Jukwaa la katiba kesho kutangaza hatua za utekelezaji

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema kikao cha Kamati Tendaji kilichokaa juzi kilibariki maazimio yote yaliyokwishatangazwa awali na kusitiza kuwa kesho kitatangaza hatua za utekelezaji wake.

“Kamati tendaji iliyokutana jana (juzi) ilijadili kwa kina hutoba zote za viongozi, ile ya Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na ya kambi ya upinzani bungeni,” alisema Kibamba na kuongeza;“Baada ya kupitia yote hayo kamati hiyo ilibariki maazimio yote yaliyokwishatangazwa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari na siku ya Jumanne (kesho) tutatoa tamko litakalohusu utaratibu utakaotumika kutekeleza adhima hiyo,” alisema Kibamba.

Novemba 14 mwaka huu, jukwaa hilo liliitisha kongomano la Katiba jijini Dar es Salaam na kuelezea adhima yake ya kuitisha maandamano nchi nzima endapo Serikali ingepeleka muswada huo kusomwa kwa mara ya pili bungeni.

Pia likatumia fursa hiyo kuonya wabunge ambao wangeunga mkono na kupitishwa muswada huo uliosomwa kwa mara pili kuwa lingetangaza majina yao haradharani kama wasaliti wa wananchi waliowachagua.
 
Deus Kibamba "ban" ya Ukonga inamuwasha. Tuendelee.

Haki mahali popote pale duniani haiji bila mikiki mikiki ikiwemo kufungwa, kuumizwa na hata kupoteza maisha. Baadhi huyu DK watamuona ni mvuruga amani na kwa wengine anaonekana ni mtetezi wa haki ya walio wengi.
 
Ni biashara ya ku-justify mamilioni ya fedha za wafadhili. Tunamkaribisha lakini we will not be cowed.
 
Deus Kibamba "ban" ya Ukonga inamuwasha. Tuendelee.
Nadhani Kikwete alikuwa anatafuta support ya watu kama nyinyi alipokutana na wale 'wazee wa dar'. Inaonesha jinsi ulivyo shortsighted...yaani unatetea muswada ambao unakuja kutengeneza sheria ambayo itatengeneza katiba yenye kulinda maslahi ya serikali ya CCM kwa sababu una mapenzi mazito na Jakaya Kikwete...!? Dada yangu hii inatakiwa iwe katiba ya wananchi siyo ya kulinda maslahi ya CCM.
 
Maandamano yanaweza kufanya hivyo wakati huu ambapo muswada haujawa sheria, baada ya hapo itakuwa ngumu. Na itakuwa vizuri kama yeye binafsi akaongoza badala ya kuchochea watu wengine kufanya hivyo.
 
Namuunga mkono kibamba kwa uaamzi wowote ule atakaouchukua maana anafanya hivyo kwa masilahi ya Taifa na vizazi vijavyo maana ukweli uliopo katiba hiyo itakuwa ya ccm na si ya wananchi.
 
Back
Top Bottom