Judge Warioba ateuliwa kuwa Mwenyekiti Tume ya Katiba

Masikini kumbe bado JF wachanga wa siasa ni wengi japo kila siku wanaongea siasa! Msitizame majina ya watu na kushangilia. Angalia ni maswala gani ya msingi yanabishaniwa katika katiba na wajumbe hasa MKT wana/wahi onyesha misimamo gani katika hayo.
 
JK anataka kutibu madonda ya salim ahamed salim aliyomsingizia kuwa ni hisbu alimua karume na kumkatisha ndodto yake ya urais anataka kurudisha mahusiano anajua salim anamachungu sana katika hili kwa hilo natilia shaka uteuzi huu utakuwa na comflict of interest.kuhusu walioba mwoga kigeugeu siku moja niliwahi kufanya mahojiano naye wakati wa mahafali katika chuo kikuu kimoja kuhusu katiba alionesha kuogopa kujibu swali langu huyu sina imani naye .Profesa baregu nimefurahishwa sana na uteuzi wake ,lakini mbona shivji amekosekana kuananini?,mtikila shujaa asiyeshindwa kesi kwanini hajawekwa ,Augustino Ramadhani sina imani naye kabisa ,ni wakati wa ujaji mkuu wake alishindwa kutoan hukumu ya mgombe binafsi ambayo mtikilia ilifungua kesi ya kudai kuwepo kwa mgobea binafsi huyu ramadhani hanasifa kabisa kuwa katika tume hiyo mwache eende kapige kinanda huko anglikan.senkondo sawa kabisa ,butiku sawa kabisa ,lete majina mengine wameyaficha au na chenge yumo
 
Timu nzuri bt naona elmaamry amezeeka sana,ataweza kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni? Au ndo wanataka kumuua? A.m nangy
 
13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb) - Pengine anawakilisha albino. Lakini Bi Helen Simba au Ananilea Nkya wangetoa mchango mkubwa zaidi ya huyu mheshimiwa.

14. Nd. Mwantumu Jasmine MALALE - huyu ni nani na ameingiaje kwenye hii katiba?

M2wantum Malale ni Mkuu wa chuo cha Kislamu Morogoro na aliwahi kuwa katibu mkuu mara kadhaa. Ni swahiba mkubwa wa JK pamoja na mumewe Mzee malale ambaye pia aliwahi kuwa katibu mkuu wizara kadhaa
 
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,
Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)
______________________________
UONGOZI WA JUU
1.
Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA
- Mwenyekiti
2.
Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino
RAMADHANI
- Makamu Mwenyekiti

WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - BARA
1.
Prof. Mwesiga L. BAREGU

2.
Nd. Riziki Shahari MNGWALI

3.
Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI

4.
Nd. Richard Shadrack LYIMO

5.
Nd. John J. NKOLO

6.
Alhaj Said EL- MAAMRY

7.
Nd. Jesca Sydney MKUCHU

8.
Prof. Palamagamba J. KABUDI

9.
Nd. Humphrey POLEPOLE

10.
Nd. Yahya MSULWA

11.
Nd. Esther P. MKWIZU

12.
Nd. Maria Malingumu KASHONDA

13.
Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)

14.
Nd. Mwantumu Jasmine MALALE

15.
Nd. Joseph BUTIKU


WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - ZANZIBAR
1.
Dkt. Salim Ahmed SALIM

2.
Nd. Fatma Said ALI

3.
Nd. Omar Sheha MUSSA

4.
Mhe. Raya Suleiman HAMAD

5.
Nd. Awadh Ali SAID

6.
Nd. Ussi Khamis HAJI

7.
Nd. Salma MAOULIDI

8.
Nd. Nassor Khamis MOHAMMED

9.
Nd. Simai Mohamed SAID

10.
Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA

11.
Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN

12.
Nd. Suleiman Omar ALI

13.
Nd. Salama Kombo AHMED

14.
Nd. Abubakar Mohammed ALI

15.
Nd. Ally Abdullah Ally SALEH


UONGOZI WA SEKRETARIETI
1.
Nd. Assaa Ahmad RASHID
- Katibu
2.
Nd. Casmir Sumba KYUKI
- Naibu Katibu
 
Mkuu sidhani kama Shivji hatatumika in one way or another. Hata maoni yake atakayotoa kuhusu katiba iweje yanafaa. Ila ningefurahi sana kama ange-Chair hii Tume. Tatizo ni kwamba watawala wanataka watu wanaoweza kuwa-manipulate, Shivi ni mtaalam huwezi kumuagiza afanye upuuzi unaotaka wewe, hayupo tayari ku-impair taaluma yake kwa mwanasiasa mbumbumbu wa sheria, kama ambavyo mahakama zetu sasa zinavyokubali kutiwa najisi na wanasiasa.
Shivji is no saint. Hao walioandikwa kama kweli wamo wanatosha sana. Wengine wapate nafasi ya kuongea wakiwa nje. Ila uwepo wa Kabudi unanichukiza.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Shivji vipi?

Amependekezwa na Chama au ASASI gani? Yeye ni mwanachama wa CCM na CCM hawawezi kumpendekeza.
Inawezekana kuwa Warioba na Butiku wamependekezwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (sina hakika kama Shivji naye ni wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere)
 
kwa vile uteuzi huu sio kama maandiko matakatifu, basi JK naaone haja ya kumuongeza Prof.Shivji kwani dhamira siyo sura ya nani but input, mchango wa mwanazuoni huyu adhimu ni muhimu sana na hata yeye atajihisi vema
 
Shivji angefaa zaidi kuwa mwenyekiti zaidi ya Warioba.Nina wasiwasi kama Warioba atakubali kumpunguzia rais nguvu
Babu M.
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Ila JK amefanya fair kumteua Jaji Warioba, Prof. Shivji ndio angekuwa the best ila kumtumia Shivji angetupatia katiba bora kabisa kwa kuzingatia Shivji ndie mtaalam bingwa wa Sheria ya Katiba wa UDSM na ndie mkosoaji mkuu wa process iliyotupatia katiba zuga ya JMT ya mwaka 77!.

CCM imeweza kudumu madarakani kwa kutumia loop holes za katiba mbovu iliyokiwepo hivyo Shivji angeleta katiba bora ambayo ingeitupa CCM nje outright, hivyo kumteua Shivji ingekuwa sawa na CCM kulikata tawi ililokalia!.

If you can't get what you want, just take what you get!. Tumpe Jaji Warioba ushirikiano stahiki!. Haya na wale ambao wao kazi yao ni kulaumu kila jambo JK, hili nalo sii jema?.
 
Back
Top Bottom