John Tendwa na Ombi la Vyama Kushushwa Daraja, Serikali JE???

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Msajiili wa Vyama katika mahojiano yaliyorekodiwa na kituo cha TV, alisikika akisema utitiri wa vyama unakera na hivyo anapendekeza baadhi ya vyama vya siasa vishuwe daraja ili vibaki kuwa vyama vya harakati/wanaharakati tu.

Hoja ya Tendwa inatokana na ukweli kuwa vyama vingi tangu zipate usajili wa kudumu bado havijaweza ktk miaka 20 ya vyama vingi TZa kupata japo kiti kimoja cha udiwani wala Ubunge. Hoja yake inaukweli ndani yake.

Suala langu ni kwanini Tendwa asikifirie mbele zaidi na kusema serikali pia ishushwe daraja maana kuna serikali iko madarakani miaka 50+ lakini haijaweza kuinua uchumi wa TZ, kubadilisha maisha kuwa bora kwa wananchi wake, serikali imeshindwa hata kudhitibi mfumko wa bei, imeshindwa hata kutoa ulinzi wa raia na mali zake, serikali imeshindwa kukamata mafsadi, wala rushwa kubwa, imeshindwa kutoa huduma kwa jamii, imeshindwa kutoa elimu bora japo imeweka kiila mtu apate elimu, imeshindwa kumkomboa mkulima toka jembe la mkono hadi kilimo cha kisasa, imeshindwa kwa kila kitu isipokuwa sikukuuu na anasa, Je si sahihi serikali nayo ishushwe daraja??? kwa maana vyama vya siasa ni serikali in waiting, Kama in waiting anashughulikiwa aliyepo madarakani na kushindwa kila kitu tumfanyeje??

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom