Joseph Sinde Warioba kaishia wapi?

KyelaBoy

JF-Expert Member
Nov 9, 2008
206
22
Nauliza Mh Warioba mbona kimya,hapo zamani alikuwa na kawaida ya kutoa maoni au kushauri juu ya mustakabali wa nchi yetu pale Wakubwa walipokuwa wanafanya madudu yao.Lakini baadaye tukasikie kuwa nae anatishwa na wakubwa kuwa watampeleka mahakamani kwa madai ya ufisadi,hapo akajitetea kidogo na sasa sijui ndio KANYWEA kwa kuogopa kufikisha mahakamani kwani kwa jinsi masuala yanavyoenda ndani ya chama chake cha CCM na yeye kukaa kimya nashindwa kumwelewa kama yule Warioba jasiri kakaa kimya au ndio kaona ni kama KUMPIGIA MBUZI ZEZE?
 
Yeye ni mtume? anaogopa watu kama wewe wanaodhania kuwa lazima Warioba aseme neno asiposema neno hakuna story vijiweni, wala magazeti hayahuziki, after all mmeisha sema naye ni FISADI kitu ambacho kwa misimamo yangu kwa kuwa yeye ni CCM basi zawadi ya ili neno baya analo, maana hakuna msafi CCM!
 
hakuna msafi katika ccm wote ni mafisadi hakuna msafi katika chama kile ni wezi wauaji majambazi na waongo na matapeli
 
Ha ha ha warioba angekuwa fisadi si angekuwa anakunywa whisky na sio gongo,,,,,,,ooopss,,,,,,,,,did i say that?
 
Hii ni blackmail,

Wengi wlio CCM kila mmoja wao atakuwa kuna ka-ufisadi alifanya mahala fulani wakati akiwa mtumishia wa umma, na kila anayejaribu kukemea maovu, mafisadi wa sasa watajaribu kumkumbisha madhambi yake mwenyewe ya huko nyuma na wazee wetu wengi waoga sana tangia walipomwona Mramba na Yona kizimbania wote wameufyata!

Na asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe!
 
Nauliza Mh Warioba mbona kimya,hapo zamani alikuwa na kawaida ya kutoa maoni au kushauri juu ya mustakabali wa nchi yetu pale Wakubwa walipokuwa wanafanya madudu yao.Lakini baadaye tukasikie kuwa nae anatishwa na wakubwa kuwa watampeleka mahakamani kwa madai ya ufisadi,hapo akajitetea kidogo na sasa sijui ndio KANYWEA kwa kuogopa kufikisha mahakamani kwani kwa jinsi masuala yanavyoenda ndani ya chama chake cha CCM na yeye kukaa kimya nashindwa kumwelewa kama yule Warioba jasiri kakaa kimya au ndio kaona ni kama KUMPIGIA MBUZI ZEZE?

Mafisadi walipomuona anachonga sana, wakapenyeza ya kwake ya Meremeta, akaiona Keko ileee ikabidi aufyate!
 
kwa sasa yupo South anapata matibabu,sijui kwa nini ameugua wakati huu ingali tunahitaji busara zake kwenye uchaguzi mkuu!
 
Ha ha ha warioba angekuwa fisadi si angekuwa anakunywa whisky na sio gongo,,,,,,,ooopss,,,,,,,,,did i say that?

Hii myth ya kwamba Mzee Warioba anakunywa whisky/ gongo sijui inatoka wapi, huyu mzee hanywi kilevi chochote. You will be hard pressed kumkuta anakunywa hata white wine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom