Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
- Thread starter
- #41
Mkuu MsandoA.,
Makala yako ni muamsho kwa wanaJF wengi ambao kweli ni bendera kufata upepo, mipasho na matusi. Pia jukwaa limevamiwa na wapenzi wa CDM ambao huona wengine wa vyama vyengine au wasio na vyama hawana haki ya kutofautiana na misimamo yao. Kwa hili umegusa ukweli mtupu.
kuna kipande hiki katika makala yako.."Tatizo la CDM ni kutokusimamia ukweli kwamba 'kila chama kisimame kwa miguu yake na kitekeleze au kisimamie sera zake'.
Mkuu wako watu, mimi ni mmoja wapo ambao ningependa kuona upinzani unashirikiana, kwani kazi ya kuing'oa CCM ni ngumu kwa chama kimoja kimoja...Lakini hiyo red, jee huo ni msimamo mpya kuanzia 2010? Au ni kwa sababu CDM imepata wabunge 20 uchaguzi wa 2010?
Huo sio msimamo wa CDM. Ni maoni au mawazo yangu kama Alberto. Chama kina taratibu zake za kutoa misimamo na inawezekana msimamo huo ukapingwa na wanachama wengine wengi hivyo kukosa sifa ya kuwa msimamo wa pamoja.
Tatizo la ushirikiano ni kwamba viongozi wa vyama haviaminiani. Tatizo la Mrema na CDM ni pale ambapo alitangaza waziwazi kumkubali Kikwete na alipoanza kumshambulia Dr Slaa wakati wa kampeni Vunjo. Hii ilikuwa ni baada ya CDM kumsimamisha John Mrema kama mgombea. Hoja ya CDM ilikuwa ni kwamba John ni kijana na ana elimu. Mrema ni mzee na muda wa siasa umefika kikomo. Kutokana na tofauti hizo ushirikiano ukashindikana.
Cuf unajua yanayojiri! Bado kwao ni kwamba kama inawezekana kuunda serikali ya kitaifa bara na CCM haina tatizo. Ni kwa maslahi ya Taifa!
Ni vizuri kama wanaJF tukalingalia upya suala la ushirkiano wa vyama na kutoa mawazo yetu. Isiwe kwa sababu CDM na CUF hawajaungana au kwa sababu tunataka waungane. Tuzungumzie ni maslahi yapi ya Taifa na yatapatikanaje kwa ushirikiano wa vyama vya siasa tulivyonavyo!!