Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,854
FM, mzee umechanganya mambo mawili. Jukwaa la Wahariri linaongozwa na Datoo. Jukwaa hiloliliunda tume baada ya mazishi ya Wangwe iliyoongozwa na Kubenea. Hii ilikuwa kabla ya kasheshe la Mkuchika. HIvyo katika mkutano wao wa leo Jukwaa lilitoa uamuzi na ile tume (iliyoongozwa na Kubenea) na iliyomaliza ripoti yake kabla ya toleo la wiki iliyopita ilikuwa inatoa ripoti yake leo pia.
Ila ni kwa kiasi gani Kubenea alishiriki katika kuinfluence maamuzi dhidi ya Mkuchika sina uhakika. Nakubaliana na wewe angetakiwa kurecuse.
MKJJ. Asante kwa ufafanuzi. Ilibidi hawa wahariri waweke bayana kuwa huu uamuzi umetokana na ripoti ya tume iliyoundwa na kuwasilishwa kabla ya tukio la hivi karibuni. Bila hivyo, kweli wengi wetu tutaiuunganisha kimakosa na kasheshe ya hivi karibuni. Kuondoa mzizi wa fitina, ingekuwa vizuri zaidi kama hiyo ripoti ingewekwa wazi kwa umma. Waibandike humu, tujisomee.