Las Mas Bobos
JF-Expert Member
- Jun 15, 2012
- 991
- 326
Sidhani kama mtu anayeropoka hurudia mara mbili kwa msisitizo. Mnyika alikuwa anajua anachokifanya na Lukuvi na Ndugai wanalijua hilo na ndiyo maana wakaamua kumkatiza asiendelee kuwamwagia sumu. Kama Ndugai hakumpa nafasi ya kutoa maana ya kumwita Rais dhaifu ulitaka atolee wapi? ni dhairi atafanya hivyo nje ya bunge.
Nafikiri Ndugai ndiyo alikurupuka na sasa ataonekana yeye ndio dhaifu kuliko hata huyo rais anayemtetea. Tukianza kuwekeana mipaka ya nini kiongelewe tutakuwa na wabunge mazuzu wengi zaidi ya wale wa CCM ambao tayari ni loss kwa taifa.
Pamoja sana mkuu. Kama kuna mtu anadhani haya maneno huwa yanaropokwa, naomba akamkumbushe Spika kuhusu ule ushahidi wa Godbless Lema kuhusu kauli yake kuwa PM ni MUONGO. Mbona hawataki kuusikia mpk leo?
Kama Mnyika anao ushahidi kuwa Rais ni legelege na alitakiwa apewe nafasi ya kuelezea na sio kumwambia afute kauli, utafuta vipi UKWELI!