Joshua Nassari apitishwa kura za maoni ya mkutano mkuu wa CHADEMA - Arumeru

wanaouana ni CCM au CDM???

Wanaouna ni wale wanaowekeana sumu toka enzi za kolimba,wanaotumiana majambazi toka enzi za nicas mahinda(r.i.p),wanaologana chamani na kushinda pwani za bagamoyo kila week end!
 
Nipo arumeru kwa sasa na wakuu wapo kwenye kikao muda huu,nipo hapa kwa gharama za jasho langu.....Mtazamo wako wa kuwa mimi ni fundisho hahahhahahahaaaaaaaaaaaa yawezekana umeishia hapo kufikiria lakini bado unauwezo wa kufikiri zaidi ya hapo.
Mzee Tunte..hujanusa chochote utumegee na sisi tuliombali..kuna mtu alikuona chini ya mwembe ukivizia tunakutegemea mkuu.
 
MNYISANSU,
Hakuna povu tunawekana sawa tu, povu lipo kule kwenye thread ya 19M, Chadema wenzako wataka kutoana macho.
Wewe huoni kazi ya visibility study....vipi mgombea wetu Sioi anaendeleaje au umehama kambi.
 
hatuna haja kumshukuru mungu ndugu wana cdm,kwaqni ndio mwanzo mzuri,mungu ibariki cdm mungu wabariki wanapigakura mungu nmbartiki mgombea wetu kwani ndio chaguo la watanzania wote tuko pamoja:A S 465:
 
Mzee Tunte..hujanusa chochote utumegee na sisi tuliombali..kuna mtu alikuona chini ya mwembe ukivizia tunakutegemea mkuu.

Tuntemeke siyo chadema hata kidogo. Huyu ni pro-ccm na yuko kazini kuvuruga cdm akijifanya ni chadema ili kuwachanganya tu.

Niliwahi msikia Nape akisema aliwaomba wakuu wake wampe ruhusa ya kubadili muundo wa ofisi yake badala ya kuendelea na Tambwe hiza anahitaji mfumo mpya wa propaganda nao ni kuwafuata vijana huko huko waliko yaani kwenye mitandao kama JF, FB, tweeter, n.k maana vijana hawaji mikutanoni wako kwenye mitandao ambako chadema ndo wamewapata wengi huko.

Sasa hawa akina Ritz, Rejao, MS, Tuntemeke, na wengineo ni team aliyoipanga nape ingawa wengine ni wa siku nyingi JF amekuja waimarisha zaidi.

So chadema mnapochangia hoja za watu kama Tuntemeke muwe na mtizamo huo kabla hamja fika hata pg ya 3, 4,5.....25.... Msiniulize source...za mbayuwayu....
 
Pongezi sana Nassari kwa ushindi wa kishindo..

Isingewezakana hata kidogo kushindwa kwenye kura za maoni kwa nguvu aliyepewa na viongozi wa Chadema Arusha.

Lema, pamoja na wanachama wa Chadema zaidi ya 50 walimfanyia harambee Nassari, na kuchanga Sh10 milioni na magari manane.

Wagombea wengine walikuwa kama watoto yatima hakuna hata mmoja aliyechangiwa Bajaji au Toyo.

Huo uchaguzi wa kura za maoni ilikuwa sawa sawa kuwapambanisha Villa Squad na Real Mardrid...unategemea nini?

Utahangaika sana lakini Fitna za udini Arumeru hazitafanikiwa.
 
Vipi Jungu la kabila la Washiri aliloibua Tendwa limefika wapi?
Hawawezi kuliendeleza kwa vile mtoto wao anataka kuchinjiwa baharini.
CCM wana kazi safari hii hakuna cha hijab wala mdogo wake mtandio.
 
Hongera kamanda Nassary, Hongera makamanda waliomtia kajoto, sasa unganisheni nguvu yenu iwe moja, kwa maslahi ya chama chenu na wananchi wa Arumeru. Kazi iliyobaki ni moja tu, kuhakikisha Nassary anashinda beyond 90%
 
Hawawezi kuliendeleza kwa vile mtoto wao anataka kuchinjiwa baharini.
CCM wana kazi safari hii hakuna cha hijab wala mdogo wake mtandio.

Nakuambia kila Jungu lao linachemsha.Wewe fikiria mtu mzima na akili yake anatoka Dar hadi Arumeru kwenda kuropoka eti Lema akienda Arumeru damu itamwagika.
 
Ndugu Wanabodi

Kijana Joshua Nassari Amepita Kura Za Maoni Kwa Asilimia Zaidi Ya Tisini, Kuiwakilisha Chadema katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki.



Kura Zilizopigwa zilikuwa 888, Na Nassari Kapata 800 anaemfuatia ni Anna Mgwira 26.





Jumla wagombeaji walikuwa saba, Kwa Majina Ni;



1. Joshua Nassari
2. Anna Mgwira
3.Anthony Msami
4. Godlove Temba
5. Yohhane Kimuto
6. Samweli Shami
7. Rebbeca



Kura hizi zimepigwa leo katika ukumbi Meru Garden maeneo ya Kwa Aloisi Maji ya Chai, wagombeaji wote waloshindwa wamekubali matokeo na wana furaha tu kumuunga mkono kijana wetu Nassar

na sasa kinachoendelea ni katibu mkuu Dr. Wilbrod Slaa anaendelea kuhutubia nyomi ya wafuasi wa Chadema walofurika hapa.

habari hizi Source yake ni mimi mwenyewe niko tukioni. Picha baadae au kesho tukializa hizi pilika

Asante kiongozi
 
Back
Top Bottom