Jukwaa la siasa inaanza kunipa jibu la wabunge wa vitu maalum katika bunge la jmt.

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
wanajf;
haya ni mawazo yangu, nini mawazo yako ktk hili?
nimekuwa nikifuatilia majukwaa mbalimbali ktk jf na nimekuja kugundua kwamba jf ina member wengi sana na ktk hao members kuna wanawake kwa wanaume. Japo ni vigumu kutambua gender za members; lkn ukifuatilia thread hasa zinazohusu mambo ya gender utaweza kupata picha fulani kuhusu gender ya member fulani. Na ktk hili nimegundua kwamba tofauti kati ya wanaume si kubwa sana ktk jf.

Sasa turudi kwenye hoja yangu ya msingi; nikifuatlia michango mingi sana ya members ktk majukwaa yote; napata picha fulani kwamba wanaume wamekuwa na mwamko mkubwa sana katika jukwaa la siasa kuliko dada zetu ambao wameonekana kuwa active sana ktk jukwaa la mmu na chit-chat. Sasa picha ninayopata ni kwamba; labda wakinamama mambo ya kisiasa hawapendi/hawataki kujishughulisha nayo ndiyo maana hata michango yao ktk jukwaa la siasa imekuwa kwa nadra sana. Yaani ni wakinamama wachache sana wenye kutoa michango yao hapo, na si ajabu yawezekana hata wengi wao hawapendi kutembelea jukwaa la siasa.

Hivyo basi, napata jibu la kuwepo kwa viti maalum ktk bunge letu la jmt. Hayo ni maoni yangu na nipo tayari kukosolewa.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom