John na japhet

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
John alimtembelea rafiki yake Japhet ili ajue maendeleo ya ujenzi wa nyumbaya Japhet. John akafika kwenye hiyo nyumba mpya ya japhet na kumkuta rafikiye akitokwa na majasho mengi huku akiwa bize kupiga nyumba rangi, Kumwangalia Japhet vizuri, John akagundua kuwa kumbe rafikiye alikuwa amevaa makoti mawili.Ilibidi John amhoji Japhet kwa nini kuvaa makoti mawili mchana na jua liko utosini. Mazungumzo yalikwenda hivi:
JOHN: "Eee bwanae! Mbona makoti mawili jua lote hili?
JAPHET: "Nataka kazi hii ya rangi iwe safi"
JOHN: "Ndo uvae hayo makoti?"
JAPHET: "Hasa!" Kisha kusema hivyo,Japhet alinyanyua kopo moja la rangi na kumwonesha John huku akimwambia, "Soma hapa!" John alisoma maandishin haya kwenye kopo la rangi: "FOR BEST RESULTS PUT ON TWO COATS.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom