JOHN MNYIKA: Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu bungeni!

habari ndo hiyo...hivo ndivo tulivoelewa toka kitambo..sema naibu spika kaingiza siasa kama kawaida yake...haiwezekani kuzikalia kimya kauli walizotoa wabunge wa chama chake toka jana za kuwaita wabunge wa upinzani machizi wana pepo na leo kashabikia kauli za kibajaji lusinde bila kuwawajibisha then inatoka kauli ya mnyika inakua isue...?? siasa zinaliangamiza taifa letu...ccm siowazalendo....

spika kajijitea kwamba jana hakuendesha kikao yeye hivyo hawezi kujibu ya jana ambayo kiti cha spika kilikaliwa na mwingine ( two wrongs don't make one right)
 
Ameshaanza kujitetea, hii ndio faida ya kuropoka. Sasa woga wa nini wakati umesha chafua hali ya hewa?

Sidhani kama mtu anayeropoka hurudia mara mbili kwa msisitizo. Mnyika alikuwa anajua anachokifanya na Lukuvi na Ndugai wanalijua hilo na ndiyo maana wakaamua kumkatiza asiendelee kuwamwagia sumu. Kama Ndugai hakumpa nafasi ya kutoa maana ya kumwita Rais dhaifu ulitaka atolee wapi? ni dhairi atafanya hivyo nje ya bunge.

Nafikiri Ndugai ndiyo alikurupuka na sasa ataonekana yeye ndio dhaifu kuliko hata huyo rais anayemtetea. Tukianza kuwekeana mipaka ya nini kiongelewe tutakuwa na wabunge mazuzu wengi zaidi ya wale wa CCM ambao tayari ni loss kwa taifa.
 
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

John Mnyika
19 Juni 2012
"The will of the People shall be the Ruling force in any society.....Go on Champ time will tell and nature will countercheck."
 
Mkuu, CDM wamechangia kivipi udhaifu wa rais wenu??

tatizo hapa hatuelewani, spika hajasema kusema Rais dhaifu ni kosa kasema ni kosa kwa kanuni za bungeni hivyo maneno hayo hayo angesema nje ya bunge kanuni za bunge zisingembana
 
Kuja kutoa ufafanuzi nje ya mbunge haisaidii Mnyika angekiokoa chama chake kwa kutoa maneno ambayo yamepelekea adhabu

Mbona wewe unakiherehere sana? Kwani ufafanuzi alioutoa alikwambia una lengo la kukitetea chama chake? Wanaotetea vyama vyao ndio wale waliobakia bungeni wakiogopa kusema ukweli lkn wakifika nje wanaongea unafiki.

Unafikiri Mnyika ni taahira kiasi atoe malalamiko meeeengi kuhusu bajeti halafu mwishowe aseme anaunga mkono kwa 100%?

Kama huna cha kuchangia kaa kimya, chama chama, unafikiri Mnyika anawakilisha chama, pale anawakilisha wananchi na ndio maana anajitetea kwa wananchi.
 
Inawezekana Rais ni dhaifu lakini spika anasema hiyo siyo lugha ya kibunge labda kama atakwenda kusemea mtaani ( nje ya mbunge) kwani bungeni anabanwa na kanuni

Hapo spika ame tupotosha kwa kututaka kutuaminisha hivyo swala liko wazi tuu kuwa JK ni dhaifu sana tena kiutendaji kama anajiamini yeye ni ngangali amwage wali na mchuzi si twajua wana lindana kimtido.

Hii kama ni mbwai mbwai tuuuu


 
Sasa mbona anaomba apewe nafasi ya kujitetea? Kama sio woga huo ni nini?

Sio uoga,asipotoa ufafanuzi hatakua hawatendei haki wananchi,kwani madini aliyotaka kutoa ndugai kayakatisha,so ni better ayarushe kwenye mtandao tuweze kupata yale madini tuyasambaze mtaani
 
Mbona wewe unakiherehere sana? Kwani ufafanuzi alioutoa alikwambia una lengo la kukitetea chama chake? Wanaotetea vyama vyao ndio wale waliobakia bungeni wakiogopa kusema ukweli lkn wakifika nje wanaongea unafiki.

Unafikiri Mnyika ni taahira kiasi atoe malalamiko meeeengi kuhusu bajeti halafu mwishowe aseme anaunga mkono kwa 100%?

Kama huna cha kuchangia kaa kimya, chama chama, unafikiri Mnyika anawakilisha chama, pale anawakilisha wananchi na ndio maana anajitetea kwa wananchi, toy we

Mishipa inakutoka kulikoni, Mnyika hajatolewa nje kwa kukosoa bajeti bali kwa maneno ambayo kanuni za bunge zimeanisha kama matusi, udhalilishaji nk.
 
Nimegundua common sense sometimes is not common!
Udhaiu wa JK kama raisi ndo tumefika apa!
Kama amiri jeshi mkuu Qatar wameleta dege lao kuja chukua wanyama wetu tena wakiwemo Twiga ambao ni marufuku kuwasafirisha wakiwa hai isipokuwa kwa sababu maalum.
TRA kila siku wanapresent mapato ndivyo sivyo wakuu wao bado wanapeta!
Watu wameiba ela za safari za JK ivi enzi za mwalimu unaweza thubutu fanya haya!Ni udhaifu wake ndo unafanya watu wafanye watakavyo wanajua hawezi act!
 
Huo ni msimamo wa chama au wako binafsi. Kwa nini Zito yuko tofauti nawe juu ya msimamo wako wa kumsuta Rais

Wewe PIMBI unafahamu namna ya kukopi tweet za watu au mnakopi tweet za ma coward wa magamba wanaolalamika kwa zito na kudha ni za zitto hebu cheki hii....

Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe
Wanaomlaumu Mnyika hawakupata fursa kusikiliza alikuwa anasema nini? Rais anaruhusu vipi mpango wa maendeleo aliousaini ukiukwe?
 
Back
Top Bottom