Joyce Mhavile ashauriwe

babykailama

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
251
243
Ni wazi kuwa siku za karibuni, vipindi vilivyoanza vyema vya ITV kv. Dakika 45, Malumbano ya Hoja na Kipima Joto sasa vinapwaya na kukosa mvuto.

Tafadhali fuatilia uone ni wapi hao waandaaji wa vipindi wamekosea Kitaaluma.

1. Kijana wa kipindi cha Dk 45 akaribishe mchanganyiko wa Wataalam mbalimbali na si viongozi tu wa Serikali na maswali yake yaonyeshe umahiri ktk tasnia ya habari. Mwonyeshe hata vipande tu vya Hard Talk kwa wiki yote akiwa peke yake studio ajifunze!!
Mfano. vipindi vijavyo waite, Kiongozi wa Chama cha Madaktari, Kiongozi wa TUCTA, Viongozi wa vyama vya upinzani, Viongozi wa vyama vya Walemavu, Viongozi wa Taasisiza Haki za binadamu, Watu waliokuwa tishio ambao wamejirudi na kuwa watu wema ktk jamii, Kiongozi wa Wazee waliotumika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

2. Couple (Original wa awali) wa kipindi cha Malumbano ya Hoja, kama wasimamizi wawe serious katika ku moderate mijadala na uchaguzi wa washiriki uwe 'balanced'. Waache kuongea sana wao, vinginevyo wawe washiriki tujue moja.


3. Mzee wa kipindi cha kipima joto, angalia kwa upya uchaguzi wa mada nyeti na pia urudi kama zamani ambapo wawakilishi wa makundi mbalimbali walikaribishwa bila kukosa wawakilishi wa wananchi - walala hoi na pia wanaharakati. Na kwa nini hampokei simu zetu kila wakati mnajidai mko buzy??? Tena wa kutoka nje ya nchi nadhani ndio kabisaaaaa,mnaogopa nini?

Mada nyeti zaweza kuwa: Marekebisho ya Katiba , Muungano - Tanzania, Mafisadi Tz, Digrii feki nchini, Maslahi vs wajibu wa Wabunge, Sayansi & Teknolojia Tanzania, Michango ya Mitandao ya habari ktk maendeleo ya nchi na dunia kwa ujumla, Malalamiko ya wananchi ya migogoro ya ardhi.


Bado sijapoteza kabisa imani yangu katika ITV, Mhavile you can make it!
 
Yaani inaboa kweli hakuna uwakilishi wa wananchi ni kama imekuwa jukwaa la serikali
kujisafisha,sijui wametishwa!!!
 
Joyce Mhavile huwa hashauriki daima!!!!!!! Nahisi umempigia mbuzi gitaa pamoja na kwamba hoja zako ni EXCELLENT!
 
Inaonekana hiyo ni agenda ya hao viongozi wa vyombo hivyo manake inasemekana hata huyo Mzee Mengi na wanae wote huwa hawapendi kusikiliza maoni ya nje, basi shauri yao mwisho wa kutosikiliza maoni ya maana ni kutangaza biashara zao tu.
 
Thinktank cabinet ya IPPmedia ina matatizo makubwa, probably inaundwa na ma conservatives ambao wameshindwa kuendana na wakati kabisaa, mambo ni yale yale tuu miaka nenda miaka hakuna maboresho
 
Si uanzishe vipindi vyako na uwauzie stesheni za TV kama ni sahali.
 
Unapanga mechi kikocha eeenh? Upo nje ya uwanja unaanza; wewe cheza hivi, wewe cheza vile. Haya, nadhani wahusika watakusikia, ila sina uhakika kama watakufatisha unavyotaka.
 
Ndo matatizo haya ya kina mama kujifanya wanajua wao kila kitu


Hivi Fidel80 ugomvi wako na kina mama hauishi tu? Hujaona akina baba wanaojifanya wanajua kila kitu wewe? Mtu mhasibu lakini anajifanya anajua mpaka kung'oa/kutibu meno! Mh, ngoja nikimbie nisije nikaanzisha malumbano ya hoja hapa.
 
Joyce's pigheadedness and inflexibility can comfortably be put down to her spending of life without one permanent husband. This woman has been changing husbands on annual basis and that tendency has greatly affected her mentality, her disposition as well as her job performance. This problem therefore can be completely solved by finding her a man to eventually be her life partner and someone must volunteer counselling her against the behaviour of changing men.
 
Back
Top Bottom