John Samuel Malecela: Ameanza mahojiano dk 5 zilizopita TBC!

Shabani kisu anamhoji Mzee Malecela kihusu mafanikio na changamoto ndani ya miaka 50 ya Tanganyika/ Tanzania na changamoto za Umeme, Elimu na mambo mengine muda huu fuatilia....
 
anaongea mambo gani,hatuna haja ya kusikiliza magomvi ndani ya chama chao
 
Anasema lile time bomb la ajira,kweli tunalo. Lakini hata Marekani bomu hilo lipo,na India bomu hilo lipo..
 
Anasema anashangaa na angemchallenge mtu aliyesema kuna watoto wanaofika darasa la saba bila kujua kusoma.. Angemdai ushahidi!
 
Aaaaah, kumbe ni kuho? Nilidhani ni yale mahojiano yale yenyewe ya kiukweli kule ninhi ... kule BBC!!
 
anakubali tatizo la management ndiyo chanzo cha viwanda kufa.. Amekwepa upande wa ubinafsishaji. Shaaban Kissu kamwachia..
 
Sasa watakua wanamuuliza nini vile au kama labd sasa hivi anakubali yale Magamba ya Chama yaendelee tu kuzawadiwa nafasi ya kugombea urais 2015?
 
Anaongea mate yanaruka mdomoni kama mvua, naona mtangazaji anavuta kiti chake nyuma asije akalowa! huyu mzee wetu amechoka sana apunzike tu
 
Naona anaongea pumba kwamba Lisu alipinga masada kwa Sababu ni mpinzani tu du Kweli Mzee amezeeka nashauri shabani kisu ajikite katika kuongea na vijana zaidi kuliko wazee
 
Kuhusu katiba mpya amempa sifa JK kuendesha mchakato vema. Na hata kwenye bunge muswada ulipita bila matatizo yoyote. Anasema hashangai Chadema kupinga,maana ni wapinzani! Huwezi kutegemea wapinzani wakuunge mkono
 
katoa mfano hatuna haja ya kuchuna ngozi ya kiroboto.. Mchakato wa katiba mpya ni mzuri. Wananchi wawe tayari kutoa maoni yao..
 
Anasema anachukia sana ufisadi! Anaona mambo ya ajabu kununua gari Uingereza na kulisafirisha hadi nchini! Anasema mtu huyo sanda yake haitafika hata shilingi elfu kumi na tano[15,000/-],na kaburi la kawaida kama wengine... Kasema anawashangaa sana watu wa aina hii..
 
Back
Top Bottom