Judge Warioba ateuliwa kuwa Mwenyekiti Tume ya Katiba

Taarifa za kuaminika toka Magogoni ni kuwa Rais Jk ameteua tume ya katiba mpya ambayo itaongozwa na Jaji Joseph Warioba!


Katika timu hiyo wapo
Profesa Mwesiga Baregu,
Dk Salim Ahmed Salim,
Ndugu Joseph Butiku,
Dk Sengodo Mvungi,
Esther Mkwizu,
Yahya Msulwa,
Said El Maamry

Wapi Issa Shivji
 
Cha muhimu kwa sisi wananchi ni ku-outline mambo ya msingi yanayofaa kuwemo kwenye katiba mpya na yasiyofaa kuwemo ili hata tukiwa matembezi vijijini kwetu tuweze kuwaelewesha babu,bibi na wajomba zetu kwa urahisi zaidi.
 
kuna kitu kikwete anataka kufanya'huyu mtu aweka taifa mbele kakiacha chama chake'kama ni kweli nitaanza kumweshimi kikwete
 
Panapostahili kupongeza tuwe wazi tupongeze, hii ni nchi yetu hakuna wakutujengea! Mimi nampongeza Mh rais kwa uteuzi wake!

Watanzania kwa makundi yote tuiombee hii tume ifanye kazi yake sawasawa na matakwa ya watz!

Mungu ibari tz!
 
Wapi prof Safari, Shivji, Jenerali Ulimwengu, Ananilea Nkya kidogo hawa hawana nidhamu ya woga ila sio mbaya is a good begining... Na je waislamu tutapata haki yetu? Kwa tume sidhani! Ila sijui
 
Siku tunajadili rasimu ya katiba pale karimjee mzee warioba alipopewa nafasi kuchangia alianza kwa kuchangia kimagamba style, wahudhuriaji wakamzomea akabadili style na kuchangia kwa muono wa wananchi, ndipo akapata credit, sasa nawaonya nyinyi nyote mnaofurahia uteuzi huu, Bado kitambo kidogo sura halisi ya sinde warioba mtaiona!!!!
 
JK mbona amekuwa mtu mwema na mkarimu hivi ghafa?Hii kamati ikipendekeza muda wake uongezwe ili katiba ikamilishwe sidhani kama kuna atakaye bisha.lol!
Anyways timu nzuri, hongera JK.

Hii inaitwa 'contaiment strategy'. Yaani anachofanya ni kutuliza munkari wa watu ili amalizie kipindi chake, na mwisho wa siku ndiyo utajua kuwa alikuwa na nia ya dhati au ni delayment strategy. Kuna tume nyingi sana zimeundwa huko nyuma kama vile Tume ya Nyalali(vyama vingi), Tume ya warioba(rushwa), Tume ya Kisanga(muungano) etc. Ila hakuna any positive news kutoka kwa yale yaliyopendekezwa.

Mimi bado ninaamini kuwa mchakato huu ni kiini macho na hakuna jipya. Waswahili husema safari mguu wa kwanza.. ukiisha jikwaa mguu wa kwanza basi ujue safari hiyo haipo tene na kwenye hili tuliisha jikwaa pale CCM walipoingiza ushabiki wa chama zaidi na kuona katiba mpya ni mbinu ya kuwatoa madarakani. Ningekuwa nina imani sana na Tume hii kama sheria ingeweka wazi kuwa majukumu ya tume ni pamoja na kusimamia kila kitu na mtu akiteuliwa hakuna wa kumtoa mpaka mchakato ukamilike. Na uteuzi huo ungewekwa wazi kabisa ni watu wa kutoka makundi gani wawemo.
 
mwenyekiti ni jaji joseph warioba na makamu wake ni jaji augustino ramadhani.
ina wajumbe 30 , 15 kutoka tanzania bara na 15 kutoka tanzania visiwani.

Katika timu hiyo wapo .
.profesa mwesiga baregu,
.dk salim ahmed salim,
.ndugu joseph butiku,
.dk sengodo mvungi,
.esther mkwizu,
.yahya msulwa,
.said el maamry  N.K

timu nzuri hivyo tunasubiri utumishi uliotukuka.
 
Back
Top Bottom