Johnson Mashaka na mbio za Ubunge Ukonga

ii) Kupitia CCM. Sign of cowardness. Mapinduzi na mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa kupitia CCM. Atakachofanikiwa sana sana ni kujifunza kutetea ufisadi.

Anyway kama anataka uwaziri huko CCM ndiko kunakomfaa. Lakini kama kweli ana nia ya kushiriki kuleta mabadiliko aende upinzani, aache longolongo na woga.

Kitila
Upinzani gani wewe unataka kutuambia?Ujinga gani wewe unataka kutuletea hapa,Miaafrika bana tayari limesahau yaliyotoke upinzani.Labda Mashaka ni Mchagga....kwi..kwiii
 
Wrong and very bad start:

i) Anatumia hela katika kujaribu kupata huo ubunge. Huo nao ni ufisadi na hadaa, maana anatumia umaskini na shida za wana Ukonga kujipatia ubunge. Mara baada ya uchaguzi atafanya kazi ya kutafuta namna ya kurudisha hizo sh 350,000m. Ameingia kwa gia ileile aliyoingia nayo Masha huko Nyamagana na tukamshangilia sana, tena hapahapa JF, lakini leo sote tunajua anachofanya Masha!

ii) Kupitia CCM. Sign of cowardness. Mapinduzi na mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa kupitia CCM. Atakachofanikiwa sana sana ni kujifunza kutetea ufisadi.

Anyway kama anataka uwaziri huko CCM ndiko kunakomfaa. Lakini kama kweli ana nia ya kushiriki kuleta mabadiliko aende upinzani, aache longolongo na woga.

Baba Kitila,

Sasa waleta mabadiliko waende wapi? Kama ni CHADEMA ndiko ambako hawataki vijana na maamuzi yote yanafanywa na mwasisi.

Kumewashinda akina Wangwe na Zitto huko kweli kutamfaa kijana wa bara ambaye hajaoa uchagani?

Labda mwenzetu umeoa huko ila kama sivyo, wewe subiri tu kusaidia kuingiza kura kwenye chama ili wenzako wafaidi.

CCM ni bomu lakini angalau ni jumba la kila mtu na tutabanana humo humo kuliki CHADEMA ya wenye nayo. Ukiwapinga kidogo tu wanakuita fisadi.

Hivi kati ya Zitto na Mbowe, ni nani fisadi kuliko mwenzake?

Huyo Zitto mwenyewe CHADEMA watamchanganya kwa matusi na kejeli mpaka arudi CCM. Wanamwita fisadi huku wamempa kuwa naibu katibu.

Acha vijembe baba Kitila. Haya mavyama yenu yote yanafanana na watu ni wale wale. Wote hamtujali sisi maskini na mnatutumia tu.
 
Halafu na yeye kaingia na mijipesa yote hiyo (kama ni kweli) haitakuwa ridhaa ya wananchi bali rushwa (HONGO) itamfanya achaguliwe yaanii MULE MULE KUKUZA UFISADI TU, hakuna haja hata ya kumshangilia kiivyo
 
Huyu Nape wako hafui dafu kwa Myika huko Ubungo afadhali angekwenda Temeke anaweza kuambulia!! Ubungo wamejaa wasomi wasioweza kurubuniwa na propaganda za CCM!!Kama Nape haamini ajaribu aone atakavyogaragazwa.
 
Wrong and very bad start:

i) Anatumia hela katika kujaribu kupata huo ubunge. Huo nao ni ufisadi na hadaa, maana anatumia umaskini na shida za wana Ukonga kujipatia ubunge. Mara baada ya uchaguzi atafanya kazi ya kutafuta namna ya kurudisha hizo sh 350,000m. Ameingia kwa gia ileile aliyoingia nayo Masha huko Nyamagana na tukamshangilia sana, tena hapahapa JF, lakini leo sote tunajua anachofanya Masha!

ii) Kupitia CCM. Sign of cowardness. Mapinduzi na mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa kupitia CCM. Atakachofanikiwa sana sana ni kujifunza kutetea ufisadi.

Anyway kama anataka uwaziri huko CCM ndiko kunakomfaa. Lakini kama kweli ana nia ya kushiriki kuleta mabadiliko aende upinzani, aache longolongo na woga.

Waziri kijana, mchapa kazi sana....lol....
 
John Mashaka akishatumia hizo $350,000 je atazilipaje au amezitoa wapi kiasi kwamba ameamua kuzitumia? Je chanzo chake cha mapato ni nini haswa?

Kwanini asitumie nguvu ya hoja zaidi kuliko pesa? Hii ni dalili ya kuendeleza umasikini kwa jamii kwa kuwekeza hela nyingi kwenye siasa kuliko kwenye maendeleo halisi ya kumkwamua mtu kimaisha.

Mimi sikufurahia hii hatua yake ya kupita na kugawia watu unga, juice, biscuti kutoka marekani etc, kwanini asitoe scholarship za watu kusoma shule? au kulipia watu ada walioshindwa kusoma chuo?

Watu kama hawa ndio wanaozidi kuifanya jamii kuwa masikini zaidi kwa kufanya kuwa tegemezi zaidi kuliko kuisaidia kujikwamua ili waondokane na umasikini walionao...!
 
Nadhani mtoa maada hapa jukwani unaweza ukawa unampigia debe au kumtoa kabisa huyu kijana ktk harati zake.Kama ni kweli anategemea kutumia kiasi chote hicho inamaana yeye anategemea baada ya ku-ukwa ubunge apate zaidi ya hizo ndo mambo mengine yaendelee.Naoana kama hatakuwa na mda wa kuwatumikia wananchi zaidi atakuwa anatafuta njia za kifisadi kurudisha hela aliyotumia kwenye kampeni.
Pia chama anachotaka kupitia kinaweza kuwa kikwazo kwake maana hata kama atakuwa na mawazo mazuri hataweza kuyatoa ataogopa kunyang'anywa uanachama kwenye NEC.
 
Mkandara,

Usijiangushe kaka yangu, na wewe unakaa huko kwa wachovu Ukonga?

Mizee yote hoi hoi ile ya huku kwetu Kyela inakaa hayo maeneo ukianzia akina Mwakipesile, Mwakalukwa mpaka yule aliyekuwa mkuu wa magerza.

Sikushangaa nilipoona Malafyale na ES nao ni mwendelezo huo huo wa hoi hoi wa Ukonga wakiongozwa na mbunge wao hoi Mahanga.

Nakushauri hama huko, usije ukaishia kama yule katibu mkuu wa rais hata jina nimesahau.

Watu wa UKONGA mko hoi sana, afadhali hata sisi wa huku Kyela.

Labda Mashaka awachangamshe kidogo.

- Mkuu kila unapofungua kinywa unazidi kuonyesha uwezo wako wa kufikiri ulipoanzia na kuishia, kila siku unalia lia hapa kwamba Kyela unaibiwa na kuongozwa na mafisadi, hivi kweli unaweza kulinganisha maendeleo ya jimbo la Ukonga na Kyela?

- Mkuu jimbo la Ukonga lina kata nyingi zikiwemo za Kinyerezi, Kipunguni, Kitunda, Ukonga Magereza, Majumba Sita, Sitaki Shari, Segerea, Airwing na zinginezo, sasa hebu nitajie kata moja tu kati ya hizi unayoweza kulinganisha na hata jimbo zima la Kyela kimaendeleo?

- Ndio kwanza tumefungua bara bara mpya ya lami, kutoka getini Airwing yaani njia panda ya Airport mpaka gerezani Segerea kufikia Tabata unaunganisha mpaka Kimara. Mahanga sio siri ni kiongozi mchovu, lakini Ukonga sio Mahanga ambaye amekaa bungeni kwa miaka minne tu so far, hili jimbo ni bomba kabla hata yeye kuhamia Ukonga.

- Eti mkuu jimbo lenye vitega uchumi na kutoa ajira kwa wananchi jimboni kama Julius Nyerere International Airport, FFU HQ, JWTZ-Airwing HQ, JWTZ-Mizinga Squad, Gereza Kuu la Ukonga, Gereza Kuu la Segerea, Viwanda vya nguo Kiltex na Sungura tex, Kiwanda maalum cha kutotota vifaranga vya kuku, Segerea Catholic Seminary, unasema unaweza kulinganisha hili jimbo na Kyela? Hivi unajua hili jimbo lina secondary ngapi mkuu? Hebu nitajie jimbo moja tu Tanzania nzima linaloweza kulifikia jimbo hili la Ukonga kwa maendeleo?

- Na pia jimbo hili tunajivunia sana kwa kuwa na kata ninayotoka ya Kinyerezi/Sitakishari ambayo ni a home for national celebrities kama the sitting national leaders Waziri Wasirra, Mkuu wa Itifaki Balozi Itatiro, RC wa sasa Mbeya Mwakipesile, Mbunge wa Kawe Rita Mlaki, Managing Director Azania Bank Charles, Managing Director Wananchi Bank Mzee Mkwawa, pia tuna wastaafu wa taifa kama familia ya waziri wa zamani wa afya Mzee Sterling, Mzee Apiyo, familia ya marehemu Waziri Itatiro, familia ya marehemu makamu wa mwenyekiti wa kwanza wa Chadema Mzee Ngwilulupi, familia ya Balozi wetu wa zamani Nigeria Marehemu Mwasakafyuka, Wakuu watatu wa zamani wa Magereza Mzee Mwanguku, Mzee Mwaijande na Mzee Mwaipopo, familia ya mkuu wa polisi zamani marehemu Mzee Liani, Pia tuna wafanya biashara maarufu kama kina Mujuluzi, majority owner wa Imma, Dr. Mwaijande owner wa pharmacy maarufu pale Muhimbili hospital, kampuni kubwa ya mabasi na malori ya Mahende, Club maarufu sana Dar ya Hill-teck, pia ni a home for a former Simba player/national team Idd Pazi "Father" na pia ni a home for mimi mwenyewe Mukulu Field Marshall Es, yaani wazee wa sauti ya umeme! na Mkulu Mashaka John.

- Engineeer, hili jimbo haliwezi kuwa chovu kama lako huko Kyela not even close mkuu, msiwe mnakurupuka kurupuka jamani ulizeni kwanza, infact hili jimbo la Ukonga linaweza kuwa numero uno kwa maendeleo bongo nzima, sasa hivi kiwanja cha kujenga nyumba cha eka moja tu Ukonga kitakugharimu atleast Shillingi Millioni 20-30, sasa Engineer unasema nikitaka kununua kiwanja kama hicho Kyela kweli bei itakuwa sawa na hii ya Ukonga? Bwa! ha! ha! mkuu karibu sana Ukonga, usingoje ya kusimuliwa mkuu!

Wakuu Malafyale, Sinkala na Mkandara huuu ni wakati wa kuhamishia hii elimu tunayoipata hapa JF, katika jimbo letu badala ya kurushiana maneno machafu yasiyo na mshiko kwa masilahi ya taifa kama hao wa Kyela, na ni lazima tujihusishe sana na hii process ya kutafuta mbunge anayefaa kwa jimbo letu yaani wa kuendeleza aliyoyakuta, mimi toka jana nilipoiona hii habari ya Mashaka, nimekua nikiwasiliana na wazee wa jimbo kujua kinachoendelea na soon tutaweka msimamo hapa. Mkuu Engineer karibu sana jimboni kwetu ujifunze elimu ya maendeleo ya jimbo mkuu.

Respect.

Field Marshall Es!
 
Bahati nzuri kwa Dar yalipo makazi yangu ni Kipunguni-kitunda,na sijaona hata siku moja John Mashaka akishirikiana na sisi kweye suala la maendeleo;kwa ufupi kama kweli anakuja kugombea Ukonga na aje na "tutamnyoa" na hizo" hela zake!Kama suala ni mgombea kiana wapo wengi tu Ukonga na sio lzm awe John Mashaka ambaye umaarufu wake kwa wana Ukonga tunausikia tu kupitia blog ya Michuzi inayomtangaza kweli kweli!

Pia kama kweli ataleta Wamarekani kuja kumfanyia kampeni hapo atakuwa anavunja katiba,sheria mama za uchaguzi wa TZ zinakataza kabisa kwa mtu asiye raia wa tz kuhusika kwa lolote lile ktk uchaguzi wetu kama sisi ambavyo hatuingilii chaguzi za nchi zingine!

"Mwisho ni hii habari ya dola 350,000 na gari hizi zake za kifahari",Kwa maisha ya USA kujikusanya hadi kufikisha hela hizo na kununua magari hayo ni ngumu;anyway acha niamini kama anavyo vitu hivyo,lkn je vitamsadia kupata Ubunge wa Ukonga bila mtaji wa watu?

Kwa mtu makini au mwanasiasa makini hawezi kutumia kiasi hicho kwa ajiri ya campaign tuu. Then unataka kuwalinganisha hao vijana na Kabwe Zitto! Ni vitu viwili tofauti, angalau tumeziona juhudi za Nape katika kupinga ufisadi, lakini January! atawezaje wakati yuko kwenye system hiyohiyo
 
Na msinisahau Mkandara nipo Matembele, Ukonga..

Yaani hii mada ya FISADI imeonyesha ni jinsi gani wana CCM wa Ukongo walivyo wachovu na waoga wasiokuwa na jipya kwetu!

Kama ni kweli bwn. Mashaka. J anamwagwa mihela mnafikiri hizi pumba za kusema eti tutaenda kuwaelimisha wana-Ukonga zitafanikiwa? kumbukeni ni chama chenu CCM ndicho kilichowazoesha wa-Tanzania kupokea fedha toka kwa wagombeA sas mnalialia nini?

Je mnataka kulihakikishia hili jamvi tukufu kama naye huyo mchovu wenu dakitari feki Mahanga hatamwaga mihela??? mi nafkiri njia pekee ya nyie kumuokoa Mahanga wenu ni kumchangia mihela ili muendeleze libeneke lenu la takrima kwa sababu mmeshawazoesha watanzania kupokea fedha zaidi ya hapo mkono mtupu haulambwi!!!! mwenyenazo ndio atachaguliwa!

Na mwisho kumbukeni kwamba ushindani wa kweli kwa huyo mgombea wenu bwn.Mashaka. J utatoka kwa vyama vya upinzani nyie mpitisheni tu halafu mje muone jinsi atakavyokuja kaangwa sambusa kwa mafuta ya ufisadi wa CCM!

Amani iwe kwenu!

 
Yaani hii mada ya FISADI imeonyesha ni jinsi gani wana CCM wa Ukongo walivyo wachovu na waoga wasiokuwa na jipya kwetu!

Kama ni kweli bwn. Mashaka. J anamwagwa mihela mnafikiri hizi pumba za kusema eti tutaenda kuwaelimisha wana-Ukonga zitafanikiwa? kumbukeni ni chama chenu CCM ndicho kilichowazoesha wa-Tanzania kupokea fedha toka kwa wagombeA sas mnalialia nini?

Je mnataka kulihakikishia hili jamvi tukufu kama naye huyo mchovu wenu dakitari feki Mahanga hatamwaga mihela??? mi nafkiri njia pekee ya nyie kumuokoa Mahanga wenu ni kumchangia mihela ili muendeleze libeneke lenu la takrima kwa sababu mmeshawazoesha watanzania kupokea fedha zaidi ya hapo mkono mtupu haulambwi!!!! mwenyenazo ndio atachaguliwa!

Na mwisho kumbukeni kwamba ushindani wa kweli kwa huyo mgombea wenu bwn.Mashaka. J utatoka kwa vyama vya upinzani nyie mpitisheni tu halafu mje muone jinsi atakavyokuja kaangwa sambusa kwa mafuta ya ufisadi wa CCM!

Amani iwe kwenu!

- Mkuu Great Thinker hii habari ya Mashaka na Ukonga, yaani tayari kumbe umeithibitisha kwamba ni ya kweli? Sisi wakazi wa jimbo mbona bado kuithibitisha?

- A great thinker hawezi rusha maneno mazito kama yako ya kuwatukana wananchi wote wa jimbo la Ukonga, unless ana uthibitisho wa facts kwamba kwanza habari za Mashaka ni za kweli, na kwamba wana-CCM wote Ukonga ni wala rushwa,

- vipi mkuu great thinker unaweza kutuwekea huo ushahidi hapa kabla hatujaendelea na hii mada? Si unajua ile sheria ya no research no right to speak! au?

Respect.

FMEs!
 
Nape naamini atashinda kwa ushindi wa mezani kama kawaida yao CCM.

- Nape anaweza kumhimili Mnyika, one on one I mean utakuwa uchaguzi wa mwaka huo, hata Muungwana anakubaliana na mimi kwamba only Nape ndiye anaweza kumsimamisha Mnyika.

- I can't wait!

FMEs!
 
- Nape anaweza kumhimili Mnyika, one on one I mean utakuwa uchaguzi wa mwaka huo, hata Muungwana anakubaliana na mimi kwamba only Nape ndiye anaweza kumsimamisha Mnyika.

- I can't wait!

FMEs!

Kaka Nape kamwe hawezi kupambana na MNYIKA one on one. Mnyika he is detailed informed kuliko Nape ambaye ni mzuri wa vibwagizo lakini vinakosa mishiko/nyama. Mnyika ni mzuri sana on details ba anajua kuzipanga na kuzitumia kuinua emotions.

Hata hivyo Mnyika atakuwa na kazi kubwa this time kuliko 2005 kwa kuwa hana advantage ya ujana, hana party network, hawezi siasa hovyohovyo kama ambavyo Nape ameweza kuonyesha hivi karibuni katika KAMPENI YAO YA VICOBA na zaidi Mnyika hana DOLA.

Kitakachomsaida MNYIKA ni siasa za makundi CCM zenye chimbuko lake tangia enzi za NAPE-MALECELA Vs NCHIMBI-JK....wale jamaa hawajamsahau bado na hili la VITA YA UFISADI (sio vita dhidi ya ufisadi) ndio line nzuri ya MNYIKA....

omarilyas
 
Je Mnafahamu ya Kwamba John Mashaka anasukumwa na Mafisadi?? Hbari ndo hiyo......

Soma Hotuba yake



HOTUBA YA JOHN MASHAKA KATIKA
VIWANJA VYA BIAFRA, KINONDONI

Mheshimiwa Profesa David Mwakyusa, Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, wadhamini wetu kampuni ya zain, clouds FM na Business Times, wageni waalikwa na watanzania wenzangu.

shukrani za dhati kwa kuukubali huu mwaliko, na kujumika nasi wa siku ya leo kujikumbushia maswala muhimu kuhusu taifa letu hasa maswaa ya haki na usawa. Huu ni uzalendo wa aina yake, ni uzalendo unaotukumbushia uhuru wetu wa mwaka 1961, nchi hii iliposaini hati ya makabidhiano ya uhuru,

Hati ya mwaka 61 iliikabidhi nchi yetu haki yake ya msingi, haki ya maamuzi yaliyo mhakikishia kila raia maisha bora, na usawa. Hati hiyo ya mwaka 1961, ilitoa matumaini kwa kila mmoja. Raia wa Tanzania, walihaidiwa maendeleo makubwa.Watanzana hawakuahidiwa haya yanayojitokeza kwa sasa ; hawakuhaidiwa ahadi zisizotekelezeka, Walipewa ahadi za dhati za kukabiliana na maradhi, ahadi za kuondokana na umasikini na ujinga. Watanzania walipewa ahadi za haki, bila kujali matabaka, walihaidiwa usalama kwa raia wote.

Ahadi za mwaka 1961 hazikuwa za kuleta ufisadi kama huu tunao ushuhudia sasa. Hati ya Uhuru ilikuwa ni ya manufaa kwa raia wote. Kwa hakika katika miaka 48 ya uhuru wetu, yapo mambo kadhaa ya kujivunia.


Kuna mabadiliko makubwa hasa katika jiji la Dar es Salaam na hata kwingineko Ambako Kuna majengo marefu, mazuri ya kisasa, yanayoelekea mawinguni. Miaka 48 imeleta mabadiliko ya kijamii, kuna matabaka ya wasomi wenye maisha ya juu. Kuna makundi ya watawala na wenye mamlaka; Kuna kundi la matajiri wanaoshi katika sayari tofauti na watanzania walio wengi.

Watanzania wenzangu, wakati wapo wenye maisha mazuri, wanaoishi katika raha na utukufu, wapo pia wengi ambao wana maisha ya dhiki, wapo mamillioni wanaoshi katika ukiwa. Wapo wengi wanaoishi kwa kubahatisha na kwa kukata tamaa; wale ambao hawaoni faida waliyoitegemea kutokana na kupatikana kwa uhuru wao. Wapo maalbino wanaoishi kwa ukiwa na wasiwasi mkubwa.

Umbali mfupi tu kutoka hapa tulipo wapo wenzetu ambao wanaishi kwa hofu; wanaume kwa wanawake walio na wasiwasi, siyo tu juu ya maisha yao wenyewe, bali maisha ya umbele ya kiafya, na kielimu kwa watoto wao.Hawa ni raia wenye hofu kuhusu usalama wao. Ni raia wenye hofu jinsi watakavyowalisha watoto wao.Ni raia wenye wasiwasi ni jinsi gani watawasomesha watoto wao, siyo katika shule za ng'ambo bali katika shule za humu nchini. Hawa ni raia wenye hofu ya kupata hata mmlo mmoja kwa familia zao nahuu ndio ukweli wa mambo; Ni ukweli unaouma.

Ukweli wa mambo wenye machungu,haupo mbali nasi, ukweli huu upo manzese, upo kigogo na kule Temeke. Hali mbaya zaidi ya ukweli huu upo pale msimbazi center ambapo vitoto vichanga vya miezi mitatu vinaishi kwa uwezo wa mwenyezi Mungu ili hali nchi yao inayo uwezo wa kuwapa maisha yenye uhakika. Ukweli unaosononesha tunao hapa kati yetu, ambapo maelfu ya vijana hawana ajira, ni wachovu katika lindi la ufukara. Ukweli huu unaoumiza tunauona kwa vijana wetu ambao, licha ya kuwa wamesoma vya kutosha, wanabakia wakichuuza maji ya kunywa ili kujikidhi kimaisha.

Wengine wanaamua kuchukua silaha na kufikia hatua ya kuyachukua maisha ya wengine ili kujipatia riziki. Huu dio ukweli wa mambo; ni ukweli unaouma.

Natumia nafasi hii kuwasihi wale wote wanaochota raslimali za inchi hii; Wale wote ambao wanahamisha mamilioni ya pesa za walipa kodi na kuyapeleka katika akaunti nje ya nchi, Nawasihi wale wote wenye roho za kifisadi kufikiria mara mbili juu ya maadili na vitendo vyao.

Nawasihi hawa waliopewa dhamani ya kuilinda hii nchi kuvitembelea vyuo vyetu, na tasisi nyingine za elimu ili kuangalia hali halisi ya mahitaji katika taasisi hizo. Nawasihi viongozi wetu kwenda katika vituo vya mabasi, na masokoni na kuwaona vijana na watoto wadogo waliolemewa na ufukara, wanaolala kwenye mabaraza ya majumba na kwenye magenge kwa sababu hawana makazi. Nawasihi viongozi wetu kutega masikio yao ili kuwasikia, vijana wenye majonzi makubwa , vijana wanozishuhudia ndoto zao za kielimu zikitokomea kutokana na ufukara mkubwa walionao wazazi wao.

Siku ya leo ndugu zangu, tunawaomba viongozi wetu wavisikie sauti za ndugu zetu wanaowindwa kutokana na uumbaji wa Mwenyezi mungu. Tunawaomba wazisikie sauti za ndugu zetu maalbino wanaoishi kwa uwoga na ukiwa . Tunaomba walindwe, na kupewa haki zao za kimsingi, na za Usalama. Hii siyo tu kwao maalbino, bali kwao watanzania wote wanaotikiswa na wimbi la ujambazi. Hii siyo hati nchi yetu ilisaini kwa ajili ya raia wake, Hii ni hundi batili MAFISADI wa kimaadili wanawalazimisha raia wema kuvichukua.

Tunawasihi viongozi wetu waondoke nje ya ofisi zao ili watafute muhafaka kwa kushirikiana na wananchi wengine juu ya ulinzi wa watoto albino wasio na hatia. Ninawasihi, msikie kilio cha yule Albino, binti wa miaka 10 ambaye hawezi kukilalia kitanda kimoja kila siku kwa sababu tu anawindwa na watu wenye tamaa na imani potofu. Huu ndiyo ukweli wa mambo, ukweli wa miaka 48 ya uhuru wetu!

Ni ukweli unaouma !

"Miezi michache iliyopita nilighafirika kwamba kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa Kimarekani niliyeongea naye, aliweza kuikumbuka Tanzania kwa mauaji ya albino badala ya mambo mengine mengi mazuri tu yanayoihusu Tanzania".Jambo hili ni la kifedheha! Huu ni umaskini wa kifikra na UFISADI wa kimaadili ambao umetukumba sisi watanzania. Kumuwinda binadamu kutokana na umbile lake siyo utanzania, huu ni ushetani.

Tusiitegemee serikali kuwa na miujiza ya kusuluhisha kila tatizo letu la kijamii na kiusalama. Tatizo hili lipo mikononi mwetu. Sisi raia ndio wenye nguvu na uwezo wa kutokomeza haya mauaji ya kinyama. ni lazima tushirikiane ili kuzuia jambo hili la kiovu. Watanzania wenzangu, wakati wapo wenzetu wanaume kwa wanawake chini ya bahari, angani na kwingineko wakifanya utafiti na shughuli zenye hatari kubwa kwa manufaa yetu, nchini kwetu, wengine wanatafiti namna ya kuwaua maalbino wasiokuwa na hatia. Tuwalindeni maalbino, tuwasaidieni tunapoweza.

Ndugu zangu, tusipojitizama vizuri, basi tunakokwenda ni giza kubwa na majonzi yasiyokuwa na kipimo kwa sababu binadamu ambaye hawezi kuyathamini maisha hana zaidi ya kuthamini.

Tumeumbwa tulindane, si kuwindana.
Tumeumbwa kuwa watumishi, siyo watumikiwa,
Tumeumbwa kuwatendea haki wanyonge, siyo kuwanyanyasa,
Tumeumbwa kujitolea kwa hali na mali kwa manufaa ya wengine.

Hiyo ndiyo maana halisi ya maadili, Hiyo ndiyo maana ya uongozi!
Mwanafalsafa wa Kimarekani , Edmund Burk, alipata kusema kwamba, " tofauti kubwa kati ya kiongozi wa dhati na yule ajifanyaye kuwa kiongozi ni kwamba; kiongozi wa dhati uangalia mbele, wakati yule bandia uangalia ya leo. Kiongozi bandia anaishi kwa ajili ya leo na anatenda udanganyifu, wakati mwenzake anavumilia machungu ili kuyalinda madili na kutizama maisha ya baadae".

Viongozi wanaoipenda hii nchi, badala ya kutafuta utajiri wa kitambo, tunawaomba muangalie ni wapi tunaelekea. Tunawaomba mtafakari mustakabali wa nchi na maisha ya mbeleni ya vijukuu vyenu ambavyo havitahitaji mabillioni ya fedha ya wizi iliyolimbikizwa nchi za nje. Bali mazingira mazuri ya kuishi yenye amani .

Ndugu zangu, muda hauna uhadilifu wala subira. Muda hauwezi kubadilisha au kutatua matatizo yetu, Muda hauwezi kuponya vindonda vilivyosababishwa na umasikini. Muda hauwezi kuyarudisha maisha yaliyopotezwa kutokana na tamaa na ulafi wetu. Muda haupo upande wetu, wala maneno matupu hayawezi kuponya maumivu.Muda hauwezi kutuondoa katika masumbuko yetu, bali unaweza kutuacha ili tuendelee kuumia.

Wakati umefika tujitoe mhanga ili kuleta mabadiliko na kuondokana na maumivu yanayotukabili. Wapo wengi ambao wamekuwa wakihoji haya ninayoyafanya katika jamii, wengine wamekuwa wakidhania kwamba nina malengo ya kisiasa !

Ninachoweza kusema ni kwamba mtu yeyote mwenye hutu ambaye analiona wingu la umasikini uliotanda katika taifa letu, anayo jukumu la kimaadili kutoa mchango wake ili kuondoa kukata tamaa kunakowakabili mamilioni ya wanachi wetu, dhamira hii ipo juu ya dhamira nyepesi za kisiasa.

Ninalilipa deni langu kwa jamii yangu. Nalipa fadhila kwa mwenyezi Mungu. Haraka iliyopo katika hitaji la kuwasaidia ndugu zetu wenye matatizo, ni ya kasi zaidi kuliko haraka ya kukimbilia madaraka ya kisiasa. Hitaji la kumsaidia mtoto mwenye kulala na njaa ni kubwa kuliko tamaa za madaraka ya kawaida ya kisiasa.

Kimsingi huo ndio mvuto mkubwa ambao umekuwa ukiusumbua nafsi yangu kwa muda mrefu. Ninachokifanya ni sehemu tu ya utashi wa kiroho ambao umenifunulia wajibu wangu, na jukumu langu kama binadamu mwingine anayetambua kati ya wema na uovu. Huu ni utashi ulionipa changamoto ya kujitazama upya katika taswira ya maadili. Ni utashi unaotusihi wote kujitolea mhanga kwa ajili ya amani katika taifa letu.

Kila mmoja ana ndoto ya kuishi maisha yenye furaha. Wote mliopo hapa mmekuja kwa sababu mnaamini kwamba tunalindwa na bendera moja, na kutumikiwa na rais mmoja. Hivyo, nawasihi mrudi majumbani kwenu na ujumbe mmoja kwamba, maisha yenye matumaini ni muhimu kuliko maisha ya kukata tamaa.

