John Mnyika awe mwenyekiti CHADEMA...

Hakuna sehemu niliyosema ku 'compromise ' ni kuwa double agent..
ku 'compromise ni mfano wa Zitto ambae
jimbo lake 'vitu kama barabara na shule'
vimepatikana wakati ni serikali ya ccm 'imewezesha'
na yeye alikiri na kukataa kushiriki kutoka nje wakati Kikwete anahutubia bunge...
na sasa anaonekana
ni 'msaliti'...

huwezi kuwa mpinzani 'ukawajengea barabara jimboni mwako'
lazima uka 'lobby' na ku 'lobby ni ku 'compromise'
elewa siasa inavyochezwa...


Hapo bolded wengi ndio wanapatilia shaka, kwamba mheshimiwa huyu nidhamu ya uoga ameipata kutoka shule gani? Je mnyika naye kaenda lini shule hii ya nidhamu ya woga mpaka ameaminiwa kuwa apigiwe debe kuwa mkt wa cdm ili aondoe huu utaratibu wa maandamano, ambayo yanawanyima usingizi viongozi wetu hawa mafisadi?
 
mkuu kwenye politics
'image na reputation' ni kila kitu..
ishu sio ukweli,ishu ni nini watu wanaamini kuwa ni 'ukweli'

Mkuu BOSS, katika kampeni za uchaguzi za 2010 Magamba katika propaganda zao walijitahidi sana kuionyesha CHADEMA kama ni chama cha Wakristo na Wachagga lakini pamoja na upumbavu huo wa magamba lakini bado CHADEMA walijikusanyia kura nyingi za makabila mengine na hata Waislamu na hivyo kujiongezea viti vingi bungeni, hivyo reputation na hiyo image wakati mwingine inaweza kabisa isiwe na ukweli wowote na wapiga kura wasiikubali kabisa.

Kwa hiyo kwa kuhitimisha pamoja na jitihada za nguvu za Magamba za kukipaka matope CHADEMA kwamba ni chama cha Wakristo na Wachagga lakini wapiga kura hawakuamini hivyo na ndio maana Magamba walikuwa hawana jinsi bali kuuchakachua uchaguzi ule vinginevyo sasa hivi kungekuwa na mkazi tofauti pale Ikulu.

 
Ukifuatilia matatizo meengi ya nchi hii
utakuta tatizo la 'age gap' kati ya viongozi wanaotawala na wananchi..

zaidi ya nusu ya watanzania ni 'below 30 years old...inasemekana almost 60
au 75 percent ya watanzania umri ni below 35
na ukichukua below 40 unaweza kukuta ni almost 65-80 percent....
mwenye accurate data
tafadhali aweke hapa.......

sasa basi mimi kwa maoni yangu naona viongozi kama Zitto,Mnyika,January,Kafulila na wengineo vijana
angalau wana 'advantage' ya kuwa connected na masula hasa ambayo viongozi
kama Kikwete na wazee wenzake wengi hawaelewi kabisa...
kuna a 'A BIG DISCONNECTION' kati ya wananchi na wazee kwa hakika...

Mimi ningependa Zitto awe mwenyekiti CHADEMA....lakini
ameshaanza kuwa 'na wapinzani wengi' ndani ya CHADEMA itakuwa ngumu kwake kupata
Uenyekiti au 'legitimacy' inayohitajika pengine kwa sasa....

sasa nilipomuangalia John Mnyika jinsi alivyoendesha kampeni ya ubungo
bila 'kumjeruhi' Julius Mtatiro na jinsi 'anavyo perfom bungeni now'
pamoja na kutomkubali huko nyuma,ameni convince now kuwa 'he is a better leader'
kulinganisha na wengine ndani ya CHADEMA....

1.Sifa ya kwanza ni 'uniter'..ataweza kuunganisha CHADEMA na vyama vingine.


2.Sifa ya pili anapenda 'dialogue' kuliko 'maandamo'....


3.Sifa ya tatu ambayo mimi naona ni muhimu mno now ni age...
ata 'connect' na wananchi ambao wengi ni vijana
yuko engaging na watu....

4.hana 'political garbage' ya aina yeyote for now...haitaji kulipa fadhila kwa yeyote
yuko free kufanya maamuzi kwa jinsi anavyoona,ana uwezo wa kuwa 'ndependent'
kimawazo...

na sifa zingine nyingi kumlinganisha na wengine......

now its time,tukisubiri 'azeeke' atakuwa 'corrupt' na mazoea na culture za siasa za makundi

Chadema wafanye kama DEMOCRATS walivyofanya kwa OBAMA....

mimi nafikiri its time Mnyika awe Mwenyekiti,CHADEMA itawasaidia
1.hoja ya uchagga na ukaskazini
2.hoja ya chama cha familia...

na hoja zingine...nyiingi....Urais anaweza kugombea SLAA au yeyote but Mnyika awe Mwenyekiti....

Hapana! haitawasaidia CDM bali itakusaidia wewe na magamba wenzako
 
Inaonyesha Mbowe anawanyima usingizi ndugu zetu wa magamba!

Mbowe hatuna shida naye hata kidogo..anaweza kuongea na sabodo, lowassa etc ..

Ninachoogopa kwenye hii thread ni "hilo bifu la mbowe kwa Mnyika"

Boss humpendei mema mwenzako halo
 
Ahsante sana Mkuu. Mie nawahusudu sana Wachagga na nina bahati kubwa sana ya kuelewana nao kupita kiasi, labda nina damu yao kiasi hahahaha lol!
Mkuu BAK,hawa watu wanaoihusisha chadema na uchagga hawawafahamu uchagaa ndo shida.

Na hakuna mtu anayejisumbuwa kuwaelewesha,hata huyo Mnyika mwenyewe historia ya wachagga aliyonayo ni welll distorted,kulishakuwa na mjadala kama huo miaka ya nyuma na nilishangazwa sana na ukosefu wake wa busara.

Mkoa wa Kilimanjaro,chadema ina inlfuence kama ilivyo kwa mikoa mingine tofauti na Kililimanjaro.

Mji wa moshi umeshikiliwa na chadema kwa muda through Ndesamburo,lakini hilo ni jimbo moja tu la Mkoa wa Kilimanjaro,na pia ni hulka ya miji mingi ya Tanzania kushikiliwa na upinzani hususan chadema,si Moshi peke yake...

Kuna jimbo linaloshikiliwa na TLP through Mrema,kuna jimbo limeshikiliwa na ccm miaka nenda rudi,jimbo la Rombo chini ya Mramba,kuna Moshi vijijini linaloshikiliwa na Chami wa ccm...Kote huko ndipo mahali halisi wachagga walipotokea.

Sasa unapozungumiza uchagga,unazungumzia mkoa wa Kilimanjaro,sasa hapo kuna uchagga na uchadema kweli?

Kama kuna uchagga uko chadema,ni lazima wawe specific kuwa ni uchagga wa wapi,kwani hawatambui kuwa hata wachagga nao ni tofauti?

Kwasababu kama chadema kingekuwa chama cha wachagga,then ni kwanini warombo ama moshi vijijini ama vunjo hawakukichaguwa?

Watumie akili na waisome historia ya nchi yetu vyema na si ku spread chuki tu.
 
mkuu kwenye politics
'image na reputation' ni kila kitu..
ishu sio ukweli,ishu ni nini watu wanaamini kuwa ni 'ukweli'
Soma bandiko langu nililomjibu BAK,halafu assume nimelielekeza kwako.

Nili avoid duplications...Hiyo image na reputation ni a distorted one!
 
kweli mnyika mwenyekiti slaa awe makamu na zitto awe katibu wenje naibu katibu na wamtafute kijana msomi awe msemaji wa chama
 
Soma bandiko langu nililomjibu BAK,halafu assue nimelielekeza kwako.

Nili avoid duplications...Hiyo image na reputation ni a distorted one!

actually sijasema image na reputation ni real...
hata kama ni 'distorted one'
je haina damage?????
 
actually sijasema image na reputation ni real...
hata kama ni 'distorted one'
je haina damage?????

Inategemea BOSS jinsi wapiga kura wanavyodhani/wanavyotaka. Unakumbuka ya Bill Clinton baada ya scandal ya Monica Lewinsky? hakuna aliyedhania kama angeshinda awamu ya pili...Pia nadhani unakumbuka mambo ya 'Bama walipokuwa wanasema, "America is not ready for a Black President." lakini wapiga kura wakafanya vitu vyao ambavyo hata Mapundits waliobobea hawakuvitegemea kabisa.
 
Mkuu BAK,hawa watu wanaoihusisha chadema na uchagga hawawafahamu uchagaa ndo shida.

Na hakuna mtu anayejisumbuwa kuwaelewesha,hata huyo Mnyika mwenyewe hstoria ya wachagga aliyonayo ni welll distorted,kulishakuwa na mjadala kama huo miaka ya nyuma na nilishangazwa sana na ukosefu wake wa busara.
Mkoa wa Kilimanjaro,chadema ina inlfuence kamailivyo kwa mikoa mingine tofauti na Kililimanjaro.

Mji wa moshi umeshikiliwa na chadema kwa muda through Ndesamburo,lakini hilo ni jimbo moja tu la Mkoa wa Kilimnjaro.

Kuna jimbo linaloshikiliwa na TLP through Mrema,kuna jimbo limeshikiliwa na ccm mika nenda rudi,jimbo la Rombo chini ya Mramba,kuna linaloshikiliwa na Chami wa ccm.

Sasa unapozungumiza uchagga,unazungumzia mkoa wa Kilimanjaro,sasa hapo kuna uchagga na uchadema kweli?

Kama kuna uchagga uko chadema,ni lazima wawe specific kuwa ni uchagga wa wapi,kwani hawatambui kuwa hata wachagga nao ni tofauti?

Kwasababu kama chadema kingekuwa chama cha wachagga,then ni kwanini warombo ama moshi vijijini ama vunjo hawakukichaguwa?

Watumie akili na waisome historia ya nchi yetu vyema na si ku spread chuki tu.

nakubaliana na wewe.wahaya wengi ambao wangeisaidia nchi hii wanaogopa kuingia ktk siasa kutokana na madai ya kipuuzi kama haya ya ukabila.
 
Inategemea BOSS jinsi wapiga kura wanavyodhani/wanavyotaka. Unakumbuka ya Bill Clinton baada ya scandal ya Monica Lewinsky? hakuna aliyedhania kama angeshinda awamu ya pili...Pia nadhani unakumbuka mambo ya 'Bama walipokuwa wanasema, "America is not ready for a Black President." lakini wapiga kura wakafanya vitu vyao ambavyo hata Mapundits waliobobea hawakuvitegemea kabisa.


watanzania bado sana aisee
kama kuna mtu better na clean ni bora aisee
 
  • Thanks
Reactions: BAK
watanzania bado sana aisee
kama kuna mtu better na clean ni bora aisee

BOSS simuoni mtu kama huyo ndani ya Magamba, bila ya kuchakachua uchaguzi kwa kutumia tume ya uchakachuaji chaguzi na vyombo vya dola basi Magamba hawana chao.
 
Hata wao (Waarabu) walikuwa Kondoo ndio maana yule fisadi Mubarak aliweza kukaa madarakani zaidi ya miaka 30 na chaguzi za kishkaji huku akiendelea kukwapua mabilioni ya dollars za misaada toka US. Watu wakisema sasa basi liwalo na liwe basi hakuna wa kuwazuia. Kama walivyoweza Wamisri na Watanzania pia tunaweza kabisa...YES WE CAN!!!

Sikupenda niingilie hapa ila nimevutiwa na majibizano yako na Mwita!
Mkuu wangu BAK, sitaki kukukatisha tamaa ila pia siwezi kukuruhusu ujipe moyo kiasi hicho,
nakubaliana na Mwita kuwa sisi watz ni "MAKONDOO" kweli jamani.
Labda kwa kizazi kijacho cha wajukuu wetu ila hichi cha sasa ni hamna kitu kabisa.
Saiv huku bongo tunaburuzwa kwenye suala la katiba lakini kila kitu kinaendelea as usual utafikiri KATIBA ni suala la watu flani tu.
Nina sikitishwa sana na mwamko wa sisi wabongo katika masuala ya misingi mikuu ya nchi.
Ntarudi na hoja kwa The B!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom