chadema ndo wanataka kuleta vita?
utakuwa una matatizo ya akili
chadema ndo wanataka kuleta vita?
Habari zenu ndugu zangu great thinkers! kwanza kabisa poleni na shida/taabu mbalimbali ya dunia hii, Ok baada ya salaam hizo leo nimekuja na hii hoja baada ya kusikia habari zikienea sana mitaani toka kwa mapaparazi wanaojiita wao ni makachero wa mbinguni wakidai mwisho wa dunia ni 21/5/2011, sasa sijui kama kuna ukweli wowote wa hili jambo?
Habari zenu ndugu zangu great thinkers! kwanza kabisa poleni na shida/taabu mbalimbali ya dunia hii, Ok baada ya salaam hizo leo nimekuja na hii hoja baada ya kusikia habari zikienea sana mitaani toka kwa mapaparazi wanaojiita wao ni makachero wa mbinguni wakidai mwisho wa dunia ni 21/5/2011, sasa sijui kama kuna ukweli wowote wa hili jambo?
SOMA MATHAYO 24
'' Wanafunzi wake wakamwendea wakamuuliza Bwana ni lini siku ya kuja kwako au Mwisho wa Dunia?
'' Akawajibu asiwadanganye mtu.
>watakuja wengi kwa jina langu
>Watakuja manabii wa uongo
>watawadanganya wengi yumkini kama wateule
> Watasema yuko huku yupo kule
> Msiwaamini hao
>>Kutakuwa na vita mahali na mahali
>>Ufalme kupigana na Ufalme
>>Taifa kupigana na taifa
>> Huo ndio mwanzo wa Uchungu!!!!!
>>Watu watakuwa wenye kupenda fedha kuliko kumpenda Mungu
>> Watawachukiwa wa kwao
>> Watoto hawatawahesimu wakubwa
>> Mioyo ya wengi itapondeka
>>Kutakuwa na njaa mahali na mahali
PALE MTAKAPOONA CHUKIZO LA UHARIBIFU LINAINGIA PATAKATIFU PAKE MJUE ULE MWISHO UMEKARIBIA
>> Ndipo aliyeko shamba asirudi nyumbani
>>Aliyepo nyumbani asiende sokoni
>>aliyepo darini abaki huko huko
>>>Aliyepo Tanganyika asiende anzibar
>>>Aliyepo Zanzibar asije Tanganyika
MWENYE KUSIKIA NA AFAHAMU MANENO HAYA!
in loving memory of myself mhh!!
Ngoja nikachukue mkopo kibaruani niponde raha kuanzia wiki ijayo mpaka tarehe 21 :biggrin1::biggrin1::biggrin1:
Una mpango wa kwenda kokote katikati ya mwaka huu? Mie nilikuwa na mpango, na bado ninao, wa kwenda kushangaa wanyama huko mbuga ya Mikumi. Pia nina mpango wa kufanya marekebisho madogomadogo katika nyumba ninayoishi kwa sababu mwenye nyumba wangu kagoma kunikarabatia. Pia nina mpango wa kukutana na watu hapa kijijini na kujuzana hili na lile kama ilivyo ada kila siku.
Lakini ati pamoja na kuwa na mipango yote hii ambayo inasubiri utekelezaji jamaa wananambia ati tarehe 21 /05 /2011 dunia yetu inafika tamati, au kwa kiswahili rahisi ni kwamba tarehe hiyo ndio 'mwisho wa dunia', namaanisha ' Kiama'.
Waliokuja na habari hizi ni jamaa fulani huko Carlifornia, Marekani, ambao wanasemekana kutumia fursa hiyo kujiongezea umaarufu kwa kutafuta air time kwenye vyombo vya habari.
Jamaa hawa waliokuja na habari hizi za 'mwisho wa dunia' ni wafuasi wa dini ya Kikristo wenye msimamo mkali wanaoongozwa na mtangazaji wa radio, Harold Camping, anayetangaza katika radio ya Family Radio Network.
Akitumia mistari ya Biblia, jamaa huyu amesema kwamba dunia itafika tamati miaka 7 ,000 kutokea mafuriko makubwa katika uso wa dunia, na kwa mujibu wa kalenda yake ni kwamba mwisho wa dunia yetu ni Mei 21.
Inasemekana hii si mara ya kwanza kwa Harold kufanya utabiri kama huu kwani mwaka 1994 kutabiri kuwa mwaka huo dunia ilikuwa ikifikia tamati lakini cha kustaajabisha hadi leo bado yupo pamoja na wafuasi wake. Siku zote amekuwa na namna ya kujitetea utabiri wake unapokwenda kombo, " Kuna wakati Mungu anakuonesha mambo lakini hakuoneshi kwa ukamilifu wote.
Ni miaka mitatu iliyopita ndipo Mungu amenionesha ukweli wote." Lakini mara hii, Harold amekuwa akisisitiza kwamba yuko sahihi kabisa tofauti na mwaka 1994 , na mara hii emungwa mkono na watu wasiopungua 50 , akiwemo Gary Vollmer, mwajiriwa katika wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ambaye amechukua likizo ya bila malipo, likizo inayokwisha tarehe 23 Mei.
Gary amesema hategemei kurejea kwa mwajiri wake kwani tarehe 21 Mei atakuwa ' amekwishanyakuliwa'.
Enewei, nimefurahi kufahamiana na kila mmoja tuliyekutana na kubadilishana hili na lile hapa kijijini. Iwapo kweli tarehe 21 litatokea la kutokea tukutane upande wa pili. Chiazzzzz.