John Pombe Magufuli katika kipindi cha 45mn ITV

Magufuli aisifia mji wa moshi! NDESAMBURO umeonyesha kuwa upinzani ndio suluhisho la maendeleo nchi
 
Amesifia hakuna mwananchi anayefanya biashara maeneo ya reserve road.pia kuanzia himo hakuna kutupa takataka hovyo!amesema ni bora halmashauri zote zijifunze toka moshi!source itv
 
anatoa wito kwa watanzania.wasiwe wanashushwa wanapokaribia minzani.na kama wewe ni mula rushwa hata kama unapokea mshahara elfu50 utakula rushwa tu.
 
Naona masifa atamzidi awamu Hii. Maana akigusa maslahi ya wakubwa atapingwa.
Anasema ukweli lakini utekelezaji taabu.
 
Anahitimisha na kuwashauri makandarasi wazalendo waungane wakati wa kuomba kazi. Waache majungu na kupigana vita.
 
Mh. Magufuri na Takwimu kichwani

Hakika inafurahisha sana yaani Magufuri unataja (off head) urefu na majina ya barabara kuu na za mikoa za Tanzania, idadi ya Makandarasi waliosajiriwa, bajeti ya matengenezo ya barabara, wafadhili mbalimbali wa miradi ya barabara na madaraja n.k
Inaonyesha si tu kuwa unajua unachoshughulika nacho bali pia ulivyo na uwezo (Kipawa) wa kipekee wa kuweka kumbukumbu .

Hongera sana kwa kuongelea UVUNJAJI WA SHERIA KATIKA ROAD RESERVES NA KULITILIA MKAZO KILA MTU AWAJIBIKE KWA LILE ANALOPASWA KUAJIBIKA NALO!!!


Pamoja na yote nimeona kosa moja dogo kuwa Mh. Unafika mahala unalazimisha wewe ndiye uongoze kipindi kwa kusema unachotaka na si kujibu maswali ya mwandaaji wa kipindi na mwandaaji naye akabaki tu naitikikia mh! mh! Hili ni kosa dogo la kiufundi katika masuala mazima ya kuongea katika kadamnasi kupitia vyombo vya habari .
Hata hivyo nimefarijika na jinsi ulivyowasilisha Wizara yako na matarajio yako na kile unachokiamini.
 
Mod. Samahani: kuna makosa.
Kichwa cha habari ni Mh. Magufuri Mtu wa Data Kichwani.
 
Mod. Samahani: kuna makosa.
Kichwa cha habari ni Mh. Magufuri Mtu wa Data Kichwani.
Kwa thread ya nani unataka kuedit??Thubutu weka yakwako yenye kichwa cha habari unachotaka wewe!!Copyright mzee heshimu mawazo ya wenzako na sikuona yakwako ndiyo bora kuliko waliokutangulia!
 
Jana katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa kila jumatatu na kituo cha ITV kuanzia saa 3 usiku alikuwepo Mh. John Pombe Magufuli. Na humu JF najua wapo wengi tu waliomsikiliza, kwani alielezea kinaga ubaga kwa muda mrefu kuhusu hali ya barabara nchini.
Kwa maelezo aliyoyatoa na kazi za ujenzi wa barabara zinazoendelea maeneo mbalimbali ya nchi aliyoyataja hakuna shaka kabisa ndani ya miaka 3 aliyoisema kuwa barabara zote zilizoahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi wa CCM zitakuwa zimekwisha.

Huu ni ushahidi tosha kabisa kuwa Tanzania yenye neema inawezekana na sio kweli kwamba serikali haijengi barabara. Hongera sana Mh. Magufuli na wananchi tuko pamoja nawe
 
There's a big difference wakati Wizara hii ilipokuwa inaongozwa na Shukuru Kawambwa (Sijui hata kama alikuwa anajua kuna idadi ya makandarasi wangapi Tanzania) na sasa inapoongozwa na Magufuli kwanza niseme hicho kipindi nilikiangalia jana na huyu jamaa alikuwa anatoa data ambazo zinaeleweka na kukufanya hata kama ulikuwa haujui hali za barabara hapa chini basi unaweza angalau kuambulia machache kati ya mengi aliyoongea laiti kama mawaziri wote wangekuwa kama huyu jinsi anvyojua kufanya kazi yake.
 
mkuu huyu bazazi tuu ana jipya
watu wanakula na wanaendelea kula hiyo wizara mpaka kesho kutaka kukuonyesha upumbavu wake mwezi uliopita alitangaza kampuni moja aitakaa ieppwe dili la kazi za barabara sababu wana kazi nyingi aijakamlilika wiki moja baadae akatangaza kampuni zilizopewa tenda za barabara uwezi aminisaa ile china construction iko kwenye list nakwambia akuna waziri anaetoka maskini na hii wizara ni msanii tuu hana jipya
 
Kipindi hiki ni upuuzi

Mwongoza kipindi bogus hajui kuuliza maswali

Mkuu great thinker siku zote sio mtu wa kulaumu hutanabaisha tatizo na kulitolea solution yake, huo ndio wajibu wake. Kwa maana hiyo basi wewe unataka kipindi kiendeshweje? unataka maswali yaulizwaje? au kifutwe ? nk
 
we uliepamoja nae muulize mbona hazungumzii tena bomoa bomoa jijini Dar es salaam??????
 
Back
Top Bottom