Joseph Kussaga na ufisadi wake katika entertainment Tanzania

Mimi ni mmojawapo wa watu wake wa karibu ambao katika wachache waliofanikiwa kujikwamua kutoka kwenye himaya yake na nimeamua kujitoa muhanga na kuweka hadharani chochote wana JF ambacho kinawakwaza kuhusiana na Ufisadi unaoendelea kwenye burudani Tanzania.

Kwakuwa ningependa kufafanua kimpangilio ndiyo maana nimeweka vipengele hivyo hapo juu ili niweze kuvifafanua inapobidi. Kutokana na ufisadi huu kuwa mkubwa na wenye network nyingi ningependa kufafanua kipengele kwa kipengele kama nilivyoviorodhesha hapo juu lakini iwapo ntatakiwa kufanya hivyo.
.

Mzee mbona unamfire back boss wako wa zamani? Amekupiga chini nini? Na wewe umejikwamua kiuchumi katika mwamvuli wake huo huo?

Haya fafanua sasa!
 
Dah! hii Thread itaondolewa mda sio mrefu maana ni majungu tupu.. Afro una kula ban siku 90
Asiyeonekana hajamuona bado tu!!! Anataka kuhamishia Global Publisher na Ze uchungu hapa naona.

Mkuu Afro sema vitu kwa uhakika, sema mwaka fulani alimwibia saida kaloli (mfano) milioni ngapi kwa mkataba feki? Au alimpa ajira fulani baada ya kutembea naye walikutana hotel fulani? au kiingilio cha tamasha la Mr 2 (mfano) la Ukumbi fulani siku fulani liliingiza sh. kadhaa ukumbi ulikata sh, ngapi? ngapi zililipia gharama zingine kama usafiri lunch, promotion n.k na sh ngapi zilikua za msanii na ngapi zake K mwisho alimwingiza msanii husika kingi kwa kulamba cha juu kiasi fulani, hapo ndio tutakuelewa la sivyo Mkuu hapa sio mahali pako, wala hoja yako haiwezi kutupa joto la kuisoma.

Thibitisha la sivyo napendekeza Permanent Ban
 
inaweza kuwa kweli nami najua ni kweli katika baadhi ya mambo hapo hasa hilo lakuibia wasanii baadhi ya haki zao, ikiwamo pesa za matamasha , kuwagawa wasanii katika makundi na mambo kama hayo.

swali kwako AFRO, Je ni mbinu gani bwana Kussaga hutumia kukwapua , haki na stahili za wasanii.?
Kwenye haki za msanii mara nyingu husimamiwa na bwana Ruge,Yeye Kussaga anachofanya ni kumbana na kulazimisha msanii kusaini mkataba anaoutaka yeye kwenye tamasha mabalo kussaga anataka msanii huyo aperform. kwa mfano,kuna tamasha la la Fiesta kuzunguka mikoa karibia 10 na tamasha hilo litachukua miezi mitatu kwa ujumla.lakini anachofanya anamsainisha msanii mkataba miezi miwili kabla na mojawapo ya sheria za mkataba huo ni kutokea siku msanii anaposaini mkataba huo,msanii haruhusiwi kujihusisha kwenye shughuli yoyote ya kisanii hadi mkataba huo utakapoisha. Inamaanisha msanii atakuwa kifungoni kwa miezi mitano bila kufanya chochote. na kwenye makubaliano ya malipo anawalipa kiwango anachotaka yeye na iwapo anataka ushiriki kwenye tamasha hilo na ukaonyesha hali yoyote ya kutoridhika na mkataba huo basi atakwambia kabisa huo ndiyo mwisho wako kiusanii na kinachofuata ni kwenda moja kwa moja libraly na kuvunja cd yoyote yenye sauti yako na nyimbo yako yoyote hata kama umeshirikishwa haitasikika kwenye kituo cha CLOUDS FM. Malipo ya msanii always yanakuwaga ni asilimia 25 ya pesa aliyoomba kwa wadhamini kwa ajili ya kumlipa msanii kwenye ushirikishi wake wa Tamasha.
 
Umalaya,
Kama nilyowahi kuyasoma kwenye mjadala wa MR 2 n ruge,kuna mdau mmoja alitoa hoja kuhusu bwana Ruge ya kwamba ili kumtoa msanii ni lazima alale nae ndiyo amtoe...hoja hiyo ni ukweli mtupu na si kwa wasanii tu bali mtu yeyote mwenye jinsia ya kike akija kuomba msaada wowote wa kimaendeleo ni lazima avue chupi.

Nikija katika suala la Bwana Kussaga,ni vile vile kama Ruge ila yeye kwa kiwango cha juu zaidi. yeye ni kwa wanawake wa wafanyakazi wake yani watangazaji,vitengo vya udhamini vinavyosimamiwa na wanawake,wanafunzi walomaliza vyuo vya uhandishi wa habari na kutaka kuja kufanya practical Clouds FM. Na kibaya zaidi,katika kila tamasha analofanya anatenga complimentaries 50 kwaajili ya kina dada ambao anauhusiano nao na anajua mwisho wa siku watampigia simu kuomba complimentary na ni vigumu kwa yeye kuwanyima kwakuwa anajua kinichoendelea.

Hii nzito ila nimeipenda na ikimuvuzishwa nitasikitika sana. Bw Afro nasikia kuna mdogo wake wa huyu Don naye mambo yake ya kula vibinti ktkt idara hiyo ni kawaida kweli hii kitu? Weka data watashindwa kuimuvuzisha hii naifananisha na ile ya MMKJJ ya "Huyu ni nani" so inafaa kuendelea kuwepo!
 
Kwenye haki za msanii mara nyingu husimamiwa na bwana Ruge,Yeye Kussaga anachofanya ni kumbana na kulazimisha msanii kusaini mkataba anaoutaka yeye kwenye tamasha mabalo kussaga anataka msanii huyo aperform. kwa mfano,kuna tamasha la la Fiesta kuzunguka mikoa karibia 10 na tamasha hilo litachukua miezi mitatu kwa ujumla.lakini anachofanya anamsainisha msanii mkataba miezi miwili kabla na mojawapo ya sheria za mkataba huo ni kutokea siku msanii anaposaini mkataba huo,msanii haruhusiwi kujihusisha kwenye shughuli yoyote ya kisanii hadi mkataba huo utakapoisha. Inamaanisha msanii atakuwa kifungoni kwa miezi mitano bila kufanya chochote. na kwenye makubaliano ya malipo anawalipa kiwango anachotaka yeye na iwapo anataka ushiriki kwenye tamasha hilo na ukaonyesha hali yoyote ya kutoridhika na mkataba huo basi atakwambia kabisa huo ndiyo mwisho wako kiusanii na kinachofuata ni kwenda moja kwa moja libraly na kuvunja cd yoyote yenye sauti yako na nyimbo yako yoyote hata kama umeshirikishwa haitasikika kwenye kituo cha CLOUDS FM. Malipo ya msanii always yanakuwaga ni asilimia 25 ya pesa aliyoomba kwa wadhamini kwa ajili ya kumlipa msanii kwenye ushirikishi wake wa Tamasha.

Mh habari inaendelea ndugu wasililizaji.........
 
Tuendelee kabla wenyewe hawajaamka. Mi nataka kujua hapo ktk vyombo vya serikali anahusika vipi? Tanesco na Polisi. Na vipi kuhusu wafanyakazi wa kiume ufisadi gani anafanya?
 
Hizi tabia za kipuuzi za watu kuiba, na then mkizulumiana ndo mnajifanya kuja hadharani ni za kupigwa vita. No wonder unashindwa kumwaga details kwa visingizio vya kitoto eti step by step ! Kama kweli weye ni msafi, basi sema tukupe mahali pa kupeleka hizo tuhuma zako, tena pa uhakika ambapo hakuna atakayekugusa wala kukutisha na zitafanyiwa kazi...! Ila kama na weye ulikuwa beneficiary wa huo ufisadi, umalaya n.k basi either funga bakuli au achana na hizi tabia za kitoto....
 
Ni kweli wasanii wa Bongo hawanufaiki na kazi zao,utaalamu wao na manufaa yao yako mikononi mwa wachache.Sikutegemea kumuona msanii kama Saida Kalol yule niliyemfahamu na nikahudhulia tamasha lake la kwanza uwanja wa Taifa nikakosa hata sehemu ya kuweka mguu kwa sababu ya wingi wa watu, leo hii hana kitu. Je ni nani aliyefaidika hapo?
 
Kwanza karibu kwenye jamvi.

Pili, sidhani kama ni sawia sisi kuanza kukuuliza ufafanuzi wa hizo tuhuma zako.

Unachotakiwa kufanya ni kwamba baada ya kuanisha vipengele vya ufisadi wa bw. Kusaga, unatakiwa sasa upige hatua moja mbele, utoe ufafanuzi wa hizo hoja zako ndipo sasa nasi tupate nafasi ya kuzichambua moja baada ya nyingine, vinginevyo utaonekana wewe ni hater tu ama la unaleta udaku tu hapa.
Pamoja Mkuu!!!!! ndugu yangu Afro, ili mradi unajua hayo yote weka wazi hapa jamvini.
 
Well . tupe . Kwenye TANESCO anafanya nini? Kama anaiba umeme tuambie maana hili lina maslahi kwa umma .
Tanesco:
Iwapo kuna tamasha lolote linaendelea na yeye hakubaliani nalo kwakuwa labda siku za mbeleni litakuwa na ushindani katika matamasha yake makubwa ya mwana,watu wake wakubwa wa kuvuruga mambo ni Tanesco.Kussaga ameshikiria karibia wakuu wote wa Tanesco kwenye wilaya zote za Dar es salaam. kwa mantiki hiyo basi,Taacha onyesho liandaliwe kwa kila kitu na kwa gharama kubwa na siku ya onyesho,eneo hilo la tamasha litakatwa umeme ili kulikwamisha tamasha hilo na nia kubwa ni kulivuruga tamasha hilo na kuwatisha wadhamini ili wasilidhamini tmasha hilo tena kwa siku za mbeleni kwakuwa tayari limeshaingia dosari. na umeme kwa kawaida ukatika pindi onyesho linapoanza na kama hamjajiandaa kikamilfu na mapema huo ndiyo mwisho wa onyesho hilo kwakuwa majenereta yote makubwa ya mjini anakuwa ameshayakodi ili mkose pa kukodi,na majenereta yanayoweza kuendesha onyesho kubwa kama hilo ni machache mjini na yanajulikana ni ya kina nani.
 
Ikiwa ni post yangu ya kwanza,ningependa kuwajulia hali wana JF na wadau wote wenye nia njema na nchi yetu Tanzania.

Leo nimeamua kuidadicate post yangu ya kwanza kwa wanaentertainment wote wa Tanzania ambao wengi wao ndoto zao zinaishia hewani kutokana na ufisadi unaofanywa na The Don of entertainment Tanzania Mr. Joseph kussaga kama anavyopenda kujiita The Don aka Mullah.

vifuatavyo ni vipengele ambavyo niko tayari kuvielezea kwa atakae taka kujua kiundani jinsi bwana huyu alivyoishikiria nchi kwenye nyanja ya burudani kwa maslahi yake binafsi.

  • Udhamini(sponsorships)
  • Bongo flava
  • Wafanyakazi wake(watangazaji na wengineo)
  • Polisi
  • Tanesco
  • kumbi za starehe
  • Umalaya
  • na chochote kuhusiana na burudani Tanzania.
Mimi ni mmojawapo wa watu wake wa karibu ambao katika wachache waliofanikiwa kujikwamua kutoka kwenye himaya yake na nimeamua kujitoa muhanga na kuweka hadharani chochote wana JF ambacho kinawakwaza kuhusiana na Ufisadi unaoendelea kwenye burudani Tanzania.

Kwakuwa ningependa kufafanua kimpangilio ndiyo maana nimeweka vipengele hivyo hapo juu ili niweze kuvifafanua inapobidi. Kutokana na ufisadi huu kuwa mkubwa na wenye network nyingi ningependa kufafanua kipengele kwa kipengele kama nilivyoviorodhesha hapo juu lakini iwapo ntatakiwa kufanya hivyo.

Nawakaribisha jamvini wana jamii ili tuweze kuutokomeza ufisadi huu kwa maslahi ya taifa.

Ahsanteni na karibuni.

Hakuna lolote hapa...full udaku(mmetofautiana kimaslahi nini?).....Home mods watafanya ze needfull
 
Nakuuliza kuhusu timing ya hizi allegation zako
kwa nini umezitoa leo ja sio january au december mwaka jana au mwaka juzi. Je umechukizwa zaidi baada ya kuona donge allokua apate Mr II limeenda kwa kina kusaga & companies. ?Au ushirika wako na kusaga umevunjila last week? Au ulikuwa bado unatafuta hoja za uhakilka ili taarifa zako zisiwe na FACT?

Na tutapataje uhakika kama hawa kina dada wao ndio hawajota rushwa ya mapenzi ili wapate kazi na si Ruge anayetaka rushwa mapenzi ili atoe kazi.
 
Ni kweli wasanii wa Bongo hawanufaiki na kazi zao,utaalamu wao na manufaa yao yako mikononi mwa wachache.Sikutegemea kumuona msanii kama Saida Kalol yule niliyemfahamu na nikahudhulia tamasha lake la kwanza uwanja wa Taifa nikakosa hata sehemu ya kuweka mguu kwa sababu ya wingi wa watu, leo hii hana kitu. Je ni nani aliyefaidika hapo?

Mkuu unatakiwa kujua jmabo moja kuwa kuwa na kipaji ni jambo moja, kukikuza kipaji ni jambo lingine, na kuuza kazi ya kipaji chako nalo ni suala lingine. Ili ufanikiwe unatakiwa kuchanganya haya yote.

sasa Saida alikuwa na kipaji lakini hakujua kama anacho hicho kipaji, pia hakujua atakikuzaje, alafu atakitumiaje kupata mafanikio, na hata afanye nini? hakujua hata kama kuna recording studio, sasa mtu kamuokota huko mashambani kamleta bongo kufika hapo kamwingiza studio kalipa gharama zote zinazohusiana na kazi yake kuwa hewani, kwa makubaliano (mfano sema) mwisho wa siku msanii utachukua 0.001% ya mapato yote na yeye akakubali shida ipo wapi???

Nimewaona wadogo zangu wengi kila siku wanatoroka darasani wanafanya mazoezi ya kukariri mashairi wenyewe wanaita Verse, lakini hana hata pesa ya kununulia hiyo pencil ya kuandikia hizo verse zake, nia yake kubwa ni kuona wimbo wake unapigwa kwenye kituo cha redio sasa mwisho wa siku wajanja akina Ruge wakitokea wakamwambia dogo tutakutoa utasikia muziki wako Clouds FM kwanini asiingie kichwa kichwa, akiliwa kichwa sio kosa la promoter ni kosa lake yeye mwenyewe kutojipanga kisawa sawa.

sawa na hawa wasanii wa filamu bongo nao michosho kila mwezi wewe unatoka na filamu mpya, Kanumba miaka 3 ya uigizaji ana movie zaidi ya 40 mara nne ya movie za Denzel Washngton ambaye masiha yake yote ni movie na tayari ameshakuwa director wa movie mmmmmh hawa bwana kama hawapo tayari kutumia ushauri wa watu wataliwa mpaka t.
 
Tanesco:
Iwapo kuna tamasha lolote linaendelea na yeye hakubaliani nalo kwakuwa labda siku za mbeleni litakuwa na ushindani katika matamasha yake makubwa ya mwana,watu wake wakubwa wa kuvuruga mambo ni Tanesco.Kussaga ameshikiria karibia wakuu wote wa Tanesco kwenye wilaya zote za Dar es salaam. kwa mantiki hiyo basi,Taacha onyesho liandaliwe kwa kila kitu na kwa gharama kubwa na siku ya onyesho,eneo hilo la tamasha litakatwa umeme ili kulikwamisha tamasha hilo na nia kubwa ni kulivuruga tamasha hilo na kuwatisha wadhamini ili wasilidhamini tmasha hilo tena kwa siku za mbeleni kwakuwa tayari limeshaingia dosari. na umeme kwa kawaida ukatika pindi onyesho linapoanza na kama hamjajiandaa kikamilfu na mapema huo ndiyo mwisho wa onyesho hilo kwakuwa majenereta yote makubwa ya mjini anakuwa ameshayakodi ili mkose pa kukodi,na majenereta yanayoweza kuendesha onyesho kubwa kama hilo ni machache mjini na yanajulikana ni ya kina nani.

Tupe mfano wa matamasha aliyohujumu kwa mtindo huu
 
Jamani vipi? inaonekana Kusaga mnaheshimu sssana kiasi kwa mba hamtaki mtujue hata the other side yake!!
afro, endelea kumwaga vitu......ongea tuyajue.
 
Jamani vipi? inaonekana Kusaga mnaheshimu sssana kiasi kwa mba hamtaki mtujue hata the other side yake!!
afro, endelea kumwaga vitu......ongea tuyajue.
hajaleta kwa mtiririko mzuri kwa hiyo it is assumed he has nothingto Tell
 
Najua mwanzoni itakuwa ngumu kueleweka kwakuwa maswali mengi yatajitokeza kutokana na thread hii,Ila ningependa kufafanua zaidi kwamba mimi sikuwa mshiriki wa Kussaga bali nilikuwa muajiliwa niliye kifungoni kama wasanii wanavyowekwa kifungoni lakini imefikia wakati nimeshindwa...mimi fani yangu kubwa ni mwana burudani,nilijitoa Clouds FM miezi michache iliyopita na kujaribu kuendeleza fani yangu kimwenyewe mwenyewe lakini mambo yanayonikuta ni kwamba nimefungiwa njia zote na huyu jamaa na hakuna njia yoyote ya mimi kujiendesha binafsi kwakuwa nyanja nyingi zinazohusiana na Entertainments zimeshabanwa.Labda nibadilishe fani au nikubali kuendeshwa na huyu jamaa kama anavyotaka yeye.

wengi watafikiri ni udaku au majungu au Chuki lakini si hivyo kabisa.kuna mambo mengi sana ya kifisadi yanaendelea katika fani hii ambayo kwa mimi binafsi ninauhakika tunaweza kuyakemea kwa maslahi ya jamii. mi nafikiri tuwe wavumilivu na tuijadili hoja hii kiupole zaidi.
 
Ni kweli wasanii wa Bongo hawanufaiki na kazi zao,utaalamu wao na manufaa yao yako mikononi mwa wachache.Sikutegemea kumuona msanii kama Saida Kalol yule niliyemfahamu na nikahudhulia tamasha lake la kwanza uwanja wa Taifa nikakosa hata sehemu ya kuweka mguu kwa sababu ya wingi wa watu, leo hii hana kitu. Je ni nani aliyefaidika hapo?
Suala la Saida karori kupotea ni kutokana na kutokuwa na maelewano baina ya meneja wa Saida na CLOUDS FM.

Kipaji cha Saida karori kiligunduliwa na Mr Mutta ambaye ni mmiliki wa studio za FM Studios. Baada ya kugundua kipaji hicho Mutta alimuingiza studio msanii huyo na kusaini nae mkataba kama meneja wake. lakini baada ya msanii huyo kuchanua ndiyo upande wa CLOUDS wakaanza kumtolea macho na kumtaka dada huyo abadili mawazo na kusaini upya na Clouds kitu ambacho muta alikipinga sana na bahati nzuri alikuwa na documents kuhusiana na msanii huyo. Clouds baada ya kushindwa kumchukua msanii huyo ikaamua kumuua kisanii ikiwa ni pamoja na kutopiga miziki yake na kuwabana sponsors kutodhamini onyesho lolote litakalomuhusu msanii huyo.Na mwisho wake hakuna aliyefaidika..Si msanii,si Meneja wake wala si CLOUDS FM. SAD
 
Najua mwanzoni itakuwa ngumu kueleweka kwakuwa maswali mengi yatajitokeza kutokana na thread hii,Ila ningependa kufafanua zaidi kwamba mimi sikuwa mshiriki wa Kussaga bali nilikuwa muajiliwa niliye kifungoni kama wasanii wanavyowekwa kifungoni lakini imefikia wakati nimeshindwa...mimi fani yangu kubwa ni mwana burudani,nilijitoa Clouds FM miezi michache iliyopita na kujaribu kuendeleza fani yangu kimwenyewe mwenyewe lakini mambo yanayonikuta ni kwamba nimefungiwa njia zote na huyu jamaa na hakuna njia yoyote ya mimi kujiendesha binafsi kwakuwa nyanja nyingi zinazohusiana na Entertainments zimeshabanwa.Labda nibadilishe fani au nikubali kuendeshwa na huyu jamaa kama anavyotaka yeye.

wengi watafikiri ni udaku au majungu au Chuki lakini si hivyo kabisa.kuna mambo mengi sana ya kifisadi yanaendelea katika fani hii ambayo kwa mimi binafsi ninauhakika tunaweza kuyakemea kwa maslahi ya jamii. mi nafikiri tuwe wavumilivu na tuijadili hoja hii kiupole zaidi.

Dah pole sana ndugu kwa kufungiwa njia, usijali kwa hilo Mungu atakufungulia kwa njia nyingine ila usijaibu kulipiza kisasi au kutaka kushindana na mtu kama huyo maana unaweza kujikuta matatani bure, kuwa mwangalifu na jipange upya kamwe hawezi kuziba milango yote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom