John Mnyika awe mwenyekiti CHADEMA...

Na pata taabu ni saidie, kucompromise na ccm ndio maana yake uwe double agent? Kwa hiyo mnyika naye ni double agent ambaye ni makini kuliko zitto na umepewa kazi ya kumpigia debe, napata taabu kweli.

Hakuna sehemu niliyosema ku 'compromise ' ni kuwa double agent..
ku 'compromise ni mfano wa Zitto ambae
jimbo lake 'vitu kama barabara na shule'
vimepatikana wakati ni serikali ya ccm 'imewezesha'
na yeye alikiri na kukataa kushiriki kutoka nje wakati Kikwete anahutubia bunge...
na sasa anaonekana ni 'msaliti'...

huwezi kuwa mpinzani 'ukawajengea barabara jimboni mwako'
lazima uka 'lobby' na ku 'lobby ni ku 'compromise'
elewa siasa inavyochezwa...
 
haswaaaa ulipokuja wewe ndipo nilipo pataka
mimi nimemfananisha na wengine CHADEMA nimemuona yeye zaidi
tazama
1Zitto -yuko 'tarnished' na makundi ya CHADEMA
2.Mbowe- the same,background yake 'haiko convincing,hana kipya..
3. Slaa- yuko tarnished kwa waislam,na skendo ya ndoa yake..
4.Lissu- yuko so 'mwanaharakati' kuliko kuwa mwanasiasa...ana ugomvi na CUF na NCCR tayari
hawezi ku UNITE
5..Mdee- hayuko on her own ki chama,anaeegemea kundi..fulani

umeonaaa??????

mixed feeling........
 
Kama unafuatlia Bunge kwa ukaribu, utabaini kuwa hoja anazozijenga, nyingi huwa zinakubaliwa. kwa mara ya mwisho leo, katoa hoja ya kuongeza vifungu kwenye maazimio ya Bunge katika ripoti ya kamati ya jairo na Spika hakuwa na hoja za kukataa hoja za mnyika, hata alipojaribu kutaka kuzinyoosha, Mnyika alitoa hoja ambazo zilimwacha spika hana cha kusema kiasi cha kuzikubali moja kwa moja.

Kinachofurahisha zaidi ni jinsi alivyo na uwezo mkubwa wa kujenga hoja. Mark my words HOJA. haja jazba na anachokisema kinaeleweka kwa sababu kina mantiki.

Ukija Ubungo, anaweza kuwa asionekane amefanya chochote cha maanz phisically lakini nakumbuka kuna daraja (sikumbhuki vema lipo wapi lakini linaunganisha barabara ya huo Kikuu) bila harakati za Mnyika nadhani mpaka leo lingekuwa halijajengwa na linakuwa linaleta usumbufu mkubwa sana. lakini, Mnyika ni kati ya wabunge wachache sana ambao wana kawaida ya kuwazungukia wananchi wao, kabla ya kikao chochote cha bunge ili kukusanya maoni kulingana na hoja zitakazojadiliwa, na pia kurudi kwa wananchi baada ya kikao kutoa feedback. Sijaona wabunge wengi wakifanya hivyo.

Kusema kweli nimekubali utendaji na ujengaji hoja wa Mnyika.
Awasaidie kwanza wanananchiwa ubungo,kwani akiwa mwenyekiti ndo atapata nafasi zaidi ya aliyo nayo?
 
hii thread iko ki-hisia ziadi kuliko uhalisia na wengi hamuijui chadema hasa mleta thread ameonyesha chembe nyingi mapungufu katika thread yake....

sihitaki kuijua CHADEMA...
nazungumza maoni yangu kama mtanzania..
CHADEMA ni chama mali ya watanzania wote....
hata ambao sio wanachama.ruzuku zao ni kodi zetu wote..
na wapo kwa mujibu wa sheria za vyama Tanzania..
 
Hata wao (Waarabu) walikuwa Kondoo ndio maana yule fisadi Mubarak aliweza kukaa madarakani zaidi ya miaka 30 na chaguzi za kishkaji huku akiendelea kukwapua mabilioni ya dollars za misaada toka US. Watu wakisema sasa basi liwalo na liwe basi hakuna wa kuwazuia. Kama walivyoweza Wamisri na Watanzania pia tunaweza kabisa...YES WE CAN!!!

Wamisri walikuwa na sababu moja ya kumtoa Mubarak madarakani ambayo ni kukaa kwake madarakani kwa muda mrefu. Sababu hiyohiyo ndiyo iliyokuwa nyuma ya maandamano mengine kwenye nchi za kiarabu. Hapa hakuna sababu ya msingi inayoweza kuunganisha umma kuwa na sauti moja kuipinga serikali. Kwahiyo usitarajie eti siku moja watanzania wataandamana kuitoa serikali yao madarakani, hizo ni ndoto tu.
 
Hakuna sehemu niliyosema ku 'compromise ' ni kuwa double agent..
ku 'compromise ni mfano wa Zitto ambae
jimbo lake 'vitu kama barabara na shule'
vimepatikana wakati ni serikali ya ccm 'imewezesha'
na yeye alikiri na kukataa kushiriki kutoka nje wakati Kikwete anahutubia bunge...
na sasa anaonekana ni 'msaliti'...

huwezi kuwa mpinzani 'ukawajengea barabara jimboni mwako'
lazima uka 'lobby' na ku 'lobby ni ku 'compromise'
elewa siasa inavyochezwa...

mkuu kuna mambo mengi huyajui ndani ya chadema kwa ujumla na hasa linapokuja swala la zitto ndani ya chadema naona kwako liko next level.....huijua chadema na viongozi wake..thread yako umeiaharibu hasa sentensi yako ya kwanza(age-gap) na aya ya mwisho unapozungumzia mambo ya kaskazini na familia....
 
.........sure! Kitila
Mnyika hajakomaa kisiasa.

Kwanza tuone kazi on the ground.

Ubungo jimbo nalifahamu vyema.Ayashughulikie matatizo waliyonayo na kusukuma gurudumu la manedeleo hapo jimboni.

Ndivyo hivyo chama kina win hearts and minds.

Tatizo wengi wanatumia ubunge kujijenga wao binfasi na pia kisiasa.
 
Kwani lazima awe anatoka Bungeni?

Na kama wenziwe wana F kwa vigezo vyako, tumchukue yeye anaekaribia F na kumuondoa kiongozi anaekubalika kwa kuwa tu yeye si F?

kwa ni ni wewe usiseme yupi ni better?
mimi nimesema ndani ya CHADEMA yeye ni better...wewe unasema yupi?????
 
sihitaki kuijua CHADEMA...
nazungumza maoni yangu kama mtanzania..
CHADEMA ni chama mali ya watanzania wote....
hata ambao sio wanachama.ruzuku zao ni kodi zetu wote..
na wapo kwa mujibu wa sheria za vyama Tanzania..

ni kweli ni maoni yako na ndio maana hayana mpangilio na yamejaa upotoshaji
 
mkuu kuna mambo mengi huyajui ndani ya chadema kwa ujumla na hasa linapokuja swala la zitto ndani ya chadema naona kwako liko next level.....huijua chadema na viongozi wake..thread yako umeiaharibu hasa sentensi yako ya kwanza(age-gap) na aya ya mwisho unapozungumzia mambo ya kaskazini na familia....

wewe ndo hunielewi kabisa
hakuna sehemu niliposema ZITTO AU SLAA hawafai
nimesema MNYIKA NI BETTER....
kwa sababu 'hana political garbage' ambazo wengine wanazo
 
Wamisri walikuwa na sababu moja ya kumtoa Mubarak madarakani ambayo ni kukaa kwake madarakani kwa muda mrefu. Sababu hiyohiyo ndiyo iliyokuwa nyuma ya maandamano mengine kwenye nchi za kiarabu. Hapa hakuna sababu ya msingi inayoweza kuunganisha umma kuwa na sauti moja kuipinga serikali. Kwahiyo usitarajie eti siku moja watanzania wataandamana kuitoa serikali yao madarakani, hizo ni ndoto tu.

Mkuu soma alama za nyakati. Kuna sababu nyingi tu Tanzania za kuitoa Magamba madarakani na ndio maana sasa hivi tunaona mavarangati yakizidi kuongezeka katika kona mbali mbali za nchi yetu na mimi nakuhakikishia kwamba kama hakutakuwa na mabadiliko ya kweli basi vurumai hizi zitazidi kuongezeka kila kukicha. Si kweli kwamba nchi yetu ni maskini. Tuna utajiri wa kutosha kabisa kuweza kufanya nchi yetu kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika lakini kutokana na kuwa na hawa wanaojiita viongozi ambao hawana vision na wenye uroho wa utajiri wa haraka haraka hatuoni maendeleo yoyote ya kweli bali tunachokiona na hao wanaojiita viongozi kushindana nani ni tajiri mkubwa kuliko mwenzie na hawa "wachukuaji" wenyewe wanajiita "Wawekezaji" wanakuja maskini kuvuna utajiri wetu na kuondoka matajiri na huku Watanzania tukiona hakuna mafanikio yoyote yale kutokana na utajiri wetu huo wa asili.

Kama wewe huzioni sababu za kumtoa Kikwete madarakani basi huo ni mtazamo wako lakini sababu hizo ziko nyingi sana. Hakuna yoyote yule aliyedhania miaka mitano iliyopita kwamba Wamisri wataungana tena bila silaha na kumtoa Mubarak madarakani dhana kama hiyo miaka mitano iliyopita ilionekana ni ndoto tu. Kwahiyo hata hii ndoto kama unavyoiona wewe inaweza ikawa kweli baada ya miaka michache ijayo. Usicheze na nguvu ya umma Mkuu.

Ukifuatilia matatizo meengi ya nchi hii
utakuta tatizo la 'age gap' kati ya viongozi wanaotawala na wananchi..

zaidi ya nusu ya watanzania ni 'below 30 years old...inasemekana almost 60
au 75 percent ya watanzania umri ni below 35
na ukichukua below 40 unaweza kukuta ni almost 65-80 percent....
mwenye accurate data
tafadhali aweke hapa.......

sasa basi mimi kwa maoni yangu naona viongozi kama Zitto,Mnyika,January,Kafulila na wengineo vijana
angalau wana 'advantage' ya kuwa connected na masula hasa ambayo viongozi
kama Kikwete na wazee wenzake wengi hawaelewi kabisa...
kuna a 'A BIG DISCONNECTION' kati ya wananchi na wazee kwa hakika...

Mimi ningependa Zitto awe mwenyekiti CHADEMA....lakini
ameshaanza kuwa 'na wapinzani wengi' ndani ya CHADEMA itakuwa ngumu kwake kupata
Uenyekiti au 'legitimacy' inayohitajika pengine kwa sasa....

sasa nilipomuangalia John Mnyika jinsi alivyoendesha kampeni ya ubungo
bila 'kumjeruhi' Julius Mtatiro na jinsi 'anavyo perfom bungeni now'
pamoja na kutomkubali huko nyuma,ameni convince now kuwa 'he is a better leader'
kulinganisha na wengine ndani ya CHADEMA....

1.Sifa ya kwanza ni 'uniter'..ataweza kuunganisha CHADEMA na vyama vingine.

2.Sifa ya pili anapenda 'dialogue' kuliko 'maandamo'....

3.Sifa ya tatu ambayo mimi naona ni muhimu mno now ni age...
ata 'connect' na wananchi ambao wengi ni vijana
yuko engaging na watu....

4.hana 'political garbage' ya aina yeyote for now...haitaji kulipa fadhila kwa yeyote
yuko free kufanya maamuzi kwa jinsi anavyoona,ana uwezo wa kuwa 'ndependent'
kimawazo...

na sifa zingine nyingi kumlinganisha na wengine......

now its time,tukisubiri 'azeeke' atakuwa 'corrupt' na mazoea na culture za siasa za makundi

Chadema wafanye kama DEMOCRATS walivyofanya kwa OBAMA....

mimi nafikiri its time Mnyika awe Mwenyekiti,CHADEMA itawasaidia
1.hoja ya uchagga na ukaskazini
2.hoja ya chama cha familia...

na hoja zingine...nyiingi....Urais anaweza kugombea SLAA au yeyote but Mnyika awe Mwenyekiti....
Mimi ni mchagga lakini hakuna mchagga wa huko nilikotoka ambaye ana madaraka hapo chadema.

Tatizo ni kwamba hamtujui wachagga na hiyo imekuwa shida kubwa sana kwa watanzania wenzetu wengi.
Fuatilia mkuu.
 
Wamisri walikuwa na sababu moja ya kumtoa Mubarak madarakani ambayo ni kukaa kwake madarakani kwa muda mrefu. Sababu hiyohiyo ndiyo iliyokuwa nyuma ya maandamano mengine kwenye nchi za kiarabu. Hapa hakuna sababu ya msingi inayoweza kuunganisha umma kuwa na sauti moja kuipinga serikali. Kwahiyo usitarajie eti siku moja watanzania wataandamana kuitoa serikali yao madarakani, hizo ni ndoto tu.

Ningependa nikwambie huko Misri,Tunisia,Libya na hizo nchi nyingine za Kiarabu moto unaowaka siyo kuwaondoa watawala wao tu bali vyama vyao na mfumo wa utawala wa kifisadi na kidikteta. Watanzania wataungana kuiangusha CCM na mfumo wake wa kifisadi.
 
Hakuna sehemu niliyosema ku 'compromise ' ni kuwa double agent..
ku 'compromise ni mfano wa Zitto ambae
jimbo lake 'vitu kama barabara na shule'
vimepatikana wakati ni serikali ya ccm 'imewezesha'
na yeye alikiri na kukataa kushiriki kutoka nje wakati Kikwete anahutubia bunge...
na sasa anaonekana ni 'msaliti'...

huwezi kuwa mpinzani 'ukawajengea barabara jimboni mwako'
lazima uka 'lobby' na ku 'lobby ni ku 'compromise'
elewa siasa inavyochezwa...

Boss ninapenda ukielewe, chochote kile ambacho serikali itakifanya cha kimaendeleo sio hisani ni wajibu wake na ndio waliomba ajila ili wayafanye hayo, na usisahau hizo ni kodi zetu wenyewe.
 
Acheni hizo; mnyika anafaa kuwa katibu na si mwenyekiti wa chadema. Mtu potential kwa uenyekiti ni zitto kabwe. Tuache majungu vijana na tuangalie mbele. Kwanza zitto ana elimu nzuri sana na anaelewa fika wapi pa kuipeleka chadema. Zitto anahitaji tu kufundwa na akina mbowe, slaa, kitila, tundu, safari na wengineo. Na mimi nawaambieni kabisa; zitto ni mtu muhimu sana kwa future ya chadema. Tuache mambo ya mkumbo kwa kumuhukumu mtu kwa mambo ambayo si ya uhakika. Wanachadema mngejaribu sana kufikiria namna ya kujenga chama na si kupikiana majungu humu.na msipokuwa makini, sisi wana-ccm tutazidi kuwachanganya ili muone zitto hafai lkn tunajua zitto ni tishio kwetu kwa sasa na hata baadaye.hayo ni mawazo yangu tu.

ukisoma vizuri utagundua my first choice ni Zitto
lakini kama kuna watu wanamuona 'msaliti' na hawamtaki
basi my second choice ni MNYIKA.....
NA sasa anakuwa First choice kulinganisha na MBOWE NA SLAA..
all in all uchaguzi uwe wa haki tu,yeyote kati yao is better kuliko SLAA AU MBOWE...
 
Mimi ni mchagga lakini hakuna mchagga wa huko nilikotoka ambaye ana madaraka hapo chadema.

Tatizo ni kwamba hamtujui wachagga na hiyo imekuwa shida kubwa sana kwa watanzania wenzetu wengi.
Fuatilia mkuu.

Ahsante sana Mkuu. Mie nawahusudu sana Wachagga na nina bahati kubwa sana ya kuelewana nao kupita kiasi, labda nina damu yao kiasi hahahaha lol!
 
Boss ninapenda ukielewe, chochote kile ambacho serikali itakifanya cha kimaendeleo sio hisani ni wajibu wake na ndio waliomba ajila ili wayafanye hayo, na usisahau hizo ni kodi zetu wenyewe.

kweli kabisa lakini wana uhuru wa kutokufanya pia...
sawa???
 
Mimi ni mchagga lakini hakuna mchagga wa huko nilikotoka ambaye ana madaraka hapo chadema.

Tatizo ni kwamba hamtujui wachagga na hiyo imekuwa shida kubwa sana kwa watanzania wenzetu wengi.
Fuatilia mkuu.

mkuu kwenye politics
'image na reputation' ni kila kitu..
ishu sio ukweli,ishu ni nini watu wanaamini kuwa ni 'ukweli'
 
Back
Top Bottom