Jukwaa la Siasa lisilojaadili Siasa!! Uvivu wa Kufikiri na Hoja za Kufuata Mkumbo!

Unawezaje kutenganisha Jukwaa la siasa na siasa zenyewe!? Ni sawa na kumtenganisha mwanasiasa na siasa. Siasa si majadiliano pekee inajumuisha pia utendaji na utekelezaji wake.
 
Ukisoma kwa makini hoja zinazoletwa huku ni malalamiko ya siasa na siyo siasa! Majadiliano ni kuhusu CDM, CCM, CUF, NCCR na TLP! Wengi hawajui hata hivyo vyama vinasimamia nini. Suala kwamba inawezekana hivyo vyama havina vinachosimamia ni tofauti na WanaJF kutokujua kwamba hakuna vinachosimamia! Wavamizi kutoka facebook na kwingineko kazi yao ni kuweka comments kama 'crap' 'duh' na 'wagalatia' 'urojo'!

Majadiliano ya kuhusu siasa yamegeuzwa taarifa na upashanaji habari! Utasikia 'chadema watoka ukumbini' ccm mara waula' 'lowasa fisadi' 'mbowe mwenyekiti wa CDM' 'JK Raisi wa Tanzania' 'Pinda aenda Malawi' 'January Makamba sio Mtoto wa Makamba'

Sasa hapo ni siasa au taarifa za siasa? Mtu si unaweza ukapost hata jukwaa la mapenzi au ukawataarifu na huko wajue Pinda kaenda Malawi! Utasikia mtu anasema Pinda ni Mwanasiasa lazima tunjadili!!

Inapofika wakati wa hoja ngumu ndipo utajua mawazo ya watu humu ndani! Ikianzishwa thread ya 'Uchumi wa Tanzania wazidi kuporomoka: nini kifanyike' utaona idadi ya wachangiaji!! Hakuna mawazo yatakayotolewa sana sana utasikia 'kazi yao kulipa dowans' 'ccm iondoke madarakani (as if mtu hajui sheria inasemaje) 'slaa ndio raisi'

Sasa unajiuliza uchumi utakuwa kweli? Great thinkers ndio wameshafikiri hivyo!!

Tatizo letu tunaelekeza hasira zetu kule ambako sio! Hatukai chini kujipanga tufanye nini kupiga hatua! Tunatumia muda mwingi kupata taarifa ambazo hatuna cha kufanya zaidi ya kuongeza hasira!

Tunakuwa wagumu kutoa mawazo yetu kujenga chama chochote tunachoona kinafaa. Tunakuwa wepesi kutetea vyama vyetu hata kama vinakosea! Tunasahau kwamba CDM haiwezi kuanguka kisa imekosolewa! CCM haiwezi kutoka madarakani kwa kutukana!!

Yaliyotokea bungeni yanadhihirisha nafasi ya jukwaa hili katika siasa za nchi yetu! Wengine tunasupport kwa nguvu vyama vya upinzani kuungana as if vyote vinapinga! Eti CDM wakubali kugawana nafasi na wengine!! Wengine hao ni Mrema na Cheyo!! Au Kafulila na Hamad Rashid!! Ni muungano gani huo kama sio unafiki?? Tumefikiria kwa kina kabla ya kuulilia huo ushirikiano?

CDM na vyama vingine kila kimoja kina sera na mitazamo yake. Hakuna mtazamo wa pamoja hata kama ni kuing'oa CCM! Wenyewe kwa wenyewe wanapingana na hiyo ndio concept ya vyama vingi!

Tatizo la CDM ni kutokusimamia ukweli kwamba 'kila chama kisimame kwa miguu yake na kitekeleze au kisimamie sera zake'. Hakukua na sababu ya kutoa kisingizio kwamba CUF wameungana na CCM Zanzibar na vyama vingine ni rafiki wa CUF hivyo hatushirikiani navyo!!

Hakuna kosa kusimama na kutamka hilo. CDM ni CDM na CUF ni CUF! Kama ilishindikana kushirikiana wakati wa uchaguzi inawezekana vipi wakashirikiana kwenye Bunge? Huo utakuwa ni unafiki!

Mawazo yangu kama MwanaJF, tuache kuligeuza hili kuwa jukwaa la taarifa za siasa, matusi, uvivu wa fikra, kutolea hasira nk!! Hili ni jukwaa la kushusha nondo za siasa zitakazosaidia kuleta mabadiliko katika nchi hii. Ni sehemu ya kuonyesha tofauti yetu na wao!

Kunawatakaokurupuka 'umetumwa' 'wale wale' na mengineyo! Sijatumwa!

Kwa faida ya ukweli na uwazi mimi ni mwanachama hai wa CDM. Siwapendi CCM kwa sababu ya kushindwa kwao kuwasaidia wananchi wa Tanzania kufikia ndoto za uhuru. Ni chama dhaifu, hakina dira wala muelekeo. Hakijui kinasimamia nini! Viongozi wake wamefika mwisho wa kufikiri. Hawana viongozi mbadala ndio maana mtu anaweza kujiuzulu na akarudi kuwa mwenyekiti wa kamati. Mtu anaweza kuwa mwizi na akawa mbunge hata kama ana kesi ya kujibu!


CDM ni chama ambacho kimekuwa na kinaendelea kukua. Kinatoa nafasi ya mawazo mapya. Maamuzi ya Wabunge wa CDM sio lazima yawe maamuzi ya CDM ndio maana kuna kamati ya Wabunge. Endapo Wabunge hao watatoa msimamo ambao ni kinyume na yale ambayo CDM inasimamia hata wao sio zaidi ya Chama, watawajibishwa kwa ujumla wao na mmojammoja! Huo ndio uongozi!

Hayo ndio mawazo yangu!

check hiyo blue,...umeongea kizalendo lakini DOWANS ni sehemu ya uchumi pia sababu bil.94 ukiapply multiplier effect unatengeneza ajira nyingi,....na unaposema nini tufanye kujikwamua!!utajikwamuaje bila kuiondoa ccm,hata uje/uwape plan zipi za kuikwamua nchi mafisadi hawtaziimplement kwa hiyo humu tutaendelea kuuzungumzia utaifa wa chadema na usaliti wa cuf,nccr,tlp,udp,dovutwa na wengineo mpaka kieleweke,..atleast jf is the platiform where we can get things off our chests
 
Back
Top Bottom