Ni lazima wote tufahamu kwamba upendo ni muhimu kuliko chuki. Lazima mtambue kwamba ushirikiano ni muhimu kuliko utengano. Hizi ni tunu ambazo tunatakiwa kuzilinda; Ni lazima tuwe sehemu ya mabadiliko kueleka katika maendeleo chanya.

Kufika kwenu hapa leo imekuwa kama chanzo cha uharakati wa watanzania, uharakati wa kijamii ya kuwalinda wenye ulemeavu, wenye ukoma, na wasioona. Ni uharakati wa kuwavalisha wanaotembea uchi. Ni uharakati wa kuwalisha wanaoshinda njaa. Ni uharakati wa kuwalinda maalbino wanaoishi kwa wasiwasi na ukiwa

Ni uharakati na maendeleo ambayo yamevuka mipaka ya siasa, dini, hata asili za watu. Ni maendelao yaliyovuka ubaguzi wa rangi, matabaka, na hata kasumba. Ni maendeleo yanayowakutanisha Watanzania wote. Huu ni uharakati na mchakato wa masikini na matajiri. Mchakato wa wenye madaraka na wanyonge, Ni mchakato kuhakikisha kwamba MAFISADI na masikini wanapewa haki sawa mbele ya sheria.

Ni mchakato na uharakati wa kuleta upendo kwa kila mwanadamu. Ni mchakatona ambao umedhamiria kurudisha yale matumaini ambayo watu walikuwa nayo mwaka 1961 wakati nchi yetu ilipopata uhuru. Uharakati wa kuondokana na magonjwa, ujinga, na umasikini. Uharakati wa kuhakikisha usalama kwa kila raia. Uharakati wa kukomeza Ufisadi.

Haya ni mapambano ya kuwalinda watu wote bila kuwabagua,
Ni mapambano ya kuwalinda maalbino.
Ni mapambano yaliyaonza mwaka 1961;
Ni mapambano yenye manufaa kwa kila mmoja wetu.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kaka Nape kamwe hawezi kupambana na MNYIKA one on one. Mnyika he is detailed informed kuliko Nape ambaye ni mzuri wa vibwagizo lakini vinakosa mishiko/nyama. Mnyika ni mzuri sana on details ba anajua kuzipanga na kuzitumia kuinua emotions.

Hata hivyo Mnyika atakuwa na kazi kubwa this time kuliko 2005 kwa kuwa hana advantage ya ujana, hana party network, hawezi siasa hovyohovyo kama ambavyo Nape ameweza kuonyesha hivi karibuni katika KAMPENI YAO YA VICOBA na zaidi Mnyika hana DOLA.

Kitakachomsaida MNYIKA ni siasa za makundi CCM zenye chimbuko lake tangia enzi za NAPE-MALECELA Vs NCHIMBI-JK....wale jamaa hawajamsahau bado na hili la VITA YA UFISADI (sio vita dhidi ya ufisadi) ndio line nzuri ya MNYIKA....

omarilyas

- Bwana Omaar, unasema kuna kiongozi Tanzania ya sasa aliyewahi kuchaguliwa kwa sababu ni mzuri wa details na more informed kuliko mwingine? Hebu mtaje mmoja tu mkuu wangu!

- Eti unasema siasa za makundi, sio wewe umekuwa unalia hapa makundi yaliyomtosa Zitto na Uenyekiti wa Chadema? Unasema Nchimbi ataacha jimbo lake kuja kumsaidia Mnyika Ubungo?

- Anyways, habari za Mashaka na Ukonga sasa nimezithibitisha kwamba ni za ukweli, isipokuwa bado sijathibitsha kuhusu mapesa yaliyosemwa, nimeongea na wazee wengi wa jimbo, hizi habari za Mashaka kutaka kujitosa huko ni za kweli, maana viongozi wengi wa mafisadi toka jana wamekuwa wakitafuta kujua habari background ya Mashaka.

Respect.

FMEs!
 
- Ningemshauri tu kwamba aweke mapema tena wazi, background yake na Kenya, maana itakuja kumharibia sana mbele ya safari hii, mafisadi jana nzima walikuwa wanahaha kutafuta historia yake ya maisha.

- Ni ushauri wa bure tu!

Respect.

FMEs!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom