Joseph Selesani achangia kwa mara ya kwanza bungeni baada ya ajali

Ston Merchant

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
393
103
Awapongeza viongoz mbl mbl wa kitaifa kwa ushirikiano kipindi cha ajali na msiba...

1. Pongezi......Mwenyezi Mungu, CHADEMA, Jakaya Kikwete, Edward Lowasa, William Lukuvi, Anna Makinda, Agrey Mwandri, Reginald Mengi, Mizengo Pinda, James Mbatia, Augustion Mrema, Madaktari na watu wte kwa ujumla.

2. Bajeti: Asema bajeti ya wizara ya Nchimbi iongeze pesa idara ya polisi especially kwenye gharama za mafuta kwani alipopata ajali, gari la polisi liliisha mafuta walipofika kituoni hivyo kumlazimu dereva wa gari la polisi kutumia pesa zake binafsi kuongeza mafuta ili wawafikishe hospitali.

Source: Bunge Live.!

Nawakilisha..
 
Jimbo la rombo matatizo ni mengi amepona sasa arudi kwa wananchi kwan kero ni nyingi
 
Jamaa kachemka, yani shukrani kachukua zaidi ya dk 5...halafu anatoa shukrani kwa watu ambao angewapigia simu, kwenda nyumbani kwao au kutumia njia nyingine yoyote kuwasiliana nao na kuwashukuru na sio kuwataja pale bungeni kama sehemu ya kurushana.
 
Kama alivyokuwa kaka yake, kauli zake leo ni za kurudi CCM. Amewafagilia kwelikweli kuliko hata viongozi wake wa CHADEMA ambao amewakumbuka mwishoni kabisa.
 
Amewapongeza ccm kwa nguvu na lugha iliyomaanisha kupongeza! Alitumia maneno hafifu kuwapongeza chadema!
Sijui kama ni makusudi ama ni udhaifu wa kibinadamu.
 
hv hata kushukuru tu ni deal jamani? Kushukuru kunahusishwa na kurudi CCM? Kwa lipi?.. Hii hapana!
 
Amewapongeza ccm kwa nguvu na lugha iliyomaanisha kupongeza! Alitumia maneno hafifu kuwapongeza chadema!
Sijui kama ni makusudi ama ni udhaifu wa kibinadamu.

Nilichogundua ni kwamba baadhi ya wanachama wa Chadema tumejengewa dhana potofu sana kuhusu Mhe.Selasini kwa hiyo kila atakachoongea kitajaribu kubetuliwa ilimradi aonekane wanavyotana waliotujengea hiyo dhana! Tuwe makini na hili kwangu mimi sioni baya alilolifanya mhe.selasini.
 
Jamaa kachemka, yani shukrani kachukua zaidi ya dk 5...halafu anatoa shukrani kwa watu ambao angewapigia simu, kwenda nyumbani kwao au kutumia njia nyingine yoyote kuwasiliana nao na kuwashukuru na sio kuwataja pale bungeni kama sehemu ya kurushana.

Binafsi nimeanza kuona kwa mbali dhamira na chuki binafsi zikipandikizwa juu ya Mhe.Joseph Selasini. mKwa kusema Ahsante kwa njia ya simu na kusema ahsante (Live on TV) kuna tofauti kubwa sana..

Wakati huo huo mkumbuke kuwa Mwigulu Nchemba alisema kuwa Chadema tulimtupa Mhe.Selasini baada ya ajali...

Leo ametuma ujumbe kwa Mwigulu na Taifa kwa ujumla kuwa hakutupwa baada ya kuwashukuru!..
 
Kwanini hajakanusha maneno ya Mwigulu Nchemba kuwa wakati akiugua viongozi wa chadema walimtenga hata simu hawakuwa wakipiga?Inaweza kuwa kweli?Mwigulu alisema maneno hayo bungeni siku chache baada ya tukio la Ulimboka akitaka chadema wasilivalie njuga suala hilo kwani mbunge wao hata hawamjali.Nilitegemea mh.Selasini akanushe hilo speech yake ya kwanza bungeni.May be ameamua kumpuuza.
 
Jamaa kachemka, yani shukrani kachukua zaidi ya dk 5...halafu anatoa shukrani kwa watu ambao angewapigia simu, kwenda nyumbani kwao au kutumia njia nyingine yoyote kuwasiliana nao na kuwashukuru na sio kuwataja pale bungeni kama sehemu ya kurushana.
Agree with you Mkuu, kapafanya Bungen kama kwenye band, alisahau tu kuwa anasema PapaJK, papa Lukuvi na papa... aliboa sana, shkruani zilikuwa za kinafinafiki
 
Nilichogundua ni kwamba baadhi ya wanachama wa Chadema tumejengewa dhana potofu sana kuhusu Mhe.Selasini kwa hiyo kila atakachoongea kitajaribu kubetuliwa ilimradi aonekane wanavyotana waliotujengea hiyo dhana! Tuwe makini na hili kwangu mimi sioni baya alilolifanya mhe.selasini.

Kosa alilofanya mheshimiwa ni kutumia mda mrefu kuwashukuru waliomsaidia wawe kutoka CCM au Chadema. lakini jabo la kushukuru ni lakiugwana kabisa na hakuna kosa
 
Kwanini hajakanusha maneno ya Mwigulu Nchemba kuwa wakati akiugua viongozi wa chadema walimtenga hata simu hawakuwa wakipiga?Inaweza kuwa kweli?Mwigulu alisema maneno hayo bungeni siku chache baada ya tukio la Ulimboka akitaka chadema wasilivalie njuga suala hilo kwani mbunge wao hata hawamjali.Nilitegemea mh.Selasini akanushe hilo speech yake ya kwanza bungeni.May be ameamua kumpuuza.

Hilo Mhe.Selasini alishakanusha na mimi nilileta Habari hiyo hapa kutoka kwenye ukurasa wake wa Facebook.. Sidhani kama ingekuwa na maana tena kama angeendelea kumjibu bungeni
 
Fanya subira tu. Familia hii ina historia ya kuyumba sana. Kama umemsikia leo Selasini ungegundua kule CHADEMA sio kwake.

Nimemsikia sana!
Wanaodhani na kusambaza uvumi huo ni yale masalia yaliyokosa kura za kutosha kwenye kura za maoni 2010. Selasini ataendelea kuwa Chadema na mimi bado nina Imani naye.
 
Back
Top Bottom