale wa CUF utarudi na chama chake kitavipiku vyama vyote hapa nchini.
Wadau imekaaje hii? Kweli Julius Mtatiro ataweza kufuta dhana hii....................
Wadau imekaaje hii? Kweli Julius Mtatiro ataweza kufuta dhana hii....................