John Pombe Magufuli katika kipindi cha 45mn ITV

Mengi ya mambo aliyozungumza ni ya kufikirika zaidi kwa hali halisi ya Tanzania. Kwa mfano barabara ya kutoka Nzega kuelekea Igunga imeanza kuwa na mashimo makubwa ajabu na sidhani kama ina umri wa zaidi ya miaka 5. Feasibility study ya bara bara ya Nyakanazi-Kibondo-Kasulu ilifanyika 2008 lakini hadi sasa ni politics tu zinaendelea.

Halamashauri nyingi Tanzania wameshageuza uwekaji wa mabango bara barani ni projects zao na ni wazi hakuna siku atazuia hiyo kitu maana inagusa maslahi ya wanaume wenye ndevu kama yeye na ndio maana anaongea lakini mabango yanawekwa na hakuna kinachoendelea.

Tanzania bado hatujali suala la kutii sheria...wachace wanaothubutu ndio hao kwa sehemu ndogo wanaweza kufanikiwa na sio CCM....Mfano ndio huo halmashauri ya Moshi..:bange:
 
Jana katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa kila jumatatu na kituo cha ITV kuanzia saa 3 usiku alikuwepo Mh. John Pombe Magufuli. Na humu JF najua wapo wengi tu waliomsikiliza, kwani alielezea kinaga ubaga kwa muda mrefu kuhusu hali ya barabara nchini.
Kwa maelezo aliyoyatoa na kazi za ujenzi wa barabara zinazoendelea maeneo mbalimbali ya nchi aliyoyataja hakuna shaka kabisa ndani ya miaka 3 aliyoisema kuwa barabara zote zilizoahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi wa CCM zitakuwa zimekwisha.

Huu ni ushahidi tosha kabisa kuwa Tanzania yenye neema inawezekana na sio kweli kwamba serikali haijengi barabara. Hongera sana Mh. Magufuli na wananchi tuko pamoja nawe

Mkuu vipi kuhusu suala la "Mgawo wa Umeme kuwa historia"? kauli hii imekuwa ikirudiwa rudiwa na JK pamoja na Ngeleja kwa zaidi ya miaka mi5 sasa, na jana imerudiwa tena. Mbaya zaidi wakimaliza tu kujigamba tunapata "Mgawo wa Giza". Hii unaizungumziaje?
 
Kwa hakika namkubali jamaa yuko juu anajua nini kinafanyika wapi na ni mzuri katika kufuatilia. Tatizo tu yuko kwenye kile Chama Cha Magamba kilichojaa fitina na mizegwe hasa kwa wachapa kazi kama Mheshimiwa Alchol Locks
 
CCM kuna watu vichwa sana mkuu ! cha muhimu ni kupewa fursa ya wao kutenda kwa mujibu wa sera na taratibu
 
Mkuu vipi kuhusu suala la "Mgawo wa Umeme kuwa historia"? kauli hii imekuwa ikirudiwa rudiwa na JK pamoja na Ngeleja kwa zaidi ya miaka mi5 sasa, na jana imerudiwa tena. Mbaya zaidi wakimaliza tu kujigamba tunapata "Mgawo wa Giza". Hii unaizungumziaje?

Mkuu hili la mgawo wa umeme Magufuli aliliongelea ? mkuu kuwa ndani ya mada usiruke
 
we uliepamoja nae muulize mbona hazungumzii tena bomoa bomoa jijini Dar es salaam??????

Mkuu kwani suala la barabara ni suala la itikadi uwe ya chama fulani ? hata ww uko nae pia kwani anatujengea barabara tunazo tumia sote
 
Maghufuli ni mbwabwajaji namba moja ambaye hajapata kutokea mfano wake kipindi cha jana ndio kimenipa picha halisi ya huyu muheshimiwa kaongea vitu vingi vya kusadikika toka alivyoanza kusem hataki kuona Barabara zinaingiliwana mgari makubwa yanayopaki kwenye feeder roads karibu miezi sita hakuna gari hata moja lilotoka haswa jiji la Dar es Salaam,huyu si mtu wa kumwamini kwa kusema data kibao na kukariri mafigure na mahesabu bila utekelezaji,anajishusha hadhi kila siku,ni maneno mengi vitendo hakuna , hatuna waziri hapo ni vuvuzela lingine
 
Amesifia hakuna mwananchi anayefanya biashara maeneo ya reserve road.pia kuanzia himo hakuna kutupa takataka hovyo!amesema ni bora halmashauri zote zijifunze toka moshi!source itv
Duu mkuu umenikumbusha my wife juzi alienda Moshi alipofika stand akanunua voucher alipomaliza kukwangua na kuingiza zile namba si akajisahau akatupa vocha, jamaa walimg'ang'ania mpaka TZS 30,000 ilimtoka baada ya mabishano ya saa 2....Hongereni sana manispaa ya moshi mnafanya kazi nzuri...ila hiyo TZS sikuona risiti yake
 
Maghufuli ni mbwabwajaji namba moja ambaye hajapata kutokea mfano wake kipindi cha jana ndio kimenipa picha halisi ya huyu muheshimiwa kaongea vitu vingi vya kusadikika toka alivyoanza kusem hataki kuona Barabara zinaingiliwana mgari makubwa yanayopaki kwenye feeder roads karibu miezi sita hakuna gari hata moja lilotoka haswa jiji la Dar es Salaam,huyu si mtu wa kumwamini kwa kusema data kibao na kukariri mafigure na mahesabu bila utekelezaji,anajishusha hadhi kila siku,ni maneno mengi vitendo hakuna , hatuna waziri hapo ni vuvuzela lingine
Magufuri ni Kiongozi mzuri sana sema wasaidizi wake na wakubwa wake ni tatizo....
 
Hv kadaraja kalikozolewa na maji njia inayopita UDSM vp ? Kalishajengwa ? Maana ile njia ni msaada mkubwa wa kupunguza foleni ktk junction ya ubungo tokea Kimara. Saiz ni karibu wiki 3 toka kazolewe.

Magufuli + Mnyika mpo ?
 
nakumbuka lawrence masha aliyekuwa waziri ya mambo ya ndani hajui hata tanzania kuna magereza mangapi!
 
Maghufuli ni mbwabwajaji namba moja ambaye hajapata kutokea mfano wake kipindi cha jana ndio kimenipa picha halisi ya huyu muheshimiwa kaongea vitu vingi vya kusadikika toka alivyoanza kusem hataki kuona Barabara zinaingiliwana mgari makubwa yanayopaki kwenye feeder roads karibu miezi sita hakuna gari hata moja lilotoka haswa jiji la Dar es Salaam,huyu si mtu wa kumwamini kwa kusema data kibao na kukariri mafigure na mahesabu bila utekelezaji,anajishusha hadhi kila siku,ni maneno mengi vitendo hakuna , hatuna waziri hapo ni vuvuzela lingine
agiza pepsi baridi kwa bili yako
 
Mh. Magufuri na Takwimu kichwani

Hakika inafurahisha sana yaani Magufuri unataja (off head) urefu na majina ya barabara kuu na za mikoa za Tanzania, idadi ya Makandarasi waliosajiriwa, bajeti ya matengenezo ya barabara, wafadhili mbalimbali wa miradi ya barabara na madaraja n.k
Inaonyesha si tu kuwa unajua unachoshughulika nacho bali pia ulivyo na uwezo (Kipawa) wa kipekee wa kuweka kumbukumbu .

Hongera sana kwa kuongelea UVUNJAJI WA SHERIA KATIKA ROAD RESERVES NA KULITILIA MKAZO KILA MTU AWAJIBIKE KWA LILE ANALOPASWA KUAJIBIKA NALO!!!

Pamoja na yote nimeona kosa moja dogo kuwa Mh. Unafika mahala unalazimisha wewe ndiye uongoze kipindi kwa kusema unachotaka na si kujibu maswali ya mwandaaji wa kipindi na mwandaaji naye akabaki tu naitikikia mh! mh! Hili ni kosa dogo la kiufundi katika masuala mazima ya kuongea katika kadamnasi kupitia vyombo vya habari .
Hata hivyo nimefarijika na jinsi ulivyowasilisha Wizara yako na matarajio yako na kile unachokiamini.
Ujuaj hajaanza Leo huyu ndugu
 
Back
Top Bottom