John Mnyika amuita Rais kikwete Dhaifu, atolewa nje ya Ukumbi wa Bunge!

Kwa hakika huhitaji kisomo chochote kuona udhaifu mkubwa wa URAIS WA AWAMU YA NNE wa Tanzania.Kwa hasara ya kukosa uwepo wa KOMANDOO MNYIKA kwenye mjadala,kwa kuwa tunajua makomandoo waliobaki watafanya kazi kusudiwa vizuri bila kujali uchache wao NA UWEPO WA REFARII AMBAYE AMEVAA JEZI YA CCM, ni vizuri neno hilo likabaki kwenye HANSARD!bravo JOHN!
 
Mimi nitaipenda CCM kwa dhati kama itatokea kuwa na mbunge mzalendo kama JJ Mnyika.Tungepata wakunge kama wa CDM tungekuwa mbali sana.
 
Kwani uwongo kwamba Kikwete ni dhaifu? Swala la Jairo limeishia wapi kama sio udhaifu wake na serikali yake? Magamba yote ni dhaifu. Mnyika juuuuuuuuu......
 
Namsifu Mnyika kwa kukubali kutolewa nje kwa kusimamia kauli yake kuwa Kikwete ni dhaifu na CCM na wabunge wake ni wazembe na machizi. Kweli Ubungo wanajembe la ukweli.
 
Amesema kitu ambacho hata wao wanajua kuwa kikwete ni dhaifu ila huwa wanauficha udhaifu wake kwa kusema kuwa wasaidizi wake ndio wanomwangusha
 
Unajua nchii hii lazima tufikie sehemu watu waambiwe ukweli.
Ila napata shida na heshima ya kiti cha spika. Jana hotuba ya upinzani imetupwa kwa aibu na kiti kilikaa kimya.

Lakini Mnyika kesho si anarudi asubuhi, watamfukuza kila siku maana kiti cha spika kinashindwa kuregulate na kubalance mijadala.

Wakitoa lugha ya kuudhi wana CCM hakuna mwongozo, ila upinzania ndo Lukuvi na kiti cha spika kinasimama.
Shame on this bunge, Shame on this government.
 
Upo ukweli katika hili si bure jamani tusimhukumu Mnyika kwa kusema ukweli. Yako mambo mengi yanayoonyesha kuwa yu dhaifu si kwakulalamika la.
1. Swala la Uamsho huko zanzibar kutaka kuvunja Muungano Ukiwa kama Rais wa nchi unatakiwa kutoa tamko
linaloonyesha uyumbishwi.
2. Ukiwa kama rais uoni makosa mpaka Bunge likusemee kuwa litamwajibisha waziri mkuu ndio unachukua atua.
3. Wezi wanaiba rasilimali zetu kupitia mbuga za wanayama na kwingine kimya ....
nk mengi sana
 
Safi mnyika naungana na wewe ni kweli tumefikishwa hapa na udhaifu wa rais kikwete,pia na baadhi ya wabunge na bunge lenyewe mwisho kabisa na upuuzi wa ccm!
 
Alienda Ikulu kunywa kahawa na juisi ya ukwaju, kwa huyo huyo Rais wa Watanzania wote.

Mnyika kashindwa kuwahudumia watu wa Ubungo anatafuta umaarufu.
Yaani we hujui tu............kile kitendo kimeamsha shangwe noumer i wish ungekuwepo hapa nilipo, hayo ya juisi tuyaache kwanza kwani kama ni Rais wetu wote si kila mtanzania anastahili kupata kinywaji ikulu?
 
Back
Top Bottom