Joshua Nassary, kulikoni...?

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,723
Ni muda kidogo umepita tangu kikao cha bunge kuanza bila kumsikia Mbunge machachari Mh Nassary.
Kwani imekuwa tofauti na kauli zake akiwa kwenye Kampeni kwamba "Mimi kwangu ni vitendo tu na wananchi mtaniona nikifika bungeni''.
1.Au ile kauli yake aliyoitoa ya kuigawa nchi kwa majimbo na kuandamwa sana na vingozi mbalimbali wakiwa na wachama chake imemfanya aingiwe woga.?
2.Ama ni Kamanda Mkuu amemweka chini na kumwambia achunge sana anachosema?
3.Ama Mh Nassary ni kwamba wananchi wako hawana shida yeyote ambayo inastahili wewe kuwasemea bungeni?

Please Nassary ulituahidi wananchi wako wa Arumeru tena kwa kusema "HAKI YA MUNGU NITAKULA NAO SAHANI MOJA MPAKA KIELEWEKE''
4.Ama ndiyo kimeshaeleweka hivyo?
Na usikubali kutishwa na wewe ukatishika kwani safari ndo kwanza unaianze sasa unaonyesha kukata tamaa mapema mno.
 
mbona aliongea juzi kati hadi naibu spika akasema hivi'' mh nassari unaongewa kwa sauti ya juu sana kana kawamba unapigana au unagombana na mtu, jamana waheshimiwa wabunge tuongee kwa sauti ya kawaida na hoja zetu zitasikika''

katika kujibu nassari alimjibu hivi '' hii ndio sauti yangu na ndivyo ilivyo ni sauti iliyojaa hekima na mamlaka, inafundisha, inakemea pia''

naibu spika akamwambia basi endelea......nadhani mkuu session ile ilikupita ,ilikuwa wiki ya kwanza ya kujadili bajeti ya serikali iliyowasilishwa na mgimwa
 
Manuu una majeraha ya kugaragazwa msalimie Sioi huko aliko.Tuliyompa kura tunaimani naye!
 
Anasubiri show nyingine ya sugu akarushe mistari.

Nipige Nisipigeee?.........Pigaaaaaaa aaaaa
Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii?............ .......Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mahindi yanaota na rangi ganiiiiiiiiiiiii?............K ijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mpunga unaota na rangi ganiiiiiiiiiiiiii?............ .Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?............... ............Kijaniiiiiiiii.
Piga makofi na vigelegele kwa chama cha mapinduzi.
 
Manuu: Hata JK katika kiny'anganyiro cha kuutaka uraisi kwa awamu ya pili aliwaahidi wananchi wa Kigoma kua wakimchagua Kigoma itakua DUBAI!
 
mbona aliongea juzi kati hadi naibu spika akasema hivi'' mh nassari unaongewa kwa sauti ya juu sana kana kawamba unapigana au unagombana na mtu, jamana waheshimiwa wabunge tuongee kwa sauti ya kawaida na hoja zetu zitasikika''

katika kujibu nassari alimjibu hivi '' hii ndio sauti yangu na ndivyo ilivyo ni sauti iliyojaa hekima na mamlaka, inafundisha, inakemea pia''

naibu spika akamwambia basi endelea......nadhani mkuu session ile ilikupita ,ilikuwa wiki ya kwanza ya kujadili bajeti ya serikali iliyowasilishwa na mgimwa

Mwache ajisemee mkuu...magamba huropoka bila uchunguzi..kawaida..waziri mkuu(vurugu za arusha),nchemba(kuhusu kiasi kilichotengwa kwa ajili ya maendeleo kwenye 2012/13 budget)..u name it.
 
manuu Kama unaangalia cnn, aljazeera, citizen na kusoma magazeti ya New York times na Daily mail huwezi kumwona wala kumsikia Nassari.
 
Last edited by a moderator:
Huwa anachangia kwa maandishi na kwa maneno pia sema hujabahatika kumsikia au una hila naye
 
mh nassari mbona mara nyingi sana anaongea bungeni,anauliza maswali,kwa kweli ukisema hafanyi kitu utakuwa unamsingizia au huwa hauangalii vpindi vya bunge.dogo anafanya kazi.
 
naona una umia sana asiposema kile unachotaka kukisikia, Dogo janja yupo fiti , ile mambo walijaribu kumyumbisha ila wao wenyewe wamekaa pembeni , BIG DOGO janja, endelewa kwakilisha T 2015CDM
 
Babu,uwe unauliza watu wanaongalia bunge ..Jamaa mbona anaongea

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Tembelea pia tovuti ya bunge utaona michango yake,kama ulimpa kura haikwenda bure ndugu!
 
Jamani Mhe. Nassary ni mpya BUNGENI kwa hivyo mpeni muda ==== it is too early to do things. One has to learn first and see the step of others before jumping into the music to dance. We know he is capable and learned. Please do not give him QUESTION OF DOUBT PLEASE.

USIHOFU MHE. KIJANA WETU NASSARY
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom