Kwakweli mi sijui ningeomboleza kwa stail ipi??
kweli kabisa membe anatusingizia, ni yeye mwenyewe!
membe sasa aandike maumivu makali..........ukiona mtu mzima anakiri kwenye tv ya kuwa usiku wa kifo cha swahiba wake hakulala kabisa alikuwa anaangalia luninga hadi saa nane usiku ujue njozi ya uraisi ndipo ilipokatikia................hana mfadhili wa kumrundikia mapesa ili awarubuni wa sisiemu wenzake kwenye vikao vyao vya siri vya kupeana ulaji...........Benard Mende ni msilam aliyebadili dini ili akasome shule za misheni. na izo ndoto zake za linacha za kulikamia pango la magogoni naona zinamyeyukia kama barafu. mtu waliyekuwa wanampelekea kadi za michango mithili ya wafanyavo makapera wakitaka kuoa au kuolewa kafa. anajiuliza atapata wapi mchango wa 2015? labda aende kwenye miradi ya Kinana pwani ya Somalia wakateke meli.
Haya wana JF naona ni Membe na wana mtandao hapa hoja hakuna ni matusi kwa kwenda mbele. Mimi kimyaaa
Jamani mimi kaka yangu alisoma na Membe pale londo na jina lake lilikuwa hilohilo. Mwenye ushahidi naomba aseme kabla ya kuingia ukristo alikuwa nani kwa jina
Bado hapa kwetu kitatokea kama kilichotokea kwa gaddafi waendelee tu kufanya upuuzi nq kuifanya hii nchi ni ya watu kadhaa, hamna mtu aliyetegemea gadaffi watamfanyia hivi au yeye mwenyewe hakutegemea haya yote, sasa CCCm subirieni tu.....
Hivi chaguzi zetu,kuna mgombea yoyote aliyewahi kufadhiliwa na mataifa ya nje? Kama yes, ni kwa kiasi gani? One thing that most of leaders in Africa would remember the late Gaddafi, ni huruma yake kwa waliokuwa tayari kujipendekeza na kuomba misaada hata kama ni risasi za kumpindua rais au kuzima wanaompinga. Yeyote atakayeanza was his friend indeed!
Africa ni bara jeusi. Limejazwa vibaraka na majuha, hata wanamapinduzi wachache waliopo hudharauliwa na kuonekana wenye dhambi tu.
Ulaya pamoja na utajiri wao na nguvu za kiuchumi na za kijeshi walizonazo, wameungana pamoja, wanatumia sarafu moja na wana jeshi moja.
Sisi miafrika tuliolaaniwa tunapigania utengano. Usiwashangae majuha wa Libya (Kukataa maisha bora kabisa katika viwango vya kidunia, kwa kushawishiwa na dhana ya kijinga kabisa ati dikteta katawala miaka mingi, anataka kumrithisha mwanawe), hata kama angetawala mpaka kifo chake cha halali, serikali yake ilipigania ustawi wa watu wake na mataifa mengine masikini ya kiafrika.
Sisi wenye kujidai tuna demokrasia ya kuchaguana tuna nini? Kila kiongozi anayeingia madarakani anafanya ufisadi wa aina yake na kuondoka. Hiyo ndio demokrasia wanayoipenda mabeberu. Hakika hakuna hata nchi moja yenye kufuata western democracy iliyoweza kufikia ustawi wa watu wa Libya, hata hao mabwana wa vibaraka waasi (Marekani), hawakufikia ustawi wa watu wa Libya. Na Watu wa Libya watajutia kwelikweli upumbavu wao.
the time to talk to this wicked generation of leaders is truly running out................