TANZIA John Mwankenja auawa kwa risasi

HAYA SASA KWA WALE WABISHI MSEMAO TANZANIA INA AMANI HAPO NDIO MPATE MAJIBU,Hii nchi haipo sawa!
 
hebu tupeni taarifa yenye ukamilifu ndugu. fuatilieni hilo. na mwakyembe tanga alikuwa saa ngapi?
 
Mh hii ina tisha sana,
Kama tumefika huko ni balaa.
Mungu atuhurumie atupe njia muafaka ya kutatua mambo yetu na atujaze utu na hekima.
Mungu ailaze peponi roho ya marehem
 
8589601.jpg


Marehemu John Mwankenja


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Wilayani Rungwe, John Mwankenja ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kiwira mkoani Mbeya ameuawawa kwa kupigwa risasi usiku tarehe 18 Mei 2011 majira ya saa 5.00 wakati akishuka kwenye gari lake kuelekea nyumbani kwake.

Habari zilizoifikia blogu ya "Mbeya Yetu" zinaeleza kuwa Marehemu alipigwa risasi kadhaa wakati akishusha mguu wake kutoka kwenye gari kabla ya kuingia nyumbani kwake eneo la Kiwira.

Maiti yake imepelekwa katika hospita ya Makandana kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekwisha kamatwa kuhusiana na tukio hilo.
 
Haya ni majambazi tu!! Hakuna sababu yoyote ya kutoa uhai wa mtu si siasa si nini!! Jeshi letu la polisi tafadhali wayatafute hayo majambazi wasitumalizie wananchi wasio na hatia. Nchi yetu imefika pabaya sana!! Mambo haya tulizoea kuyaona kwenye senema tu!!!!
 
A thorough investigation should be carried out to know the source/cause of the assassination. We don't want just easy answers,..like he was killed by robbers who could not take anything b/se the public was awake, etc.
If the source/cause is not establsihed, we may encounter many more assassinations of the same nature.
The investigation should not be only directed to politics but it should be broad to include family, business, community, etc.
Our thoughts goes to his family and CCM community in Mbeya.
R.I.P Mwankenja!!!!
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mh. Mwankenja ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa leo majira ya Nne na dk 10 nyumbani kwake Kiwira. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa marehemu Mwankenja alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.

Wauaji walitoweka mara baada ya kukamilisha mauaji yao na kabla ya watu kukusanyika. Hadi sasa sababu za mauaji hayo hazijafahamika. Hata hivyo baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu usiku huu wanahofu mauaji hayo kuhusiana na masuala ya kisiasa.
Poleni saana wana Rungwe wape pole saana familia ya marehemu. Mungu awape nguvu ya kuhimili machungu ya msiba huo mzito!!!!!!!! Lakini jamani Watanzania tuache mambo ya ubwenyenye, huyu mtu alirundikiwa madaraka mengi tena makubwa, Mkt wa CCM Wilaya, Mkt wa Halimashuri Wilaya, Diwani wa kata,bila shaka mjumbe wakamati sijui ipi na tume kibao. Vyote hivyo ni mzigo mzito kila anapokanyaga. Poleni wandugu wafiwa!!!!!!!!!
 
Poleni wafiwa. Tumeondokewa na nguvu kazi muhimu wakati tukiitegemea. MUngu ampe ppumziko la milele.
Ila kauli chafu kama za Kagasheki zisipewe nafasi kuwa chama fulani kinausika na mauaji.
 
Poleni wafiwa. Tumeondokewa na nguvu kazi muhimu wakati tukiitegemea. MUngu ampe ppumziko la milele.
Ila kauli chafu kama za Kagasheki zisipewe nafasi kuwa chama fulani kinausika na mauaji.

Rungwe bado hakuna nguvu ya chama fulani, huko CCM bado imeshika hatamu, kama ni sababu za kisiasa basi ni za ndani ya CCM yenyewe au katika utendaji wa kazi zake.
 
jana mishale ya saa tano usiku mwenyekiti wa ccm wilaya ya rungwe ndugu mwankenja ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasio julikana nyumbani kwake kiwira tukuyu. Habari zina sema waliomuua hawaja chukua kiti chochote kile. Tunawapa pole familia ya marehemu mwankenja na wana ccm wote wa rungwe.
 
Back
Top Bottom